ALAAA! wewe na huyo mwenzio kumbe mpo humu mkifanya kazi hii?BAKWATA hawasumbuani na mtawala yoyote, licha ya mapungufu waliyonayo BAKWATA. Na TEC hawakumpinga Magufuli kama walivyompinga Mzee Mwinyi (Allah Amrehemu), Mzee Kikwete na sasa hivi wanavyompinga Mama Samia.
Kuna Screenshot moja ilikuwa inasambaa inaonesha post ambayo mtu kaweka idadi ya matamko TEC wameyatoa kwa kila Rais, siko nayo ila hadi humu Jf niliwahi kuiona. Ninachokikumbuka kutoka mule ni kuwa TEC hawajawahi kutoa tamko lolote wakati wa utawala wa Nyerere, katika miaka yote ambayo Mzee Nyerere katawala, hakuna tamko hata moja dhidi yake. Na ukiangalia kwa marais Waislam wametoa matamko mengi kuliko kwa marais wasio Waislam.
Kusema TEC walimpinga sana Magufuli kwa kumlinganisha na nani?
Ukweli ni kwamba TEC wanapenda kuwasakama Marais Waislam.
BAKWATA siku zote hawasumbuani na watawala.
Ungekuwa na akili huru tayari ungejuwa kwamba wewe ni mmoja wao; unatazama maswala ya nchi katika mawani hayo hayo ya udini; na kundi hili limekuwepo miaka yote okea enzi za uhuru. Bila shaka wewe ni mhitimu wa chuo cha Kariakoo kinachofundisha haya mambo, au siyo?
Hujui kwa nini BAKWATA iliundwa na kuwa sehemu ya CCM, tokea wakati huo?
Na bado hujui kwamba ni hao hao BAKWATA sasa hivi wametekwa na kundi lilelile la tokea enzi za kudai uhuru?
Sasa unataka kujifanya hujui njia za ulaghai zinazotumiwa huko BAKWATA; njia zile zile anazotumia Samia; na unasubiri BAKWATA watoe matamko ndipo ujue kazi zao wanazifanya kimya kimya huku matokeo yakionekana na wala hujui kuyatafsiri kwa vile tu wewe ni mmoja wao!
Hizi akili za kijinga mnazileta kuvuruga taifa hili halafu mnajifanya hamjui chochote.
Wewe nilikutambua toka mwanzo, pamoja na kwamba hujitoi waziwazi kuwa mtetezi wa uovu huu unaofanyika sasa chini ya Samia.
Hayo kaa nayo mwenyewe hakuna atakayekusumbua katika Tanzania ya watu wote wanaoamini hayo yako na wasioyaamini.Mimi ni Muislam wala sijifichi. Na ninasimama na Dini yangu. Actually kwa mujibu wa Dini yangu haifai kuutoa mkono wangu wa utiifu kwa mtawala Muislam na hata kwa mtawala aside Muislam, tumekatazwa kumtoa kama kumtoa kutapelekea madhara makubwa zaidi. Hivyo tumeamrishwa kumtii mtawala katika yasiyo haramu.
ALAAA! wewe na huyo mwenzio kumbe mpo humu mkifanya kazi hii?
Nyinyi ni 'foot soldier'', au ndio wale "mbwa mwitu wa Mwaipopo mmesambazwa hadi huku?
"BAKWATA hawasumbuani na mtawala yeyote", sasa ndiyo maneno mnayoyatanguliza mbele kwa kutumia ulaghai ule ule unaotumiwa na Samia na Genge lake lote zima?
Huu utamaduni wa kiutawala wa falma za kiarabu hautafanya kazi hapa. Na huo ndio ujinga wanaoutumia BAKWATA; lakini sina hakika kama unayo akili ya kutosha kuelewa ninachokueleza hapa kuhusu utamaduni huo.
Na hili unaloliita "utamaduni wa kiutawala wa falme za kiarabu" ambao unaniambia "hautafanya kazi hapa" ni jaribio lako dhaifu la kuficha Islamophobia yako ambayo wanayo pia watu wanaowapa wakati mgumu watawala Waislam katika Nchi hii kwa makusudi ili kuwakumbusha kuwa mabosi ni nani katika "Mfumo Kristo" na kujaribu kuwaweka katika "nafasi" zao wanazostahiki kwenye Nchi hii.Huu utamaduni wa kiutawala wa falma za kiarabu hautafanya kazi hapa. Na huo ndio ujinga wanaoutumia BAKWATA; lakini sina hakika kama unayo akili ya kutosha kuelewa ninachokueleza hapa kuhusu utamaduni huo.
Ni wazi kabisa kwa haya maandishi hapa kwamba wewe ni mtu wa mlengo gani hata katika huo uislam.Ila Waislam tuko na Subra na Masheikh zetu wanatuusia Subra na utulivu na hata pale baadhi yetu wanapokuwa na jazba masheikh zetu huwatuliza na kuwakumbusha Mafundisho sahihi ya Dini yao.
Kuna watu wanahisi Waislam ni raia wa daraja la chini hapa Tanzania na wanachukulia hivyo na wanahisi hiyo ni status quo inayopaswa kulindwa. Na hilo linadhihiri hata rais akiwa Muislam; atawekewa mashinikizo, atatikiswa na kusumbuliwa ili kumrudisha katika "nafasi yake" kama Muislam na ajue nani Bosi.
Baadhi yetu tumegundua namna marais Waislam wanavyokuwa intimidated.
Na hili sio sawa.
Hili ni jambo lenye mizizi mirefu ambayo asili yake ni kuwapiga vita Waislam na Uislam.
Hayo kaa nayo mwenyewe hakuna atakayekusumbua katika Tanzania ya watu wote wanaoamini hayo yako na wasioyaamini.
Weka Tanzania mbele siyo hayo yako mwenyewe..
sasa unataka nikwambie vipi ndipo uelewe kuhusu BAKWATA.Pili, ni kweli au uongo kuwa BAKWATA licha ya mapungufu yao yote, hawasumbuani na mtawala yoyote anayetawala Nchi hii? Nitajie hata mtawala mmoja ambaye BAKWATA waliminyana naye.
Kama kuna huyo 'mungu' anayemlinda mtu mwovu kama Samia; huyo atakuwa ni shetani moja kwa moja.Ninamuomba Allah Ailinde Nchi yangu ya Tanzania na Aihifadhi Amani yake. ALLAHUMMA AAMIIN. Ninamuomba Allah Amuongoze na Amuhifadhi na kumlinda Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan na Aliyengeneze jambo lake kwa Kheri na Salama na Amruzuku na Amuwafikishe kufanya maamuzi sahihi na Amsamehe madhambi yake. Allah Awaongoze watawala wote wa Tanzania, Allahumma Aamiin.
Ninamuomba Allah Azirudishe kila njama ovu zinazopangwa dhidi ya Amani ya Nchi yetu katika shingo za wenye kuzipanga njama hizo na Aibakishe Amani yetu kwa Salama, Allahumma Aamiin.
Bakwata ni umoja wa waislamu CCMSasa bakwata si taasisi ya ccm!...bakwata,uvccm,uwt nikitu kimoja
sasa unataka nikwambie vipi ndipo uelewe kuhusu BAKWATA.
Hiyo mbinu ya "kusumbuana/kutosumbuana" kawaeleze wajinga wenzio.
Kama mtawala anafanya maovu; na unayaona ni mambo ya hovyo unayakalia kimya, maana yake ni nini?
Ina maana gani kuwepo na "AMANI" mahali ambapo hakuna "HAKI", uliona wapi hilo linawezekana.
Ndio maana nakwambia mnataka tukubali tamaduni za kifalme wa kiarabu hapa; jambo ambalo mnalazimisha likubaliwe.
Kama kuna huyo 'mungu' anayemlinda mtu mwovu kama Samia; huyo atakuwa ni shetani moja kwa moja.
Mungu anaipenda Tanzania na watu wake wote bila kujali hizo imani zinazowalewesha na kuwaondoa akili zote kichwani.
nilishakutana na "WALEVI" wa dini wengi hapa zaidi yako.Tumefundishwa kuwaombea Kheri na Du'aa
nilishakutana na "WALEVI" wa dini wengi hapa zaidi yako.
Usihangaike kujaza takataka humu ambazo sina muda wa kuzisoma.
Nisilotaka kufanya, ni kwa mlevi kama wewe kuwa ndiye kielelezo cha dini hiyo; kwa sababu najuwa hiyo dini siyo ya kilevi kama inavyokufanya wewe.
Hata huji matatizo mengi mnayosababisha kila sehemu watu walevi kama nyinyi. Nchi yeyote inapoingiliwa na watu wa aina yako, nchi hiyo haipati amani tena.
Inawezekana Samia ndiye mungu wako.Mimi mlevi ila wewe unayempiga vita Mama Sami
Inawezekana Samia ndiye mungu wako.
Mtu kama wewe si ajabu hilo ndilo linalokusumbua hapa.
Hapana bakwata hawana nguvu kuliko wakatoliki,kwa sababu waislamu wengi hawaitaki bakwataKwenye siasa kuwa na msimamo unaoleweka na wa wazi ni jambo muhimu sana la kujenga heshima na kuaminika.
Ukiangalia katika siasa za Tanzania BAKWATA wao wamejifungamanisha wazi kabisa na CCM na serikali yake, hawajifichi na msimamo wao uko wazi kabisa unaeleweka kwa watawala na wafuasi wao, hawaongei kwa mafumbo na vitendawili.
Kwa upande wa TEC wao hawaeleweki wamesimama upande gani. Wanasema wanatetea haki lakini hapo hapo mguu mmoja wako ndani ya CCM na mwingine uko nje. Wanajifanya kama vile hawana "leverage" yoyote kwenye utawala.
Mfano katika uchaguzi wa 2025 BAKWATA wao walisema wazi wanaunga mkono huo uchaguzi na wakawa wanashiriki shughuli mbalimbali za uchaguzi, TEC wao walibaki nyutro wakiwa hawaeleweki wala kuwa na msimamo kama wanaunga mkono au wanaupinga huo uchaguzi!
Haki ina upande.
Hapa imenilazimu nikusome hadi huku chini.Unafikiri hatujui kuwa mnampiga vita Mama Samia kwa sababu ni Muislam? Kuna watu wanafuata mkumbo katika kumpiga vita ila tunajua hii vita ni kwasababu ya Uislam wake. Na Waislam wanazidi kuamka, Alhamdulillah.
Hapa imenilazimu nikusome hadi huku chini.
Nimejiridhisha pasipo na shaka yoyote kwamba wewe umeathirika; na ni huo "ulevi mkubwa wa dini" ambayo umechanganya na bangi. humo humo.
Kaa na ulevi wako mwenyewe huko huko na huyo mwovu na mhalifu Samia Suluhu Hassan.Ametakasika Allah kutukuka Kukubwa kabisa. Mola wangu Mlezi na Mola Mlezi wa Mama Samia na Mola Mlezi wa kila kitu ni Allah Peke Yake. Hapana Mola Apasae kuabudiwa kwa Haki isipokuwa Allah, PEKE YAKE HANA MSHIRIKA YOYOTE YULE. Huyo ndio Muabudiwa wa Haki, na waabudiwa wengine wote kinyume na Allah basi ni baatwil, hawastahiki kuabudiwa na sio waabudiwa kwa Haqq. Anayestahiki kuabudiwa ni ALLAAH PEKE YAKE, HANA MSHIRIKA.
HAPANA MOLA APASAE KUABUDIWA KWA HAQQ ISIPOKUWA ALLAAH NA MUHAMMAD NI MTUME WA ALLAAH.
Ninamuabudu Allah Peke yake Bila ya kumshirikisha na chochote kile. Na Allah ndio kaniletea Dini na Akaniamrisha kupitia Mtume wake (Swala na Salamu ziwe juu yake) nimtii mtawala katika yasiyo maasi.