PreGE2025 Barua rasmi ya Tundu Lissu kwa Watanzania kutoka gerezani Ukonga

PreGE2025 Barua rasmi ya Tundu Lissu kwa Watanzania kutoka gerezani Ukonga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Leo May 3, 2025, Tundu Lissu ametuma barua ya wazi kwa watanzania akiwa kolokoloni gereza la ukonga.

Barua hii imechapishwa na Maria Sarungi kupitia mtandao wa X kama ifuatavyo,

Barua rasmi ya Lissu kwetu sote! Alituma kwa Kiingereza neno kwa neno kupitia mtu aliyenifikishia na nimeweka hapa chini 👇🏾 tafsiri isiyo rasmi

Nalaani vikali shambulio dhidi ya Padre Dk. Charles Kitima na kushambuliwa kwa kipigo kikali na kutekwa kwa Mdude Nyagali. Rais Samia na Serikali yake wanahusika na vitendo hivi viovu vya kigaidi. Natoa wito kwa Rais Samia na serikali yake kuhakikisha kuwa Mdude Nyagali anaachiwa mara moja na anapata huduma ya dharura ya matibabu anayohitaji.

Kwa Padre Kitima, namtakia ahueni ya haraka na kumsihi yeye na Maaskofu wa Tanzania kudumisha misimamo yao thabiti na yenye misingi mikuu katika mapambano ya kudai Tanzania ya haki, usawa na demokrasia.

Kwa viongozi wa CHADEMA, wanachama, wapenzi, na wananchi wa Tanzania kwa ujumla, nawaomba kutokata tamaa wala kukatishwa tamaa katika kupigania demokrasia ya nchi yetu. Ninataka wajue kwamba nipo thabiti kabisa na siyumbishwi, na hakuna kuta za gereza zitavunja roho yangu. Ninawapenda wote, na nitarudi.

P.S. Nisipopelekwa kortini Jumanne kama inavyostahili, nitaanza mgomo wa kula."

Tundu Antiphas Mughwai Lissu.
(Gereza la Ukonga).

Siyo barua kwa Watanzania hii. Ni kwa wajomba wale wanaonyimwa usingizi na Putin. Huu ndio ushamba wa CHADEMA. Watu wenu ni waswahili mnaandika barua kwa Kingereza. Ulaya wenyewe yakwao yanawashinda kila siku wanaota Putin kaingia Poland...mnadhani wana muda na ya kwenu?

Trump anafunga balozi karibu 30 za Marekani Afrika. Mambo ya Tanzania malizeni na watanzania wenzenu. Kaeni meza ya mazungumzo. Friedrich Merz hawezi amrisha Tanzania, mwenyewe Ujerumani anasumbuliwa na manazi wa AfD.🙏🙏🙏
 
Naona lissu ameamua kuanza kufanya diet kupunguza kitambi.
Lile tumbo kwa kweli lilihitaji maboresho kidogo lilizidi sana kazi ingemshinda.

20250503_155615.jpg


Sisi ngoja tupate maakuli tupitishe siku. Wadau karibuni tule au na nyinyi mtaingia kwenye mfungo kuonesha support kwa lissu?
 
Watanzania wengi wanaongea lugha gani ? Diaspora watamuelewa ila wakitaa ingeandikwa Kiswahili...
 
Back
Top Bottom