Baraza la Mitihani (NECTA) latangaza matokeo ya Kidato cha nne 2023. Ufaulu waongezeka

Baraza la Mitihani (NECTA) latangaza matokeo ya Kidato cha nne 2023. Ufaulu waongezeka

Nimeshangazwa tu manake enzi zangu 1.7 zilikuwa hazizidi 15 nchi nzima ,pia siwezi chukizwa na matokeo Yao manake Sina direct affiliation na hao wahitimu...

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Matokeo yamekosa mvuto kabisa .

Enzi zetu ukipata division one achilia mbali one ya single digit utaheshimika mno.

Na ukipata one ya 7 mpaka bungeni utaitwa
 
Miaka hio walimu walikuwa wachache sanaaa, uhaba wa vitabu, mwamko duni wa wazazi kusapoti wanafunzi,

Saizi dogo anaenda advance mzazi anatenga 300k anampa vitabu tu, kwann madogo wasifaulu,

Enzi zenu shule nzima kuna Chand 5, saiz kila mtoto ana chand
Hiyo sio sababu.

Shule kama Feza ambazo mwanafunzi anapta kila anachokihitaji lakini division three, four zilikuwa hazikosekani

Serikali imepanua goli na wanazidi kushusha thamani ya elimu.
 
Madogo wameitendea vyema shule yao.
735928126.jpg
 
Shule za private lazima wafike mbali ,kwanza ni vipanga cha pili wana uelewa mzuri wa lugha .... CCM wakitaka shule zote ziwe swa lazima waanze kufundisha kingereza tangu ngazi ya primary.

Wanabadilisha syllabus ila wanajizungusha tu , kama mlipanga kufuata elimu ya mzungu basi fuateni na lugha yake.


Miaka 7 kiswahili halafu miaka 4 kingereza ndio uchawi unaanza hapo...Nasikitika sana Prof Mkenda nae hamna kitu kabisa anashindwa kujua hili tatizo hata kujifunza kutoka kwa international schools na private.
 
Kwa shule za serikali tena za mjini uzembe ni wanafunzi wenyewe..
Wazazi hawatoi usimamizi mzuri kwa watoto, wanashindia tamthilia, miziki tu.

Shule hiyohiyo walimu walewale iweje wengine wapate division 1 wengine 4 na 0

Labda shule za vijijini hapo kweli.
 
Mods NIACHIENI uzi wangu kama ulivyo, msipeleke popote! Mnanionea sana.

-Wote wamefaulu, wachacheeeee ndo wamefeli.
-I.7 kama zote........
-Shule kubao zina ufaulu wa daraja la kwanza tu basi.....
-Watajaa chuo cha sheria Tanga hadi watapwakuka. Wakishamaliza wanarudi kuja kuingiza nyimbo kwenye simu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimesikia mwaka huu Shule za Sekondary za serikali (Umma) zaongoza kwa ufaulu

Tunaomba kwa matokeo ya shule za msingi na Sekondari; wawe wanaweka

1. Matokeo ya shule za umma wakionyesha ufaulu wa kila somo BILA KUSAHAU HESABU na matokeo ya shule za binafsi (private)

2. Mwishoni wanaweza kuweka matokeo ya ujumla

Naamini hiyo ni kazi rahisi sana wala haihitaji utaalam maalum hivyo tunatamani kuona hivyo

Na hii ndio itasaidia kwani wakisema PUBLIC/PRIVATE wanaongoza na sisi tuone wameongoza wapi (kwenye somo gani, au Div 1 au pengine Div 4?
 
Mnaziponda sana shule za umma na kuziona ni dhaifu wakati mtaala na walimu ni hawahawa wa vyuo vyetu vya ualimu. Zama za ku promote shule za private zimepitwa na wakati, ni shule za kawaida tu kama za umma tena afadhali shule za umma zina walimu wa uhakika.
 
Always shule za umma ndio zitaendelea kuwa bora kwa kila category. Tumechoka na promo za shule za private wakati hakuna cha maana kuzidi shule za umma.

Private zina walimu wa kuungaunga kiasi kwamba wengine hawana taaluma ya ualimu mradi tu mtu anaweza kubabaisha kwenye masomo fulani aliyoyasoma A Level/o level /mhitimu wa chuo fulani/fani/taaluma fulani anapewa darasa akababaishe huko na akishindwa anatimuliwa kama kocha wa timu ya mpira wa miguu.

Serikali inaajiri walimu waliosoma ualimu na kufaulu, ni wa kudumu na wanamudu ufundishaji wanafunzi tofauti na shule za private wanaokoteza walimu na kuwalipa mshahara mdogo watakavyo
 
Hii shule hiko Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani. Hii shule inamatatizo ya matokeo ya mitihani yake kutokutolewa kwa baadhi ya miaka kwa ngazi tofauti tofauti. Kwa mfano matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa jana yameshikiliwa. Inaonekana hii shule ni kanjanja kanjanja? Wazazi shituka vingine itakula kwenu!!
 
Kabla ya kumlaumu mwalimu angalieni mazingira ya watoto wenu huko majumbani.
Shule za private zinazojitambua during holiday kwenye barua kwenda wazazi wanaonya kabisa watoto wadhibitiwe - simu, tv, mavazi, makundi, nk. wawapo likizo. Mwezi mmoja tu wa likizo unatosha kumharibu mtoto completely asipokuwa controlled ipasavyo. Sasa hao wenzangu na mie uswahilini huku who cares? Sio. Mzazi, sio ndugu wala jamii inajali!
 
Back
Top Bottom