Katika round ya 3 Leo Mh. Polepole ameendelea kuuleza umma wa watanzania wa kinachoendelea ndani ya CCM na namna kundi la wanamtandao waliomzunguka Rais Samia wanavopanga mipango Yao.
Ameeleza mambo mengi ambayo sisi kama Wananchi wa kawaida hatuyajui ukiwa ni pamoja na hujuma alizokuwa anafanyiwa marehemu Rais Magufuli , namna ambavyo wanamtandao na familia zao wanavyojaribu kujimilikisha nchi na kwa bahati mbaya sana anasema hajui kama Rais Samia anajua kinachoendelea au hajui.
Mzee Wasira aliombwa na Mzee wa Heshima nchini hapa kukutana na Rais ili aielezwe kinachoendelea bahati mbaya Mzee wasira alikataa anasema polepole.
Anaendelea kusema kuwa viongozi wamjibu hoja zake wao wenyewe wasiwatume Malay men kujibu.
Ataendelea kuongea na watanzania wiki ijayo na ameahidi kuyasema yote ambayo yapo gizani kuhusu kundi linalotaka kuiteka nchi hii.
Mungu anaipenda Tanzania kuwa na watu aina ya Balozi Polepole. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki afrika
Asanteni.