Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Duh...!. Hivi hizi mambo bado zipo?!Mkuu Paskali, Kwilumba, ngoja niwape nadharia yangu katika mambo kama haya. Nayafahamu sana.
Ni kwamba, huyu jamaa ni balozi pale Austria. Anatuhumiwa na kesi ya kubaka, lakini Austria hawawezi kumfikisha mahakamani kwa sababu ya kinga ya kidiplomasia. Wanaomba Tanzania imtolee kinga ili ashitakiwe, Tanzania wanakataa. Tanzania wanasema arudishwe nyumbani kama ni mashitaka tutamfungulia huku.
Kwa shingo upande Austria wanamwamuru aondoke. Lakini pia Austria wanaripoti malalamiko yao kwa serikali ya EU (European Union) na kusema wanajua huyu jamaa akirudi Tanzania hatafanywa lolote kama ilivyo kwa mataifa haya ya Afrika, vigogo wanalindana.
EU wanaiambia Tanzania, msipomchukulia hatua huyu jamaa tutawachapa na vikwazo hadi mkome. Misaada yote tutasitisha na dunia nzima kujua kwamba tunawaadhibu kwa sababu ya balozi wenu aliyebaka lakini hamtaki kumwajibisha. Tunawapa wiki moja tusikie amewekwa ndani.
Sasa ngoma ni kwa serikali ya Tanzania - kumfungulia mashitaka balozi ni jambo la aibu, hasa kwa kosa la kubaka. Kila balozi wetu ataonwa kama anatoka nchi ya wabakaji. Samia akienda nchi fulani watu watanong;onezana raisi wa nchi ya mabalozi wabakaji huyu! Lakini pia tusipomfungulia mashitaka EU watatuchapa kwa vikwazo na kuutangazia ulimwengu jambo hili, na inakuwa mbaya hata zaidi. Wafanyeje?
Ndipo wanatambua kwamba huyu jamaa akipotezewa kesi inakwisha, hakuna aibu wala vikwazo na kashfa yote itakuwa imezimwa. EU hawatatusumbua tena, na serikali haitahitaji tena kumfungulia mashitaka na kujiabisha.
Basi, ajali inapangwa, gari linachomwa moto ili kufuta mashaka yeyote juu ya kama kweli ilikuwa ni ajali. Kamati ya Ulinzi na usalama inaambiwa iende eneo fulani kuna ajali itatokea. Mkuu wa wilaya anaongoza msafara.
Uwepo wa lori usikuchanganye. Watu wanachoma Nissan Patrol mpya katika hii mipango ya kuondoa watu. Investigative journalism hapa unaanza kumtafuta dereva wa lori ni nani, lori ni la nani, lilipakia mziigo wapi, kupeleka wapi, dereva wa lori wanasema alipelekwa hospitali ila pale hayupo kahamishiwa hospitali nyingine - ipi, tuambieni basi, nk.
Kosa wanalofanya ni kusahau kwamba kamati ya ulinzi na usalama huwa haikimbilii kwenye kila tukio la ajali bila kuambiwa ni kigogo gani amepata ajali. Kukimbilia eneo la ajali ni kazi ya trafiki, na wakitambua ni kigogo aliyekufa ndio wanaitaarifu kamati ya ulinzi. Hapo ndipo Mkuu wa wilaya alipoboronga.
Nilidhani zimekwenda na naniliu!.
Could be just an amazing coincidence!.
P