GE2025 Balozi Polepole: Rais Samia anahujumiwa, kazungukwa na Wana Mtandao (Kikwete na Rostam)

GE2025 Balozi Polepole: Rais Samia anahujumiwa, kazungukwa na Wana Mtandao (Kikwete na Rostam)

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Samia aahirishe kugombea urais,asigombee ili taifa libaki salama.


Mpaka anasema hadharani kwamba boss wake ni kikwete inaonekana Samia hana upeo wa kuona mambo na ku-reason sawa sawa,yupo yupo tu hajui thamani ya kiti alichokikalia.
Anaogopa na huenda anajua walichomfanya Magufuli au ni miongoni mwao.
 
Samia anahujumiwa kwanini asichukue hatua wakati yeye ni Rais?

Ukiona unahujumiwa na ukashindwa kuchukua hatua achia ngazi otherwise your a part of a problems!

Hoja ya kijinga Sana hii.
Unachosema wewe ndicho alichosema yeye....naona wote kumbe mna hoja za kijinga🤣🤣
 
Hawa wanaaminika maana kubwa mbowe ndo alifanya kila kitu kama boss shida ilikuwa kwa lissu ilibidi akubali shingo upande ili isionekane kama analeta mgawanyiko chamani ukiiona humukubali Lissu basi wewe ni kobazi mdini jichunguze
Lissu alimpromote Lowassa kumbuka Hilo Kwanza
 
What if kama naye ni mwana
Wamemshughulikia mwanae

Hajashughulikiwa, Ni kete zinasukumwa, jamaa huwa wana long term plan na no watu wa makubaliano na maridhiano sana ndani ya vikao vyao ili waendelee kuimiliki kampuni yao.

Kijana atakuwa ana majukumu mengine muhimu ndani ya gang lao na nje ya kampuni.
Hao ni nchi ndani ya nchi.

ndani ya mitaa ya Kabul-Afghanistan.
 
Wewe kwanini haukusema??
Wapenzi wa Chadema huwa wananifurahisha sana anahoji kuhusu polepole kwanini hakusema kipindi kile now kwanini anasema na anasema hamuamini lakini hao hao wanawaamini wakina Lissu, Lema na mnyika waliomsema Lowassa ni fisadi kwa miaka 8 alafu wakampokea kwenye chama Chao na kuwa ni mgombea wa uraisi na wakamsafisha huu ni unafiki wa aina gani
 
Watanzania wanatakiwa kupaza sauti Tanzania ni mali yetu sote siyo mali ya kikundi cha wachache wanaotaka kujinufaisha. Polepole amekuwa jasiri sana sijui watamfanyaje wakimkamata.
Huyu jamaa alijipanga mapema yawezekana ana watu ndani ya mfumo ambao hawafurahishwi na yanayoendelea wako nyuma yake kuhakikisha hakuna nzi anamgusa!
 
Bila Mbowe kutanguliza njaa mbele Lowassa asingekanyaga CHADEMA
Kama Lissu, Lema na mnyika hawakupendezwa na maamuzi ya mbowe wangetoka hadharani Kama alivyofanya Dr. Slaa na kupinga iko kitendo au wangejiuzulu lakini kitendo Chao cha kukaa kimya imeonesha wamebariki hayo maamuzi na hawakuishia hapo Hadi wakawa wanampigia kampeni my main point ni hivi kwanini wanachadema wanahoji kwanini polepole hakuongea kipindi cha Magu lakini kwanini anafanya Sasa na Mimi nikatengeneza hoja yangu kuhusu hili suala la Lowassa kwa viongozi wao Kama ambavyo wanaamini viongozi pamoja na kumleta Lowassa ndani ya chama Chao kwanini Sasa wanahoji kuhusu Polepole anayasema haya kwanini hakusema kipindi kile huwa uwalali wakusema hivyo wanapata wapi
 
Jakaya Mrisho Kikwete ni kivuruge, ameivuruga CCM na anamalizia kuivuruga nchi, hivi mtu kama huyu kuna sababu aendelee kuwa hai?
 
Support anayopewa mtandaoni inatia moyo. Sote tunajua nini kitafata ukionekana kwenye media live unafanya ambacho CCM hawakipendi.
Ukimuuliza dc wa kisarawe atakuambia Polepole ni nani?

Nilichogundua wengi tunamchukulia Polepole ni mtu wa kawaida na ccm juzi juzi tu ana miaka mitano, sio kweli
 
Mkuu uwezi kuchukuwa hatua kiraisi yaani wao ndio wanakuongoza na Bado wanakupigania uendelee kuwepo na ndio maana polepole amesema yeye mwenyewe hajui kinachoendelea na ndio serikali ya pili ambayo inayoendeaha nchi ambayo haitambuliki na ambao ndio Ina nguvu huyu polepole ukimsikiliza kimakini Kuna mambo mengi anayajua yapo nyuma ya pazia na ndio maana hao hao ccm wanampinga vikali na ndani ya ccm Kuna matabaka yameshagawanyika Yale yanayosema ukweli yameshamalizwa
Ni kweli lkn Samia lazima abebe hii lawama

Watu wanakupangia na wewe unakubali ?

And your the president? Commander in Chief? Seriously?

Ndio maana nimesema Samia is the part of problem yeye ni tatizo zaidi kuliko Hayo magenge!!

She must go !!
 
Aliyemleta Lowassa ni Mbowe ambaye amekuja kubainika kumbe hakuwa mpinzani halisi. Ndiyo maana kwa sasa chama kinasafisha wale wote waliokuwa wanafiki baada ya Mh Lissu kushika uenyekiti.
Lissu, Lema na mnyika walikuwa sehemu ya hayo maamuzi na ndio maana hukuwasikia kupinga hayo maamuzi au kujiuzulu Kama alivyofanya Dr. Slaa na hawakuishia hapo tu walimpigia na kampeni kabisa Kama ambavyo unawaamini viongozi wako pamoja na Hilo kosa waliofanya basi Huna uwalali wowote wako wakuhoji kwanini polepole hakuongea kipindi cha Magu kwanini anaongea sasa tofauti na hapo utakuwa unafanya ushabiki na chuki zako binafsi kwa polepole
 
Katika round ya 3 Leo Mh. Polepole ameendelea kuuleza umma wa watanzania wa kinachoendelea ndani ya CCM na namna kundi la wanamtandao waliomzunguka Rais Samia wanavopanga mipango Yao.

Ameeleza mambo mengi ambayo sisi kama Wananchi wa kawaida hatuyajui ukiwa ni pamoja na hujuma alizokuwa anafanyiwa marehemu Rais Magufuli , namna ambavyo wanamtandao na familia zao wanavyojaribu kujimilikisha nchi na kwa bahati mbaya sana anasema hajui kama Rais Samia anajua kinachoendelea au hajui.

Mzee Wasira aliombwa na Mzee wa Heshima nchini hapa kukutana na Rais ili aielezwe kinachoendelea bahati mbaya Mzee wasira alikataa anasema polepole.

Anaendelea kusema kuwa viongozi wamjibu hoja zake wao wenyewe wasiwatume Malay men kujibu.

Ataendelea kuongea na watanzania wiki ijayo na ameahidi kuyasema yote ambayo yapo gizani kuhusu kundi linalotaka kuiteka nchi hii.

Mungu anaipenda Tanzania kuwa na watu aina ya Balozi Polepole. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki afrika

Asanteni.

Huyu jamaa siri anazozitoa sidhani kama atabaki salama
 
Back
Top Bottom