BAKWATA wana ushwawishi na nguvu kubwa kuliko TEC katika siasa za nchi

BAKWATA wana ushwawishi na nguvu kubwa kuliko TEC katika siasa za nchi

BAKWATA hawasumbuani na mtawala yoyote, licha ya mapungufu waliyonayo BAKWATA. Na TEC hawakumpinga Magufuli kama walivyompinga Mzee Mwinyi (Allah Amrehemu), Mzee Kikwete na sasa hivi wanavyompinga Mama Samia.

Kuna Screenshot moja ilikuwa inasambaa inaonesha post ambayo mtu kaweka idadi ya matamko TEC wameyatoa kwa kila Rais, siko nayo ila hadi humu Jf niliwahi kuiona. Ninachokikumbuka kutoka mule ni kuwa TEC hawajawahi kutoa tamko lolote wakati wa utawala wa Nyerere, katika miaka yote ambayo Mzee Nyerere katawala, hakuna tamko hata moja dhidi yake. Na ukiangalia kwa marais Waislam wametoa matamko mengi kuliko kwa marais wasio Waislam.

Kusema TEC walimpinga sana Magufuli kwa kumlinganisha na nani?

Ukweli ni kwamba TEC wanapenda kuwasakama Marais Waislam.


BAKWATA siku zote hawasumbuani na watawala.
ALAAA! wewe na huyo mwenzio kumbe mpo humu mkifanya kazi hii?
Nyinyi ni 'foot soldier'', au ndio wale "mbwa mwitu wa Mwaipopo mmesambazwa hadi huku?

"BAKWATA hawasumbuani na mtawala yeyote", sasa ndiyo maneno mnayoyatanguliza mbele kwa kutumia ulaghai ule ule unaotumiwa na Samia na Genge lake lote zima?

Huu utamaduni wa kiutawala wa falma za kiarabu hautafanya kazi hapa. Na huo ndio ujinga wanaoutumia BAKWATA; lakini sina hakika kama unayo akili ya kutosha kuelewa ninachokueleza hapa kuhusu utamaduni huo.
 
Ungekuwa na akili huru tayari ungejuwa kwamba wewe ni mmoja wao; unatazama maswala ya nchi katika mawani hayo hayo ya udini; na kundi hili limekuwepo miaka yote okea enzi za uhuru. Bila shaka wewe ni mhitimu wa chuo cha Kariakoo kinachofundisha haya mambo, au siyo?


Hujui kwa nini BAKWATA iliundwa na kuwa sehemu ya CCM, tokea wakati huo?
Na bado hujui kwamba ni hao hao BAKWATA sasa hivi wametekwa na kundi lilelile la tokea enzi za kudai uhuru?

Sasa unataka kujifanya hujui njia za ulaghai zinazotumiwa huko BAKWATA; njia zile zile anazotumia Samia; na unasubiri BAKWATA watoe matamko ndipo ujue kazi zao wanazifanya kimya kimya huku matokeo yakionekana na wala hujui kuyatafsiri kwa vile tu wewe ni mmoja wao!

Hizi akili za kijinga mnazileta kuvuruga taifa hili halafu mnajifanya hamjui chochote.

Wewe nilikutambua toka mwanzo, pamoja na kwamba hujitoi waziwazi kuwa mtetezi wa uovu huu unaofanyika sasa chini ya Samia.



Mimi ni Muislam wala sijifichi. Na ninasimama na Dini yangu. Actually kwa mujibu wa Dini yangu haifai kuutoa mkono wangu wa utiifu kwa mtawala Muislam na hata kwa mtawala asiye Muislam, tumekatazwa kumtoa kama kumtoa kutapelekea madhara makubwa zaidi. Hivyo tumeamrishwa kumtii mtawala katika yasiyo haramu.

Hivyo katika hii Nchi, hata Rais akiwa sio Muislam nitamtii na kumsikiliza katika yasiyo maasi, akiwa Muislam ndio kabisaaa, hata kama mtawala huyo atakuwa ni muovu.

Na tumekatazwa katika Dini yetu kuwasema vibaya watawala hadharani, na tukaambiwa tukitaka kumnasihi mtawala tumnasihi kwa siri au tumuandikie yeye mtawala mwenyewe kwa siri. Yaani mtu kama mimi nikitaka kumnasihi mtawala nisubiri mpaka nimuone uso kwa macho nikipata hiyo fursa sasa ndio nimnasihi uso kwa uso kwa siri yeye mwenyewe akinisikia au nimuandikie kwa siri kama ni barua iende kwake aisome. Kama sijapata hiyo fursa natakiwa kuwa na subra hata kama mtawala atakuwa anadhulumu. Tunatakiwa kuwa na subra na kumtii mtawala katika yasiyokuwa maasi. Na sio kumsema hadharani.

Hili nalitangaza humu na wala sifichi. Mimi ni Muislam na ninaifuata Dini yangu na ninalitangaza hili.


So usijifanye kuwa mimi nina ajenda fulani ya siri ambayo wewe umeigundua unani expose.


Halafu BAKWATA hata kama ilianzishwa na Mzee Nyerere (unaficha ficha eti CCM) mwaka 1968, bado wale ni ndugu zetu, ni Waislam, na licha ya mapungufu yao mengi, wao bado ni Ndugu zetu Waislam na tunawaombea Allah Awaongoze wao na sisi.

Pia, miaka yote msimamo wa BAKWATA hawasumbuani na watawala. Wako hivyo, licha ya mapungufu yao yote.

Na mwisho, jambo la ubaguzi, chuki na kuwapiga vita Waislam na Dini yao lipo hapa tokea wakati wa ukoloni na hata baada ya uhuru licha ya kuwa Waislam walisimama kidete kupigania uhuru wa Nchi hii. Ila wamebaguliwa na wanapigwa vita sana sana humu na imefanywa namna imeonekana kama ni kawaida Waislam kupigwa vita humu.

Ila Waislam tuko na Subra na Masheikh zetu wanatuusia Subra na utulivu na hata pale baadhi yetu wanapokuwa na jazba masheikh zetu huwatuliza na kuwakumbusha Mafundisho sahihi ya Dini yao.

Kuna watu wanahisi Waislam ni raia wa daraja la chini hapa Tanzania na wanachukulia hivyo na wanahisi hiyo ni status quo inayopaswa kulindwa. Na hilo linadhihiri hata rais akiwa Muislam; atawekewa mashinikizo, atatikiswa na kusumbuliwa ili kumrudisha katika "nafasi yake" kama Muislam na ajue nani Bosi.

Baadhi yetu tumegundua namna marais Waislam wanavyokuwa intimidated.

Na hili sio sawa.

Hili ni jambo lenye mizizi mirefu ambayo asili yake ni kuwapiga vita Waislam na Uislam.
 
Mimi ni Muislam wala sijifichi. Na ninasimama na Dini yangu. Actually kwa mujibu wa Dini yangu haifai kuutoa mkono wangu wa utiifu kwa mtawala Muislam na hata kwa mtawala aside Muislam, tumekatazwa kumtoa kama kumtoa kutapelekea madhara makubwa zaidi. Hivyo tumeamrishwa kumtii mtawala katika yasiyo haramu.
Hayo kaa nayo mwenyewe hakuna atakayekusumbua katika Tanzania ya watu wote wanaoamini hayo yako na wasioyaamini.
Weka Tanzania mbele siyo hayo yako mwenyewe..
 
ALAAA! wewe na huyo mwenzio kumbe mpo humu mkifanya kazi hii?
Nyinyi ni 'foot soldier'', au ndio wale "mbwa mwitu wa Mwaipopo mmesambazwa hadi huku?

"BAKWATA hawasumbuani na mtawala yeyote", sasa ndiyo maneno mnayoyatanguliza mbele kwa kutumia ulaghai ule ule unaotumiwa na Samia na Genge lake lote zima?

Huu utamaduni wa kiutawala wa falma za kiarabu hautafanya kazi hapa. Na huo ndio ujinga wanaoutumia BAKWATA; lakini sina hakika kama unayo akili ya kutosha kuelewa ninachokueleza hapa kuhusu utamaduni huo.


Mwaipopo sio Sheikh wangu na wala simchukulii kuwa ni Sheikh, bali Mwaipopo sio Sheikh kabisa. Na wala mimi sipo katika kundi lake la hao sijui mbwa mwitu.

Pili, ni kweli au uongo kuwa BAKWATA licha ya mapungufu yao yote, hawasumbuani na mtawala yoyote anayetawala Nchi hii? Nitajie hata mtawala mmoja ambaye BAKWATA waliminyana naye.




Huu utamaduni wa kiutawala wa falma za kiarabu hautafanya kazi hapa. Na huo ndio ujinga wanaoutumia BAKWATA; lakini sina hakika kama unayo akili ya kutosha kuelewa ninachokueleza hapa kuhusu utamaduni huo.
Na hili unaloliita "utamaduni wa kiutawala wa falme za kiarabu" ambao unaniambia "hautafanya kazi hapa" ni jaribio lako dhaifu la kuficha Islamophobia yako ambayo wanayo pia watu wanaowapa wakati mgumu watawala Waislam katika Nchi hii kwa makusudi ili kuwakumbusha kuwa mabosi ni nani katika "Mfumo Kristo" na kujaribu kuwaweka katika "nafasi" zao wanazostahiki kwenye Nchi hii.
 
Ila Waislam tuko na Subra na Masheikh zetu wanatuusia Subra na utulivu na hata pale baadhi yetu wanapokuwa na jazba masheikh zetu huwatuliza na kuwakumbusha Mafundisho sahihi ya Dini yao.

Kuna watu wanahisi Waislam ni raia wa daraja la chini hapa Tanzania na wanachukulia hivyo na wanahisi hiyo ni status quo inayopaswa kulindwa. Na hilo linadhihiri hata rais akiwa Muislam; atawekewa mashinikizo, atatikiswa na kusumbuliwa ili kumrudisha katika "nafasi yake" kama Muislam na ajue nani Bosi.

Baadhi yetu tumegundua namna marais Waislam wanavyokuwa intimidated.

Na hili sio sawa.

Hili ni jambo lenye mizizi mirefu ambayo asili yake ni kuwapiga vita Waislam na Uislam.
Ni wazi kabisa kwa haya maandishi hapa kwamba wewe ni mtu wa mlengo gani hata katika huo uislam.

Kundi lenu hili, hata mkipewa nchi yenu wenyewe, bado itakuwa ni migogoro tu baina yenu.
 
Hayo kaa nayo mwenyewe hakuna atakayekusumbua katika Tanzania ya watu wote wanaoamini hayo yako na wasioyaamini.
Weka Tanzania mbele siyo hayo yako mwenyewe..

Ninamuomba Allah Ailinde Nchi yangu ya Tanzania na Aihifadhi Amani yake. ALLAHUMMA AAMIIN. Ninamuomba Allah Amuongoze na Amuhifadhi na kumlinda Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan na Aliyengeneze jambo lake kwa Kheri na Salama na Amruzuku na Amuwafikishe kufanya maamuzi sahihi na Amsamehe madhambi yake. Allah Awaongoze watawala wote wa Tanzania, Allahumma Aamiin.


Ninamuomba Allah Azirudishe kila njama ovu zinazopangwa dhidi ya Amani ya Nchi yetu katika shingo za wenye kuzipanga njama hizo na Aibakishe Amani yetu kwa Salama, Allahumma Aamiin.
 
Pili, ni kweli au uongo kuwa BAKWATA licha ya mapungufu yao yote, hawasumbuani na mtawala yoyote anayetawala Nchi hii? Nitajie hata mtawala mmoja ambaye BAKWATA waliminyana naye.
sasa unataka nikwambie vipi ndipo uelewe kuhusu BAKWATA.
Hiyo mbinu ya "kusumbuana/kutosumbuana" kawaeleze wajinga wenzio.

Kama mtawala anafanya maovu; na unayaona ni mambo ya hovyo unayakalia kimya, maana yake ni nini?

Ina maana gani kuwepo na "AMANI" mahali ambapo hakuna "HAKI", uliona wapi hilo linawezekana.

Ndio maana nakwambia mnataka tukubali tamaduni za kifalme wa kiarabu hapa; jambo ambalo mnalazimisha likubaliwe.
 
Ninamuomba Allah Ailinde Nchi yangu ya Tanzania na Aihifadhi Amani yake. ALLAHUMMA AAMIIN. Ninamuomba Allah Amuongoze na Amuhifadhi na kumlinda Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan na Aliyengeneze jambo lake kwa Kheri na Salama na Amruzuku na Amuwafikishe kufanya maamuzi sahihi na Amsamehe madhambi yake. Allah Awaongoze watawala wote wa Tanzania, Allahumma Aamiin.


Ninamuomba Allah Azirudishe kila njama ovu zinazopangwa dhidi ya Amani ya Nchi yetu katika shingo za wenye kuzipanga njama hizo na Aibakishe Amani yetu kwa Salama, Allahumma Aamiin.
Kama kuna huyo 'mungu' anayemlinda mtu mwovu kama Samia; huyo atakuwa ni shetani moja kwa moja.

Mungu anaipenda Tanzania na watu wake wote bila kujali hizo imani zinazowalewesha na kuwaondoa akili zote kichwani.
 
sasa unataka nikwambie vipi ndipo uelewe kuhusu BAKWATA.
Hiyo mbinu ya "kusumbuana/kutosumbuana" kawaeleze wajinga wenzio.

BAKWATA hawasumbuani na mtawala, hakuna cha kutoelewa wala nini. Kisichoeleweka hapo ni nini? Hujui kwamba BAKWATA hawasumbuani na mtawala yoyote. BAKWATA washawahi kuminyana na Mzee Nyerere, Mzee Mwinyi (Allah Amsamehe na Amrehemu), Mzee Mkapa, Mzee Kikwete, Mzee Magufuli na sasa hivi Mama Samia (Allah Amuongoze na Amlinde na Alitengeneze jambo lake kwa Salama), hawajasumbuana wala kuminyana na yoyote kati ya hao.

Sio TEC wanaowasumbua watawala Waislam halafu wanakuwa laini kwa wenzao, tena Mwalimu Nyerere ndio hawakuwahi kumtolea tamko lolote dhidi yake. Usidhani kuna ambao hatuelewi hiyo pattern, tunaelewa na tunaelewa kwanini.
Kama mtawala anafanya maovu; na unayaona ni mambo ya hovyo unayakalia kimya, maana yake ni nini?

Sisi Waislam tumefundishwa namna ya kumnasihi mtawala. Hatumnasihi mtawala hadharani, ukitaka kumnasihi mtawala basi uwe umnasihi uso kwa uso (umuambie mbele yake) kwa siri au umuandikie kwa siri. Bali Jihadi bora ni kumuambia maneno ya Haki mtawala dhalimu jeuri mbele yake uso kwa uso (kwa siri sio mbele za watu), yaani mtawala dhalimu ukikutana nae uso kwa uso ukamuambia kwa siri (sio mbele za watu) maneno ya Haki na ukamnasihi, hiyo ni katika Jihaad Bora kabisa.

Sio katika majukwaa au kuwa keyboard warrior kama hapa.

Dini yetu inapinga Dhuluma iwe inafanywa na mtawala au raia. Ila kumewekwa utaratibu wa kumnasihi mtawala. Hili limefanywa ili kufunga milango ya machafuko na vurugu.
Ina maana gani kuwepo na "AMANI" mahali ambapo hakuna "HAKI", uliona wapi hilo linawezekana.

Amani haivunjwi kwa kisingizio cha kukosekana Haki. Amani inalindwa na kuhifadhiwa.

Kila mtu akisema kuwa hajali Amani kwa sababu anaona Haki imevunjwa, ima iwe ni Haki kweli au sio Haki ila anaona ni Haki kwa maoni yake na matamanio yake ni sawa.

Mtu anaweza kuwa wala hajali kuhusu Haki kihakika kabisa ila hampendi tu mtawala (kama wanavyomfanyia baadhi ya watu Mama Samia) ila anaficha chuki nyuma ya kudai Haki. Au wala anachokidai sio Haki wala ila kwake yeye anaona ni Haki na akataka kuivunja Amani kwa jina la Haki.


Hivi kila mtu akiamua kudai anayoiona ni Haki kwake kwa kuivunja Amani, kutabaki kitu hapa?

Kuna watu wana nia ovu kabisa lakini wanajificha nyuma ya Haki.

Hata makundi ya kigaidi yanayojinasibisha na Uislam kama Al Qaeda, Ash-Shabaab, Da'esh, Boko Haram, na kadhalika ambao wana fikra za kikhawaarij nao wanaua watu na kuivunja Amani kwa kudai Haki.

Makhawaarij tokea zamani walikuwa wanawakufurisha Waislam na kuzihalalisha damu zamu na kujuzisha kuzimwaga Damu za Waislam, wao slogan yao pia ni Haki.

Khalifa Muongofu aliyeongozwa 'Ali Ibn Abi Twaalib (Allah Amridhie), Swahaba wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) alipokumbana na makhawaarij na wakampiga vita walikuwa wakisema kwa Maneno ya Allah ambayo hawakuyaelewa, wakimuambia 'Ali kuwa; إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۖ "Hukumu haiko ila kwa Mwenyezi Mungu" (Qur-aan 12 : 67) na wakiyafanya Maneno hayo Matukufu ya Allah kama kaulimbiu, Khalifa Muongofu aliyeongozwa 'Ali pale makhawaarij mbwa wa motoni walipokuwa wakimuambia Maneno hayo ya Allah alikuwa akiwajibu; "Maneno ya Haki yanayokusudiwa baatwil", yaani Maneno wanayoyasema ni ya kweli kabisa na ya Haki, ila makhawaarij mbwa wa motoni wanakusudia baatwil, wana malengo yao maovu ila wanatumia Maneno ya Allah ambayo hata hawakuyaelewa, na wala hayakuwa Hoja kwao dhidi ya 'Ali bali 'Ali alikuwa sahihi kabisa na wao walikuwa katika Baatwil, ila mpaka wakaja kumuua 'Ali Ibn Abi Twaalib (Allah Amridhie).

Ndio nyinyi mnaosema Haki Haki na wala hamkusudii Haki na wakati mwengine wala mnayoyataka sio Haki ila bado mnajificha nyuma yake.
Ndio maana nakwambia mnataka tukubali tamaduni za kifalme wa kiarabu hapa; jambo ambalo mnalazimisha likubaliwe.

Na Waislam wengi ikiwemo BAKWATA walipotulia wakati wa Magufuli walikuwa wanataka nini?
 
Kama kuna huyo 'mungu' anayemlinda mtu mwovu kama Samia; huyo atakuwa ni shetani moja kwa moja.

Mungu anaipenda Tanzania na watu wake wote bila kujali hizo imani zinazowalewesha na kuwaondoa akili zote kichwani.


Tumefundishwa kuwaombea Kheri na Du'aa nzuri Watawala wetu, na tumekatazwa kuwaombea laana na mabaya. Wakinyooka basi ni Kheri kwetu. Tukiwaombea laana wanaweza kuwa wabaya zaidi na ikawa shari kwetu.

Sisi Waislam Dini yetu ina Muongozo juu ya kila kitu. Hatuhitaji Demokrasia ili tukamilishe mifumo yetu ya kimaisha. Uislam ni Mfumo wetu wa kimaisha. Wewe kama huna Muongozo wa kuishi na kuamiliana na watawala kutoka kwenye dini yako, hilo ni tatizo lako. Sisi tuna Muongozo mpaka kwa namna ya kuamiliana na mtawala, hatujiishii ishii tu tunavyotaka.

Hatufuati matamanio yenu wala hatupaswi kufuata matamanio yenu, bali tumeonywa na kukatazwa kufuata matamanio yenu nyinyi. Tumekatazwa hata kufuata matamanio yetu ya Nafsi.

Kwetu sisi tumeambiwa Allah huwatawalisha watu waovu juu ya waovu wenzao. Yaani tukiwa waovu, watawala wetu watakuwa kama sisi. Sisi hatutawaliwi na Malaika au Majini, tunatawaliwa na watu kama sisi, watu wakiwa wezi, majambazi, wazinzi, walevi, washirikina, watesaji wa wenzao na waonevu wa wenzao na kadhalika, namuomba Allah Afya na Salama, basi Allah Atawaonesha athari ya matendo yao kwa watawala wao, Atawatawalisha watu mfano wao juu yao ili awaonjeshe sehemu ya wanayoyatenda.


Haiwezekani watu tuwe wezi, madhalimu sisi kwa sisi, mtu kuiba iwe ni sifa na akipata sehemu ya kula halafu asipige basi anaonekana mjinga, tunatapeliana, watu wanaua mwizi wa kuku na simu ya laki mbili, dhulma ijae katika jamii, watu waoneane wenyewe kwa wenyewe na kadhalika halafu mtawala akiwa kama wao makelele kibao.


Sasa sisi tumefundishwa, mtawala akiwa dhalimu ni kwa sababu ya udhalimu wa watu, watu wakitaka waondolewe watawala madhalimu basi waache dhulma wao kwanza.


Tumeambiwa kama dhulma ya mtawala ni Adhabu kwetu kutoka kwa Allah, basi hatupaswi kuiondoa kwa panga zetu, bali kwa kumuomba Allah Msamaha, na kurekebisha hali zetu na kujinyenyekeza kwake Allah. Na kama dhulma ya mtawala ni mtihani tu kwetu, basi tuwe na subra mpaka itakapokuja Amri ya Allah.

Hatupigani na mtawala wala kuminyana naye.


Na tunamuombea Kheri mtawala wetu.

Hayo matusi yako yanakudhuru mwenyewe, kwa sababu ya ujinga na jeuri yako au matamanio yako.

Allah Akuongoze.

Mimi naishia hapa kwako.


Ninamuomba Allah Afya na Salama katika Dini na Dunia yangu, ninamuomba Allah Ailinde Nchi yetu ya Tanzania na watu wake, Aiepushe na vitimbi vya kila mwenye kutaka kuiharibu Amani ya Nchi hii, ninamuomba Allah Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu Amuongoze Rais wetu Mama samia Suluhu Hassan na Amuepushe na Mabalaa na Amlinde na Amjaalie Afya na Salama na Ampe wepesi na Tawfiq ya kufanya maamuzi sahihi, Allah Alitengeneze jambo lake kwa Kheri na Salama yeye na wasaidizi wake wote, Allahumma Aamiin.
 
Tumefundishwa kuwaombea Kheri na Du'aa
nilishakutana na "WALEVI" wa dini wengi hapa zaidi yako.
Usihangaike kujaza takataka humu ambazo sina muda wa kuzisoma.

Nisilotaka kufanya, ni kwa mlevi kama wewe kuwa ndiye kielelezo cha dini hiyo; kwa sababu najuwa hiyo dini siyo ya kilevi kama inavyokufanya wewe.
Hata huji matatizo mengi mnayosababisha kila sehemu watu walevi kama nyinyi. Nchi yeyote inapoingiliwa na watu wa aina yako, nchi hiyo haipati amani tena.

Huyo allah unayemhusisha na jambazi kama Samia, kamwe hawezi kuwa 'Allah', huyo wa kwako na Samia ni shetani.

Hakuna 'Allah' anayyeweza mwizi wa uchaguzi na kuamua kutawala watu kwa mabavu hata kuwaua hao watu wasiotaka upumbavu huo.

Huyu 'allah' wenu, wewe na Samia hayupo Tanzania.
 
nilishakutana na "WALEVI" wa dini wengi hapa zaidi yako.
Usihangaike kujaza takataka humu ambazo sina muda wa kuzisoma.

Nisilotaka kufanya, ni kwa mlevi kama wewe kuwa ndiye kielelezo cha dini hiyo; kwa sababu najuwa hiyo dini siyo ya kilevi kama inavyokufanya wewe.
Hata huji matatizo mengi mnayosababisha kila sehemu watu walevi kama nyinyi. Nchi yeyote inapoingiliwa na watu wa aina yako, nchi hiyo haipati amani tena.


Mimi mlevi ila wewe unayempiga vita Mama Samia na kupuuzia Amani kwa kisingizio cha Haki na huku hukusudii Haki ndio uko sober?! Yaani sisi tusababishe kukosekana kwa Amani halafu nyinyi ndio watu wa Amani? Sisi tunaopinga maandamano ya aina zote, tunaopinga kushika silaha dhidi ya mtawala, tunaopinga mapinduzi, kupinga machafuko na kupinga umwagikaji damu na vurugu ndio walevi halafu wewe ndio mzima? Sisi ndio wavunja Amani na nyinyi ndio watengenezaji?

Hivi unadhani sisi tunapowapiga vita watu kama Al Qaeda au Boko Haram na mfano wao unafikiri tunacheza sio? Au unahisi huwa tunajipendekeza kwenu?

Sisi tunasimama na Dini yetu. Tunaposema tunataka Amani ujue tunamaanisha.


Na tutasimama na msimamo kuwa mnampiga vita Mama Samia kwa sababu ya Uislam wake. Hiyo kusema kuwa sijui baadhi yetu sijui tunaharibu kila tunapokwenda, tunajua hiyo ni label mnayotupa sisi wote. Na hiyo phobia ukichanganya na husda pamoja na kulinda status quo mliyojiwekea nyinyi wenyewe ndio mnamsumbua Mama Samia (Allah Amuongoze na Amsaidie).


Na Waislam wanazidi kuamka, Alhamdulillah. Zama za kufanywa chambo cha kuvunja Amani ya Nchi zimepita kwa Idhini ya Allah.

Unafikiri hatujui kuwa mnampiga vita Mama Samia kwa sababu ni Muislam? Kuna watu wanafuata mkumbo katika kumpiga vita ila tunajua hii vita ni kwasababu ya Uislam wake. Na Waislam wanazidi kuamka, Alhamdulillah.
 
Mimi mlevi ila wewe unayempiga vita Mama Sami
Inawezekana Samia ndiye mungu wako.
Mtu kama wewe si ajabu hilo ndilo linalokusumbua hapa.

Sasa fahamu kuwa huyo mungu wako Samia hana nafasi Tanzania; hatma yake kishajitengenezea mwenyewe.
 
Inawezekana Samia ndiye mungu wako.
Mtu kama wewe si ajabu hilo ndilo linalokusumbua hapa.

Ametakasika Allah kutukuka Kukubwa kabisa. Mola wangu Mlezi na Mola Mlezi wa Mama Samia na Mola Mlezi wa kila kitu ni Allah Peke Yake. Hapana Mola Apasae kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Allah, PEKE YAKE HANA MSHIRIKA YOYOTE YULE. Huyo ndio Muabudiwa wa Haki, na waabudiwa wengine wote kinyume na Allah basi ni baatwil, hawastahiki kuabudiwa na sio waabudiwa wa Haqq. Anayestahiki kuabudiwa ni ALLAAH PEKE YAKE, HANA MSHIRIKA.

HAPANA MOLA APASAE KUABUDIWA KWA HAQQ ISIPOKUWA ALLAAH NA MUHAMMAD NI MTUME WA ALLAAH.


Ninamuabudu Allah Peke yake Bila ya kumshirikisha na chochote kile. Na Allah ndio kaniletea Dini na Akaniamrisha kupitia Mtume wake (Swala na Salamu ziwe juu yake) nimtii mtawala katika yasiyo maasi.
 
Kwenye siasa kuwa na msimamo unaoleweka na wa wazi ni jambo muhimu sana la kujenga heshima na kuaminika.

Ukiangalia katika siasa za Tanzania BAKWATA wao wamejifungamanisha wazi kabisa na CCM na serikali yake, hawajifichi na msimamo wao uko wazi kabisa unaeleweka kwa watawala na wafuasi wao, hawaongei kwa mafumbo na vitendawili.

Kwa upande wa TEC wao hawaeleweki wamesimama upande gani. Wanasema wanatetea haki lakini hapo hapo mguu mmoja wako ndani ya CCM na mwingine uko nje. Wanajifanya kama vile hawana "leverage" yoyote kwenye utawala.

Mfano katika uchaguzi wa 2025 BAKWATA wao walisema wazi wanaunga mkono huo uchaguzi na wakawa wanashiriki shughuli mbalimbali za uchaguzi, TEC wao walibaki nyutro wakiwa hawaeleweki wala kuwa na msimamo kama wanaunga mkono au wanaupinga huo uchaguzi!

Haki ina upande.
Hapana bakwata hawana nguvu kuliko wakatoliki,kwa sababu waislamu wengi hawaitaki bakwata
 
Unafikiri hatujui kuwa mnampiga vita Mama Samia kwa sababu ni Muislam? Kuna watu wanafuata mkumbo katika kumpiga vita ila tunajua hii vita ni kwasababu ya Uislam wake. Na Waislam wanazidi kuamka, Alhamdulillah.
Hapa imenilazimu nikusome hadi huku chini.
Nimejiridhisha pasipo na shaka yoyote kwamba wewe umeathirika; na ni huo "ulevi mkubwa wa dini" ambayo umechanganya na bangi. humo humo.
 
Hapa imenilazimu nikusome hadi huku chini.
Nimejiridhisha pasipo na shaka yoyote kwamba wewe umeathirika; na ni huo "ulevi mkubwa wa dini" ambayo umechanganya na bangi. humo humo.

Ad hominem
 
Ametakasika Allah kutukuka Kukubwa kabisa. Mola wangu Mlezi na Mola Mlezi wa Mama Samia na Mola Mlezi wa kila kitu ni Allah Peke Yake. Hapana Mola Apasae kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Allah, PEKE YAKE HANA MSHIRIKA YOYOTE YULE. Huyo ndio Muabudiwa wa Haki, na waabudiwa wengine wote kinyume na Allah basi ni baatwil, hawastahiki kuabudiwa na sio waabudiwa kwa Haqq. Anayestahiki kuabudiwa ni ALLAAH PEKE YAKE, HANA MSHIRIKA.

HAPANA MOLA APASAE KUABUDIWA KWA HAQQ ISIPOKUWA ALLAAH NA MUHAMMAD NI MTUME WA ALLAAH.


Ninamuabudu Allah Peke yake Bila ya kumshirikisha na chochote kile. Na Allah ndio kaniletea Dini na Akaniamrisha kupitia Mtume wake (Swala na Salamu ziwe juu yake) nimtii mtawala katika yasiyo maasi.
Kaa na ulevi wako mwenyewe huko huko na huyo mwovu na mhalifu Samia Suluhu Hassan.
 
Back
Top Bottom