Unajaribu kumponda Samia kupitia uwepo wa Kikwete na Familia yake ndani ya CCM lakini inabidi uwe na ujasiri mkubwa sana kutoyaona mengi sana ya muhimu anayoyafanya Samia na awamu yake.
Hakuna mradi aliyouanzisha JPM halafu Samia auche nusu nusu.
SGR inaelekea kumalizika kimebakia kipande cha kuelekea Mwanza na chenyewe kitakwisha hivi karibuni.
Viwanja vya ndege karibu vyote vinaelekea kumalizika muda huu. Wawekezaji wengi wanakuja awamu ya sita.
Kigoma iliyokuwa imesahaulika muda huu inao umeme na imefikiwa na miradi ya treni.
Mwenye haki ya kuiponda awamu ya sita ni Tundu Lissu, Heche watu ambao hawapo ndani ya CCM hawa wa ndani ya chama ni wachafu sawa na wanaowanyooshea vidole.
Kina January Makamba, Luhaga Mpina na wote wa aina yao baada ya kupigwa chini ubunge wanakuja na mashambulizi kupitia majina bandia humu JF.