Pamoja na Mvua kunyesha kuanzia Alfajiri huku Temeke , lakini mpaka sasa kwenye viwanja vya Bulyaga , ambako kuna Mkutano kabambe wa kupinga Mkataba mbovu na kupiga spana madalali wa Bandari za Tanganyika , watu wameanza kufurika .
Awali kuna Mamluki wakiongozwa na Maulid Kitenge au "KITENGE DP" kama anavyofahamika sasa , walisambaza uzushi wa kwamba Msajili wa Vyama vya siasa , Francis Mutungi , amezuia Mkutano huo , lengo la Mamluki hawa lilikuwa kuwachanganya wananchi ili wasihudhurie , hata hivyo kama tunavyosema siku zote kwamba SHETANI HAJAWAHI KUMSHINDA MUNGU , ndicho kilichotokea
Vikundi vya kutumbuiza wananchi tayari viko jukwaani , awali watu wa Afya (Red cross) walishafika viwanjani mapema asubuhi
View attachment 2696905
Updates
=======
Baba Askofu Mwamakula atoa siri kwamba wao kama viongozi wa dini wanajua mambo mengi kuhusu mkataba huu ndio maana wanaukataa , anasema ni vema tukauvunja sasa badala ya kusubiri yatukute ya Djibout .
Watu ni wengi mno ! Maagizo ya Mwaipopo yamegonga mwamba
View attachment 2697017