Bar ya Picnic Arusha Kuna wizi kuanzia wahudumu, Wateja Wanawake mpaka Bodaboda Wanaopaki nje

Bar ya Picnic Arusha Kuna wizi kuanzia wahudumu, Wateja Wanawake mpaka Bodaboda Wanaopaki nje

Elimu ina gharama zake mkuu.
Mimi kamwe huwezi kunikuta bar hizi uchwara napendelea lounge tulivu na sehemu zangu ni kama.
Njooys, 40/40, kipong, Bills, tembo club nk.
Ni sehemu tulivu mno.
Hasa tembo club unakaa garden na kaubaridi kama upo Ulaya ndogo haha.


Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Kule pembeni ya Nakumati ya zamani, wanakokaa ngozi nyeupe Vip pale hukaagi , pemetulia nako
 
Mkuu kama unajirlewa nenda Andrew's, The Don, 40/40, Njooys, 2000 motel. nk
Hizo ni sehemu za watu wanaojielewa na sehemu kama hizo zipo nyingi.
Cocoriko bado nalo ni chimbo la kishamba tu kila changu anakimbilia pale.

Labda mimi kwasababu napenda sehemu tulivu.


Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Andrew ana chakula amazing sana

Na kule chobis kulivyojificha 😍 ni kutamu kwa kapoz
 
  • Changamoto iliyopo pale, ni kutokuwa na sehemu ya kuegesha magari, zaidi ya kuyaegesha barabarani.
  • Na gari ukiegesha barabarani, usalama wa chombo chako uko juu yako.
  • Kuhusu huyo dada wa ndani, inawezekana hana mahusiano yoyote na yule mwizi; zaidi ya huyo dada kutaka kujaribu bahati yake/ wengi wanaojiuza pale ubembeleza wanaume.
 
Nature yao wana mambo ya ubabe flani hivi,sasa wakishapiga na pombe confidence zinawazidi.Hata mimi nimeathirika kisaikolojia kuwa Arusha kuna wizi wa magari,sasa nikiwa na gari huwa nakuwa sina amani yani napenda nipaki gari mahali ambapo nitakuwa naliona...
Haaaaa Haaaaa Wizi wa magari ni zamani, yale majambazi yote yalishapigwa shaba yamelala chini. Sahivi ni nyokaa tu ndo zinasumbua mji
 
Hapo kaloleni kumekuwa Mahalia hatari sana kuna hao vijana wa bodaboda wanajulikana kwa jina la tatu mzuka wakikukuta unachezea mapanga ya kutosha wanachukua kila kitu na hapo kaloleni maaskari wapo muda mwingi sana ina maana hawajulikani Hawa tatu mzuka
Labda hao '3 mzuka' ni mradi wa hao askari!
 
Wakuu Niko Arusha Kwenye Miangaiko Sasa Jana nikaenda Bar ya picnic Arusha, Sasa Wakati ñaenda Nikamwambia Mwenyeji wangu, yule Mwenyeji wangu akanambia kuwa makini Na picnic kuna wezi kama wote, nikamjibu Poa.
.
Lakini yule Jamaa akanambia watu wageni wanaogopa Sana Hapo maana ULINZI zero.
.
Nikafika pale nikaagiza Kinywaji Changu, Grants Ile Kubwa nikawa nanyonya mdogo², Sasa Kuna Binti akawa amekaa kaubta ananiangalia sana.
.
Badae akamtuma mhudumu akwambia, kamwambie yule Kaka nimempenda Jinsi alivyo mrefu na Rangi yake nyeusi nikasema asante.
.
Sasa nikaenda Chooni yule mwanamke ananikonyeza halafu for the time being akanifata chooni Ananambia mbn na kuita Uje Halafu hauji, Eti njoo ule nyama Sawa Nikamjibu Poa.
.
Ila Sikwenda maana nilishaambiwa Niwe makini na wahudumu+wateja, badaye kanifata nilipokaa Ananambia ninahamia Hapa Tukae Wote.
.
Wakati Huo Nimepaki Gari nje, Nikamjibu sitakaa Sana Ila nitaondoka Kwenda Kupumzikia, akajibu nitakusindikiza, Wala sikujibu chochote.
.
Badae Akili ikanambia Toka nje kaangalie gari, nikatoka Ila kabla sijatoka nje nikachukua Kinywaji Changu nikapeleka counter Kwa usalama zaidi.
.
Ila natoka nje kupiga macho Kwenye gari Naona Mtu Yuko ndani ya gari kusogea nakuta anafight kufungua radio, alivyoniona akakurupuka akataka kukimbia nikamuwahi nikampiga teke akaanguka Chini, nikampa teke lingine la Tumboni akatulia, nikaona gari ya Polisi wale Polisi wakaja wakaniuliza vipi nikawaelezea wakamchukua wakamweka Kwenye gari Yao.
.
Kurudi Kuangalia gari kumbe alivunja kioo Kidogo Akaingiza Mkono aka-unlock zile lock za milango.
.
Nikaenda kuwalezea Uongozi wa Bar Wala hawajali wanajibu majibu ya Kawaida Tu.
.
Nikachukia nikaenda nikachukua kinywaji Changu nikasepa.
.
Wakuu sitaki kumwaribia biashara Ila Pale Sio Pazuri Wezi ni Wengi Sana, na Sjui Uongozi wa Picnic Hawalijui Hilo.
Kwan bar ipo moja si ungeenda bar zingine zenye usalama au ulikua na lako jambo mzee
 
Back
Top Bottom