Bandari na DP World: Dkt. Slaa asema ni uuzaji wa Nchi. Adai Serikali iliyopo ina uhalali wa wasiwasi
Sawa kabisa tuwekeze kwenye bandari zetu, tuondoe mapungufu, tuboreshe utendaji na miundombinu lakini sio kuwapa wengine watufanyie hayo.
 
Balozi Dkt. Willibrod Slaa anazungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, leo Juni 13 2023 kuhusu hati ya makubaliano yaliyoingiwa kati ya Tanzania na DP World.

=======

Dkt. Slaa: Hadi kufikia hatua ya azimio hili kuridhiwa na Bunge, ikumbukwe makubaliano ya awali yalifanyika tarehe 28 February, kampuni ya DP World na bandari waliingia kwenye makubaliano yalitokana na shughuli iliyofanyika Dubai expo 2022, hatujaambiwa ni tathmini gani au utafiti gani ulifanyika

Kwenye expo, kwenye maonesho kama yale ya sabasaba Dar es Salaam watu wanaingia kwenye mkataba mkubwa wa kulifunga Taifa, nadhani mnaelewa hiyo maana yake ni nini!

Hadi wakati huu Taifa na watanzania walikuwa hawajapewa taarifa yoyote ile inayohusu mkataba mkubwa wa aina hiyo.

Naomba kuwakumbusha pia kuwa pamoja na mkataba huu, katika Dubai 2020 Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Rais mwenyewe kulisainiwa mikataba 17, nani kati yenu hadi leo hii anaifahamu mikataba 17 inahusu nini, ni usiri mtupu, ni nchi inaingizwa kwenye giza, Rais wa Nchi amehudhuria lakini mambo hayo yote yako ndani ya giza.

Waliohudhuria maonesho ni viongozi wa Serikali, wamesafiri, wamelala hoteli, wamekula chakula kwa kodi ya watanzania, ni Tanzania pekee ambako Serikali haiwajibiki kwa wananchi wake, jambo ambalo katika hatua hii, jambo ambalo linalazimisha kuwakumbusha uhitaji wa haraka wa katiba mpya na bora.

Hii taarifa tunayozungumzia hatukuipata Serikalini, tumepata taarifa iliyovuja. Ni nchi gani duniani tunasubiri taarifa ivuje tuanze kuizungumzia. Siku siku 30 zilizotajwa kwenye mkataba na Bunge, kwa maneno mengine umeridhiwa ndani ya siku 30 lakini umekuja kuridhiwa baada ya miezi takribani 8, kwa hali hiyo tuna uhakika gani Tanzania ina uwezo wa kutimiza mkataba huu kama mwanzo tayari ni mbaya na hakuna anayeeleza uchelewashaji huo unatokana na nini.

Dkt. ametoa hoja zifuatazo
  1. Dkt. Slaa: Nchi inayojulikana kisheria ni United Arab Emirates, Je Dubai ni Serikali? Dubai ni mji unaojiongoza, sisi ni nchi ya Jamhuri ambayo maamuzi yetu yanafanyika kwa kutumia Bunge. Bunge lilitangaza wanataka maoni ya wananchi tarehe 5 Juni wanaotoka maeneo mbalimbali wawe wamefika bungeni tarehe 6. Kwa saa 24 mtanzania gani anafika Dodoma na kutoa maoni yake. Ni dhahiri kuliwa na hila na Serikali haikuwa na nia ya kushirikisha wananchi wake. Hatukushirikishwa na imepelekwa bungeni na mjadala ulivyokuwa bungeni ulikuwa ni mjadala wa ki-mangimushi
  2. Aidha ikumbukwe Serikali iliyopo ina legitimacy ya wasiwasi kutokana na uchaguzi wa 2019 na 2020. Simung'unyi maneno, uchaguzi wa 2019 na 2020 inaweza kuwa na legitimacy lakini sina hakika kama uchaguzi huo ulikuwa sahihi, najua ulivurugwa kwa makusudi na chama cha mapinduzi na vyombo vyake. Mwenye macho haitaji kuambiwa kuhusu hilo na wananchi wote ni mashahidi.
  3. Kwa mujibu wa kifunge cha nne cha IGA kinatamka wazi rasilimali zote zilizotajwa zinakabidhiwa kwa Serikali ya kigeni. Rasilimali hizo ni bandari zote za nchi nzima(bahari, maziwa, mito, zitakazokuwepo hata kwenye mabwawa) yale yote yaliyokuwepo leo na hata yatakayokuja. Huu ni uuzaji wa nchi, hakuna mwenye Tanzania mwenye akili atakaekubali jambo hilo bila uhakika wa rasilimali zake hizo.
  4. Serikali ya awamu ya nne wakati inataka kutaifisha mashirika muhimu ikiwemo bandari, aliyetupa taarifa alifukuzwa kazi. Alitupa taarifa ya kutokubali kuyataifisha kutokana umuhimu wake kwa usalama wa Taifa.
    Dkt. Slaa ameongelea mfano wa mbia katika kampuni ya mafuta wakati wa vita ya Uganda ambapo Tanzania ilikuwa inamiliki 51% katika kampuni hiyo huku mbia akiwa na 49% lakini aliweka ngumu kwasababu alidai mtu tunayepigana nae ni mbia wake pia hivyo. Slaa amedai kwa siku 5 vifaa havikuweza kuondoka kwasababu ya mafuta wakati nchi inaendelea kupigwa.
  5. Slaa pia ametoa mfano wa 'Entebbe Raid' ambapo amesema ndege ya Air France ilitekwa nyara na wapiganaji wa Palastine wakishinikiza mambo yao ya kisiasa ndani ikiwa na waisraiel ilitua uwanja wa Entebbe. Slaa amedai Waisrael iliwachukua chini ya dakika 90 kuwakomboa watu wao na amedai iliwezekana kwasababu wao ndio waliojenga uwanja na ramani zote walikuwa nazo ikiwepo sehemu ya kuingilia na kutokea.
  6. Slaa amesema sababu hapo juu pia ilisababisha Serikali ya awamu ya tano itumie wajenzi wa ndani kujenga Ikulu lakini sasa bandari zote zinakabidhiwa kwa mgeni.
  7. Dkt. Slaa: Mkataba unaotoa 'exclusive rights' daima uogope, inatoa pia kifungu baadae yatakayojadiliwa kwenye mikataba midogo midogo, unatoa kwanza mali yako, unajuaje wakifika kwenye hiyo mikataba midogo midogo wakikutalia! Una nguvu gani, ulishasain 'exclusive rights'
  8. Utekelezaji wa DP World sio kwamba unaanza Tanzania, katika Afrika peke yake tuna migogoro mingi. Nenda nchi za Ulaya, Brussels ni yaUlaya laikini wako mahakamani, karibu kote kunakogombaniwa ni rushwa, kuna wabungwe walipelekwa, wakalishwa, wakapewa posho ya dola 2000 yote hiyo ni rushwa. Kama ingekuwa nchi nyingine, hizo zinatosha kufuta mkataba huu na kapeleka hata hiyo kampuni mahakamani.







Mh 🤔 ngoja waje akina GUSSIE lord denning and co. Wazee wa payroll tuone wanasemaje!!!
 
Kwa hili la bandari samia amewakosea sana waTanganyika na anaonekana kutokujali kabisa

Tumshtaki Kwa Mungu
 
Back
Top Bottom