Bank tellers ni wezi wa kimya kimya, kuweni makini

kuna watu nikiwakuta mbele yangu naondoka hilo tawi natafuta tawi lingine.

maana wana hela kwenye mabegi,ndani ya suruali,ndani ya makoti,nikimuona tu najua hapa sitoboi nageuka naenda tawi jingine
ukiwa mzembe kweli unatoa hela maana yeye akiongea anaongea kwa kujiamini haswa
 
Lakini kuna notes counter pale, anaweka buku buku zikifika 100 anafunga. Unaibiwaje?
Akiamua kukuibia anakuibia tu, wizi ni taaluma.
Pamoja na kukodoa macho anavyohesabu atakuangalia position uliyokaa, ataligeuza fungu kukuchagulia eneo la wewe kuona kisha haraka sana atatumia unyongovu wa mikono kutelezesha noti moja tu hutaona kabisa.
 
Kuna baadhi ya ma Teller ni vibaka. Mimi mwaka 2020 nilipigwa Hilo tukio mkoani. Nilienda bank kutoa milioni moja (ni fixed account-kuchukua hadi ndani tu,). Yule dada alienihudumia alinipiga elfu 20,000 bila Mimi kugundua maana sikuhesabu na ni kwa sababu alinipa za elf TANO nyingi na elfu kumi kidogo kwa hiyo nikaona uvivu kuhesabu. Baada ya muda mfupi kufanya baadhi ya mahitaj yangu ndo nikagundua nimepigwa 20,000 bank.

Wewe dada mwenye mwanya, mfupi, mwili wa wastani, mweusi kwa mbali uliyenipiga elfu 20,000 ktk tawi X hapo kanda ya ziwa acha hizo tabia ipo siku utaumbuka. Km humu umeskia.
 
😂😂😂Hatar sana
 
FNB kabla haijafungwa,coco plaza kuna braza man alinipiga laki 3...bahati yake nilikuwa nishaanza safari ndio nikastuka, nigemjazia nzi, usiamini mtu kwenye pesa,hesabu pesa zako ndio uondoke,na wakikujua unatabia ya ku count hawaibi!
 
Nadhani wanaona wakifanya hivyo watakuwa hawana tofauti na fremu za wakala
Mpaka mtu anapeleka fedha bank maana yake zimemzidi na anataka aiziweke haraka ili akaendelee na uzalishaji.

Madirisha yapo mengi ili kazi ya kufanya miamala iende haraka lakini imekuwa kinyume.
 
Levo zako mkuu,ndo watakuletea mlejesho.
Kwetu cc Kwanza Kama vile unataka tukujue unamiburungutu😄😄😄😄.

Anyway mashine huwa zipo za kuhesabia maburungutu mkuu.
Pesa nyingi unapewa chumba Cha falagha.
Kingine labda wenge lako mkuu⛷️.
Ziada,uchonganishi
 
Aisee Kuna jamaa aliwai nambia kapewa pesa bandia benki, ujue nilibisha mno[emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…