Bar ya Picnic Arusha Kuna wizi kuanzia wahudumu, Wateja Wanawake mpaka Bodaboda Wanaopaki nje

Bar ya Picnic Arusha Kuna wizi kuanzia wahudumu, Wateja Wanawake mpaka Bodaboda Wanaopaki nje

Wakuu Niko Arusha Kwenye Miangaiko Sasa Jana nikaenda Bar ya picnic Arusha, Sasa Wakati ñaenda Nikamwambia Mwenyeji wangu, yule Mwenyeji wangu akanambia kuwa makini Na picnic kuna wezi kama wote, nikamjibu Poa.
.
Lakini yule Jamaa akanambia watu wageni wanaogopa Sana Hapo maana ULINZI zero.
.
Nikafika pale nikaagiza Kinywaji Changu, Grants Ile Kubwa nikawa nanyonya mdogo², Sasa Kuna Binti akawa amekaa kaubta ananiangalia sana.
.
Badae akamtuma mhudumu akwambia, kamwambie yule Kaka nimempenda Jinsi alivyo mrefu na Rangi yake nyeusi nikasema asante.
.
Sasa nikaenda Chooni yule mwanamke ananikonyeza halafu for the time being akanifata chooni Ananambia mbn na kuita Uje Halafu hauji, Eti njoo ule nyama Sawa Nikamjibu Poa.
.
Ila Sikwenda maana nilishaambiwa Niwe makini na wahudumu+wateja, badaye kanifata nilipokaa Ananambia ninahamia Hapa Tukae Wote.
.
Wakati Huo Nimepaki Gari nje, Nikamjibu sitakaa Sana Ila nitaondoka Kwenda Kupumzikia, akajibu nitakusindikiza, Wala sikujibu chochote.
.
Badae Akili ikanambia Toka nje kaangalie gari, nikatoka Ila kabla sijatoka nje nikachukua Kinywaji Changu nikapeleka counter Kwa usalama zaidi.
.
Ila natoka nje kupiga macho Kwenye gari Naona Mtu Yuko ndani ya gari kusogea nakuta anafight kufungua radio, alivyoniona akakurupuka akataka kukimbia nikamuwahi nikampiga teke akaanguka Chini, nikampa teke lingine la Tumboni akatulia, nikaona gari ya Polisi wale Polisi wakaja wakaniuliza vipi nikawaelezea wakamchukua wakamweka Kwenye gari Yao.
.
Kurudi Kuangalia gari kumbe alivunja kioo Kidogo Akaingiza Mkono aka-unlock zile lock za milango.
.
Nikaenda kuwalezea Uongozi wa Bar Wala hawajali wanajibu majibu ya Kawaida Tu.
.
Nikachukia nikaenda nikachukua kinywaji Changu nikasepa.
.
Wakuu sitaki kumwaribia biashara Ila Pale Sio Pazuri Wezi ni Wengi Sana, na Sjui Uongozi wa Picnic Hawalijui Hilo.
Pole sana Mkuu,ina maana hapo kulikuwa na mawasiliano kati ya huyo mhudumu aliyesema amekuelewa na huyo mwizi.
 
Unaenda kulewa na gari kama sio kutafuta ajali za kijinga ni nini

Unataka kustarehe Acha gari Hotel uliyofikia au nyumba uliyofikia
La sivyo ni kujitafutia majanga tu au ni show off
Umeongea point.
Arusha kuna bolt na indrive, usiku hakuna haja ya kutembelea private ukienda kulewa

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Kipindi cha Kikwete kuna ambao walikuwa wanalipia bili zao kwa kutumia dola badala ya shiling sijui kwa sasa
 
Arifu next time ukija chuga nitafute mdau nikupeleke viwanja vya kistaarabu kabisa at least ukiwa na raia inakuwa full.. juzi kuna bro wamempiga iphone alikuwa anatoka tu bar nje kakutana na hao sijui wana pikipiki wakamweka kati wakamla iphone wakasepa dah wizi sasa hivi ni noma sana tuwe makini sana hali ni mbaya especially at night.
Hivi pale nyuma ya Mtei kilombero wanapaitaje?
Pamechangamka na usalama uko full

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Mi nilipigwa laptop mlimani city kwa staili hiyo hiyo
Halafu kwa kupitia walinzi nikainunua tena laptop ile ile ilikua ya ofisi na inavitu muhimu kweli.......... hii dunia yasipo kukuta hutaelewa mtu akikwambia utamuina mjinga
Niliinunua laptop yangu mwenyewe kudadeki
Mtu ukimwambia haya mambo anadhani masikhara 😂
 
Back
Top Bottom