Hakuna cha uchawi,nyota, ushawishi wala nini, bali [emoji117]kipindi lowasa anagombea urais nchi ilikuwa imetoka ktk uongozi wa hovyo(CCM) ambao wanachi walishauchoka, hivyo kuamua liwalo na liwe bora kumchagua yeyote ambaye yuko kinyume na uongozi wa CCM.
Karibu kila mtu kipindi hicho alikuwa kinyume na utawala wa kikwete pamoja uongozi wake, kuchokwa kwa utawala huo ndio jambo lililofanya wengi wahamie upande wa kusapoti upinzani, the same way kama ilivyokuwa 2010 kwa Dr Slaa alivyopita na nyomi la wafuasi wengi waliochoshwa na utawala wa CCM, hapo hakuna cha uchawi,dawa wala mvuto bali uhalisia wa maisha unaowafanya watu kuchoshwa na aina ya mfumo na kuamua kuhamia/kutamani mfumo wa upande wa pili(upinzani).
Ndiomaana baada ya lowasa kushindwa, matumaini ya walioupinga mfumo wa ccm yalirudi baada ya kuona kumbe kuna matumaini hata huko CCM pale Magufuri alipobadili mfumo mzima wa kipuuzi huko CCM, hapo ndipo hata baadhi ya wapinzani walianza kumsapoti na hata wale waliokuwa wamechoshwa na utawala wa CCM kabla ya 2015 walirudisha matumaini.
Sio hadithi, sio stories, haya mliyashuhudia wenyewe baada ya magufuri kuapishwa tu alipoanza ziara za kushitukiza, kutumbua wazembe/wala rushwa, kuinua maisha ya walala hoi, kupambana na wakwepa kodi, haya aliyafanya ndani ya muda mfupi jambo lililorudisha matumaini kwa Watanzania.
Suala la Lowasa kuwa na wafuasi wengi lilitokana na Raia kuchoshwa na utawala wa kihuni wa CCM ndiomaana wakatamani na kushawishika na upande wa Upinzan wakifikili kutakuwa na unafuu au kutaman Uongozi mpya nje ya CCM.
Simple hakuna uchawi hapo ni suala tu la mifumo kupoteza direction.
Hata wewe hapo leo hii ukipata pesa hata kama ni domo zege utashangaa sana utakavyokuwa chambo/asali ya warembo na utajiuliza haya mambo kwanini hayakuwepo kipindi hauna hela? Jibu ni kuwa watu wanafuata kitu ambacho ni bora, kitu ambacho kwa wengine hakipo.