PreGE2025 Barua rasmi ya Tundu Lissu kwa Watanzania kutoka gerezani Ukonga

PreGE2025 Barua rasmi ya Tundu Lissu kwa Watanzania kutoka gerezani Ukonga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mbowe asingeweza kuandika hicho kingereza .

Ila Lisu sio mtu sahihi kwa Chadema.
 
Siyo barua kwa Watanzania hii. Ni kwa wajomba wale wanaonyimwa usingizi na Putin. Huu ndio ushamba wa CHADEMA. Watu wenu ni waswahili mnaandika barua kwa Kingereza. Ulaya wenyewe yakwao yanawashinda kila siku wanaota Putin kaingia Poland...mnadhani wana muda na ya kwenu?

Trump anafunga balozi karibu 30 za Marekani Afrika. Mambo ya Tanzania malizeni na watanzania wenzenu. Kaeni meza ya mazungumzo. Friedrich Merz hawezi amrisha Tanzania, mwenyewe Ujerumani anasumbuliwa na manazi wa AfD.🙏🙏🙏
Kuna Mzungu katajwa humo? Ametumia lugha kubwa ili aeleweke ndani na nje ya nchi. Tanzania ni mwanachama wa jumuia za kimataifa!
 
P.S. Nisipopelekwa kortini Jumanne kama inavyostahili, nitaanza mgomo wa kula."
Katika sheria za kimataifa, mgomo wa kula unaofanywa na mfungwa wa kisiasa ni suala nyeti linalogusa haki za binadamu, maadili ya kitabibu, na wajibu wa kisheria wa taasisi za kifungo. Hapa kuna athari kuu na mitazamo ya kimataifa kuhusu jambo hili:


1. Haki za Binadamu​


Mfungwa wa kisiasa ana haki ya kuamua kutokula kama njia ya kuonyesha upinzani au kudai haki zake. Hii ni sehemu ya uhuru wa dhamira, maoni, na kujieleza, ambayo inalindwa na mikataba kama vile:


  • International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR)
  • Universal Declaration of Human Rights (UDHR)

2. Maadili ya Kitabibu​


Kulingana na Tamko la Malta la Chama cha Madaktari Duniani (WMA), ikiwa mfungwa mwenye akili timamu anagoma kula kwa hiari:


  • Hatakiwi kulazimishwa kulishwa (force-feeding) kwani hiyo ni mateso na ukiukaji wa utu.
  • Madaktari wanapaswa kuheshimu uamuzi wake, lakini pia wawe wakimfuatilia kiafya kwa karibu.

3. Majukumu ya Kisheria ya Serikali/Mamlaka za Gereza​


  • Serikali ina jukumu la kuhakikisha usalama na uhai wa wafungwa wake.
  • Inaposhindwa kutafuta suluhisho la kibinadamu, inaweza kushutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu mbele ya vyombo kama Mahakama ya Haki za Kibinadamu (k.m. European Court of Human Rights).

4. Athari Kwa Mfungwa​


  • Kisaikolojia na kimwili, mgomo wa kula unaweza kusababisha kudhoofika kwa afya, ulemavu wa kudumu, au hata kifo.
  • Mara nyingine serikali hutumia hali hiyo kumchafua hadharani au kumbadilisha kuwa “mtu asiye na akili timamu.”

5. Athari kwa Serikali au Jamii​


  • Inaweza kuibua taharuki ya kimataifa na shinikizo kutoka mashirika ya haki za binadamu.
  • Mara nyingine huchochea mageuzi au kuamsha uungwaji mkono kwa mfungwa kisiasa.
 
Leo May 3, 2025, Tundu Lissu ametuma barua ya wazi kwa watanzania akiwa kolokoloni gereza la ukonga.

Barua hii imechapishwa na Maria Sarungi kupitia mtandao wa X kama ifuatavyo,

Barua rasmi ya Lissu kwetu sote! Alituma kwa Kiingereza neno kwa neno kupitia mtu aliyenifikishia na nimeweka hapa chini 👇🏾 tafsiri isiyo rasmi

Nalaani vikali shambulio dhidi ya Padre Dk. Charles Kitima na kushambuliwa kwa kipigo kikali na kutekwa kwa Mdude Nyagali. Rais Samia na Serikali yake wanahusika na vitendo hivi viovu vya kigaidi. Natoa wito kwa Rais Samia na serikali yake kuhakikisha kuwa Mdude Nyagali anaachiwa mara moja na anapata huduma ya dharura ya matibabu anayohitaji.

Kwa Padre Kitima, namtakia ahueni ya haraka na kumsihi yeye na Maaskofu wa Tanzania kudumisha misimamo yao thabiti na yenye misingi mikuu katika mapambano ya kudai Tanzania ya haki, usawa na demokrasia.

Kwa viongozi wa CHADEMA, wanachama, wapenzi, na wananchi wa Tanzania kwa ujumla, nawaomba kutokata tamaa wala kukatishwa tamaa katika kupigania demokrasia ya nchi yetu. Ninataka wajue kwamba nipo thabiti kabisa na siyumbishwi, na hakuna kuta za gereza zitavunja roho yangu. Ninawapenda wote, na nitarudi.

P.S. Nisipopelekwa kortini Jumanne kama inavyostahili, nitaanza mgomo wa kula."

Tundu Antiphas Mughwai Lissu.
(Gereza la Ukonga).

Hebu wekeni barua og,
 
Kwenye kugoma kula awe makini asifikie kudhoofu kama kiiza Besiyge kiongozi mkuu wa upinzani wa Rais Museveni. Alitumia hii mbinu akadhoofu kiasi cha kushindwa kutembea.
No Reform No Election.
 
Back
Top Bottom