Bado najiuliza: Nini hasa chanzo cha Lowassa kuwa na ushawishi kwa watu?

Bado najiuliza: Nini hasa chanzo cha Lowassa kuwa na ushawishi kwa watu?

Ushawishi wake umetokana na kundi lake. ukihusisha wengine wenye ushawishi hatari akiwemo Membe, kinana na wengine. Fuatilia uchaguzi uliompitisha Mkapa kuwa mgombea ulikuwa na upinzani gani na speech ya JK iliyomsimamisha Nyerere akapiga makofi kwa furaha. Uliokuwa Mtandao wa JK karibu wote wana ushawishi.
 
Shida ya wabongo wengi ni unafiki hata hamza alibeba umaarufu na kila mtu kujifanya anamjua wakati hata alipokuwa anakaa hawapajui.

Tena nilicheka zaidi kuona watoto wa 2003 wanalia kabisa na kugara gara barabarani siku aliyokufa mkapa wakati hata kweny utawala wake hawakuwepo
😀😀
Wabongo wafuata Mkumbo sio
 
Uwanja huo ulijengwa na askari mstaafu wa Uingereza Colonel Middleton kabla ya Uhuru na kuuruthisha kwa iliyokuwa Arusha Town Council.
Sasa wakaja Mafisiemu wakautaifisha na mwaka 1976 wafanyakazi wote,wafanya biashara wote tulichangishwa kwa nguvu kuujengea badhi ya majukwa na kweli wanafunzi wa secondary walifanyishwa kazi bure.
Leo mzee wangu umenifumbulia fumbo kubwa sana maishani mwangu. Nilikuwa sijui kwanini hiyo barabara toka stendi hadi Mianzini hadi stendi inaitwa Col. Middleton ndo leo nimejua. Baba yangu alisoma Ilboru alimaliza kidato cha nne mwaka 1978. Kuna siku nilimsikia akiongelea ishu ya uwanja ila alikuwa akiongea na mgeni na kama unavyojua ambacho kingenikuta kwa kuingilia mazungumzo ya watu wazima... hivyo nikakausha na sikuwahi kumuuliza tena.
 
Poleni kwa Msiba Wakuu!

Kikawaida ni kawaida watu wenye midomo, makelele na makeke kuwa na ushawishi kwa watu.

Mfano, ushawishi wa Tundu Lisu ni Makeke na mdomo kwa kujua kupepeta hoja zikapepeteka.
Ushawishi wa JPM ni makeke, kukandia wengine na uchapakazi.

Ushawishi wa Dkt. Slaa pia ni kupepeta mdomo.

Ushawishi wa Makonda ni makeke na kupepeta mdomo.

Sasa kwa Lowasa ni nini msingi wa ushawishi wake kwa Watu ukizingatia karba na tabia yake niya ukimya na sio mtu wa maneno mengi.

Au ndio tunaita Nyota?
Wenye kujua mtupe ufafanuzi. Au labda miaka ya ujanani ambapo wengi hatukuwepo alifanya jambo fulani ambalo ndilo mpaka leo limempa heshima na ushawishi mbele za watu?

Karibuni
Una miaka mingapi?
 
Anhaa!
Unajua tangu nipate akili sidhani kama kuna mwanasiasa tangu nchi ipate uhuru alikuwa na ushawishi kama Lowasa.
Wengi wanakuwa na ushawishi wakiwa ndani ya mfumo iwe wa ccm au serikali. Wakitoka wanakwama
Augustino Lyatonga Mrema alitikisa nchi zaidi yake.
 
Hakuna cha uchawi,nyota, ushawishi wala nini, bali [emoji117]kipindi lowasa anagombea urais nchi ilikuwa imetoka ktk uongozi wa hovyo(CCM) ambao wanachi walishauchoka, hivyo kuamua liwalo na liwe bora kumchagua yeyote ambaye yuko kinyume na uongozi wa CCM.

Karibu kila mtu kipindi hicho alikuwa kinyume na utawala wa kikwete pamoja uongozi wake, kuchokwa kwa utawala huo ndio jambo lililofanya wengi wahamie upande wa kusapoti upinzani, the same way kama ilivyokuwa 2010 kwa Dr Slaa alivyopita na nyomi la wafuasi wengi waliochoshwa na utawala wa CCM, hapo hakuna cha uchawi,dawa wala mvuto bali uhalisia wa maisha unaowafanya watu kuchoshwa na aina ya mfumo na kuamua kuhamia/kutamani mfumo wa upande wa pili(upinzani).

Ndiomaana baada ya lowasa kushindwa, matumaini ya walioupinga mfumo wa ccm yalirudi baada ya kuona kumbe kuna matumaini hata huko CCM pale Magufuri alipobadili mfumo mzima wa kipuuzi huko CCM, hapo ndipo hata baadhi ya wapinzani walianza kumsapoti na hata wale waliokuwa wamechoshwa na utawala wa CCM kabla ya 2015 walirudisha matumaini.

Sio hadithi, sio stories, haya mliyashuhudia wenyewe baada ya magufuri kuapishwa tu alipoanza ziara za kushitukiza, kutumbua wazembe/wala rushwa, kuinua maisha ya walala hoi, kupambana na wakwepa kodi, haya aliyafanya ndani ya muda mfupi jambo lililorudisha matumaini kwa Watanzania.

Suala la Lowasa kuwa na wafuasi wengi lilitokana na Raia kuchoshwa na utawala wa kihuni wa CCM ndiomaana wakatamani na kushawishika na upande wa Upinzan wakifikili kutakuwa na unafuu au kutaman Uongozi mpya nje ya CCM.

Simple hakuna uchawi hapo ni suala tu la mifumo kupoteza direction.

Hata wewe hapo leo hii ukipata pesa hata kama ni domo zege utashangaa sana utakavyokuwa chambo/asali ya warembo na utajiuliza haya mambo kwanini hayakuwepo kipindi hauna hela? Jibu ni kuwa watu wanafuata kitu ambacho ni bora, kitu ambacho kwa wengine hakipo.
 
Anhaa!
Unajua tangu nipate akili sidhani kama kuna mwanasiasa tangu nchi ipate uhuru alikuwa na ushawishi kama Lowasa.
Wengi wanakuwa na ushawishi wakiwa ndani ya mfumo iwe wa ccm au serikali. Wakitoka wanakwama
Acha zako wew lowasa anamfikia nyerere?, anamfikia magufuri? Suala la mvuto na ushawishi mnaweza kuliona hata hapa baada ya msiba ni akina nan na wangapi watakao umia/kuhuzunika baada ya kifo, lowasa ni mtu wa kawaida sana nje na ndan ya siasa mnampa sifa zisizo stahili, ni wakawaida sana hafiki hata kwa dr slaa/tundulisu au hata kwa yule kahaba wa instagram anayeandamanisha raia wa nchi nzima kwa Posts zake, wakati huo yeye akiwa USA na wapuuzi wakiwa TZ.

Angalieni uhalisia na sio uongo.
 
Somo la Maadili lipewe kipaumbele vijana hawana maadili. Unawezaje kusema wazee umri wa babayako eti wana "pepeta mdomo"??
Tundu LISSU amesaidia haki kwa wengi na kupinga uozo serikalini Leo unasema anapepeta mdomo eti watu wachangie hoja yakijinga isiyo na adabu.
 
Mkuu hao uliowataja bila ccm hawatoboi.
Ni kama nguvu ya mamba kumaji
 
Somo la Maadili lipewe kipaumbele vijana hawana maadili. Unawezaje kusema wazee umri wa babayako eti wana "pepeta mdomo"??
Tundu LISSU amesaidia haki kwa wengi na kupinga uozo serikalini Leo unasema anapepeta mdomo eti watu wachangie hoja yakijinga isiyo na adabu.

Kwenye siasa hayo ni mambo ya kawaida.
Labda ungesema kuwa ni uongo hawapepeti mdomo.
 
Wakati ni Waziri mkuu alikua mchapakazi mzuri tu, kama Jpm kulikua na tumbua tumbua na safisha safisha serikalini,

Pia anakubalika na "Elites" wa Nchi, Kumtoa kingunge CCM si kazi ndogo, unapikubalika na Elites, wale Elites wanakuwa na followers wao ambao wanaweza wasikukubali ila sababu wewe ni kiongozi wa watu wanaokukubali inabidi na wewe wakukubali for the time being. Mfano hapa Jf chawa wa Samia sio wote ni Loyal kwa Samia, Bali sababu tu mabosi zao wapo chini ya Samia na wao inabidi wamsifie.
Haya nayaona kama ndo majibu sahihi.
 
Poleni kwa Msiba Wakuu!

Kikawaida ni kawaida watu wenye midomo, makelele na makeke kuwa na ushawishi kwa watu.

Mfano, ushawishi wa Tundu Lisu ni Makeke na mdomo kwa kujua kupepeta hoja zikapepeteka.
Ushawishi wa JPM ni makeke, kukandia wengine na uchapakazi.

Ushawishi wa Dkt. Slaa pia ni kupepeta mdomo.

Ushawishi wa Makonda ni makeke na kupepeta mdomo.

Sasa kwa Lowasa ni nini msingi wa ushawishi wake kwa Watu ukizingatia karba na tabia yake niya ukimya na sio mtu wa maneno mengi.

Au ndio tunaita Nyota?
Wenye kujua mtupe ufafanuzi. Au labda miaka ya ujanani ambapo wengi hatukuwepo alifanya jambo fulani ambalo ndilo mpaka leo limempa heshima na ushawishi mbele za watu?

Karibuni

Nafikiri aliloga, maana sasa unakubali ushawishi alikuwa nao, na unaamini astahili, basi alienda kwa waganga kutafuta ushawishi.
 
Huo ukimya wake ndio uliosababisha watu wampende, hasa nikikumbuka kile alichofanyiwa na rafiki yake JK ndicho kilichosababisha wengi waone ameonewa hajatendewa haki.

Hivyo wakaamua kumuunga mkono kwenye kampeni zake za kuusaka urais, kwa yake mafuriko makubwa ya watu mikoa yote Tanzania Bara ambayo hayajawahi kufikiwa na mgombea mwingine yeyote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
View attachment 2899914
Tabia za Lowasa na Kikwete zinafanana.
Roho mbaya zinazocheka na kuvutia. Makatili wanaofurahisha.
Wote ni wezi wanaolisha na kushibisha wengine.

Inasemekana Lowasa ndiye aliyemwaga mkwanja kuhakikisha JK anashinda uchaguzi, ingawa JK hakurudisha fadhila na ndio ukawa mwisho wa urafiki wao mpevu ever.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Poleni kwa Msiba Wakuu!

Kikawaida ni kawaida watu wenye midomo, makelele na makeke kuwa na ushawishi kwa watu.

Mfano, ushawishi wa Tundu Lisu ni Makeke na mdomo kwa kujua kupepeta hoja zikapepeteka.
Ushawishi wa JPM ni makeke, kukandia wengine na uchapakazi.

Ushawishi wa Dkt. Slaa pia ni kupepeta mdomo.

Ushawishi wa Makonda ni makeke na kupepeta mdomo.

Sasa kwa Lowasa ni nini msingi wa ushawishi wake kwa Watu ukizingatia karba na tabia yake niya ukimya na sio mtu wa maneno mengi.

Au ndio tunaita Nyota?
Wenye kujua mtupe ufafanuzi. Au labda miaka ya ujanani ambapo wengi hatukuwepo alifanya jambo fulani ambalo ndilo mpaka leo limempa heshima na ushawishi mbele za watu?

Karibuni
Mkuu Robert Heriel Mtibeli kuna watu wanazaliwa ili kuwa viongozi na wanaujua Uongozi

Miongoni mwao ni Edward Lowassa
 
Augustino Lyatonga Mrema alitikisa nchi zaidi yake.
Mimi nilikuwepo wakati wa kampeni za 1995

Augustiono E. Mrema hakufikia alichofanya E. Lowassa kwasababu Lowassa alikuwa sababu ya vijana wengi sana kupata ubunge na power...Mrema hakufanya hivyo
 
Back
Top Bottom