TANZIA Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine J Mushi, afariki dunia kwa ajali ya Gari

TANZIA Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine J Mushi, afariki dunia kwa ajali ya Gari

Let us assume alikua anakimbia mwendo mkubwa.

Akalose control baada ya kupigwa full light na gari aliyopishana nayo.

Akatoka nje ya barabara.

Gari ikapiga mahali ikawaka....

The rest is history.

Hii ni assumption tu.
Crown inamwendo gani mkali [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Familia poleni! Mh Balozi alipaswa kuwa na dereva!!.

Nani amlipe huyo dereva wa balozi, kodi zetu ?????

Hivi unadhani balozi wa USA akiwa kwao Marekani anapewa dereva ?

Vi nchi vya masikini wachafu ndio tunataka viongozi waishi kama wafalme.

Acha watumie barabara hizo hizo , acha wafe kwenye mazingira hayo hayo tunayofia sisi.
 
View attachment 2447629
Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Joseph Mushy, amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Mkata, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Tuache ubinafsi. Boss mkubwa kiasi hicho unasafiri usiku mwenyewe? Unakosa personal driver? Mwakilishi wa nchi una mambo mengi, unajipa na jukumu la kuendesha? Alipaswa kuwa na dereva na ili kuwa busy na safari, angekuwa na mtu wa kupiga naye story. Huyu atakuwa alisinzia akahama barabarani huku mguu ukiwa kwa moto.
 
Kwa ngazi za kiutendaji, Balozi wa Tanzania anaporudi nyumbani (Tanzania) anahesabika kama Mkurugenzi wa Idara.
Hivyo ni vyema kuzingatia hilo mtu anapotoa hoja ya kushangaa Balozi kujiendesha mwenyewe. Je ni Wakurugenzi wote wanatumia madereva wanaposafiri?
 
Nani amlipe huyo dereva wa balozi, kodi zetu ?????

Hivi unadhani balozi wa USA akiwa kwao Marekani anapewa dereva ?

Vi nchi vya masikini wachafu ndio tunataka viongozi waishi kama wafalme.

Acha watumie barabara hizo hizo , acha wafe kwenye mazingira hayo hayo tunayofia sisi.
End off....🤣🤣😂
Lakini misukule itasema wao ni "the chosen one"....
Ndio maana manabii wa DINI za mataputapu wametalamaki.....
 
Thread nyingine inayosema 'kifo chabalozi kichunguzwe' kuna mdau (id yake Ranger9 nadhani) anamuelezea balozi kama mtu very humble, simple, outgoing na sifa nyingine hapo...
Hapa kuna mdau amegusia huenda balozi ame-fake death,
Nikiunga dots kwa ajili yangu ndogo
....tetesi za kufukuzwa ubalozini Austria kwa tuhuma za ubakaji
....taarifa za kifo baada ya siku 2 tokea siku ya tukio
....majibu ya katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje alipoulizwa juu ya taarifa

Naconclude mwamba tupo nae hapa jamvini![emoji3064][emoji848][emoji2827]
 
Kwa ngazi za kiutendaji, Balozi wa Tanzania anaporudi nyumbani (Tanzania) anahesabika kama Mkurugenzi wa Idara.
Hivyo ni vyema kuzingatia hilo mtu anapotoa hoja ya kushangaa Balozi kujiendesha mwenyewe. Je ni Wakurugenzi wote wanatumia madereva wanaposafiri?
Unakuwa mkurugenzi kwa nini usiwe na dereva? Yaani unashindwa kumlipa mtu 200k akupeleke unapotaka?
 
TAARIFA KWA UMMA

MSIBA WA BALOZI CELESTINE J. MUSHY

Dodoma, 16 Desemba 2022

Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki umesikitishwa na kifo cha Balozi wa Tanzania nchini Austria na Mwakilishi wa Kudumu katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa, Vienna, Mhe. Celestine J. Mushy aliyefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Mkata, Handeni Mkoani Tanga tarehe 13 Desemba, 2022.

Balozi Mushy amefariki dunia baada ya gari aliyokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Kilimanjaro kugongana na lori la mizigo na hatimaye kuungua moto na yeye akiwa ndani yake.

Balozi Mushy atakumbukwa kwa umahiri wake mkubwa katika masuala ya kidiplomasia. Wakati wa uhai wake ameitumikia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nafasi mbalimbali zikiwemo Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kaimu Katibu Binafsi wa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne na Katibu Tawala Msaidizi wa Masuala ya Uchumi, Sektetariet ya Mkoa wa Mtwara.

Wizara kwa kushirikiana na familia ya Marehemu Balozi Mushy inaendelea na mipango ya maandalizi ya mazishi na itakapokamilika wananchi watajulishwa.

Wizara inatoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa wa Marehemu kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu Balozi Celestine Mushy mahali pema peponi, Amina.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
 
Gari yake iligongana uso kwa uso na Lory kutoka kampuni ya Mahit sijui ( sikumbuki jina vizuri ) ilikua inatokea Tanga, ile impact ilifanya gari yake ilipuke hapo hapo, Lory ilidondoka na cabin yote iliungua Moto

Aliyekua kwa gari ndogo ndio aliingia upande wa Lory, kuna uwezekano dereva alisinzia au labda alikua kalewa, kwa ile impact yaan hata kama isingeungua bado asingepona
 
Back
Top Bottom