nderingosha
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 4,285
- 3,254
mkuu pamoja sana ila nawe usimungunye maneno, Zitto need to play as a team. Yeye anamjua alieleta hio barua. asitufanye kuwa hatunazo. Yani alishindwa kukaaa na Slaa wakajadiliana mpaka barua? email si wanazo? is that too formal? wenye akili wote tunajua jinsi gani Zitto asivyoshirikiana na wenzake.
Kwa hiyo Mh. Zitto, unataka kusema hata ile video ilianzia CHADEMA ndo ikaenda mtandaoni kama ilivyotokea kwenye barua yako? Kwa kifupi, namaanisha kuwa hiyo video ya Lwaka ni REAL plot ya CDM?4. Baada ya kufanya uchunguzi mdogo nimegundua kuwa ID iliyoweka video ya Lwakatare mtandaoni na ID iliyoweka barua hii mtandaoni ni IDs za mtu mmoja. Coincidence ya namna hii inashangaza na kushtusha, lakini inatuambia jambo moja kubwa
Mara zote nimeamini kuwa BILA CHADEMA imara, CCM itakuwa kama simba aliyekabidhiwa bustani yenye swala! Itafuja kila kilicho mbele. Chadema ikiwa imara, Tanzania itakuwa imara.
Acha kujifanya juha bana, sasa hapa Zitto amekuja kuimba bongo flava.
mkuu pamoja sana ila nawe usimungunye maneno, Zitto need to play as a team. Yeye anamjua alieleta hio barua. asitufanye kuwa hatunazo. Yani alishindwa kukaaa na Slaa wakajadiliana mpaka barua? email si wanazo? is that too formal? wenye akili wote tunajua jinsi gani Zitto asivyoshirikiana na wenzake.
...huyu Ben simuamini kabisa...kaeni macho viongozi wa CHADEMA huenda kuna mtu amekuja CDM kwa lengo la maangamizi kisha akishamaliza atimue zake.....well said Zitto. Nina ushauri muhimu sana sana kwako....kama ambavyo nimekua nikifanya nionapo mambo si mazuri CDM...Katika kufuatilia hali ya mambo CDM(kupitia post zenu humu JF)..nimegundua kuwa wewe mh.Zitto pamoja na mtu anayejiita Ben Saanane hamna uhusiano mzuri....kwa maana ya kutoleana shutuma humu...haswa Ben Saanane.Pale ambako amekua akikuhusisha wewe na masalia waliotemwa CDM....huku akisahau kuwa naye alikua kundi hili la masalia lakini hakufukuzwa (kama wenzake)...Inakua inaniuma sana napoona Ben anakuja kukutuhumu humu JF wewe mara kwa mara....wakati alitakiwa akutafte na mkae mmalize tofauti zenu...jambo ambalo mi naona ni jema kwa maslahi ya chama chenu.....Nasema hivi kwa kuwa mtu aliyetuma maneno ya barua yako humu ni mtu aliye ndani ya CDM...na ni mtu asiyekutakia wewe mema ndani ya CDM....Kwa hiyo ninakushauri fanya hima mtafutane na Ben (kwa uzuri tu)na kwa manufaa ya chama...tafuteni reconciliation...malizeni tofauti zenu ili mkijenge chama...Mimi binafsi nina imani sana nawe kama kiongozi mahiri wa CDM...na sipendi nione unachafuliwa.....kama ambavyo sipendi nione Dr.Slaa au Mh.Mbowe wakichafuliwa humu JF....Nakushauri sana..kama bado hamjamaliza tofauti zenu na Ben.....malizeni....kwa manufaa ya CDM....Najua umewahi kusema humjui Ben Saanane...basi ni vizuri umtafute...kupitia wanaomjua...ili mumalize tofauti zenu....huwa nashindwa kuelewa lengo haswa la Ben kutoa shutma kwako humu JF...na kwa maana hiyo mtu wa kwanza kwa wewe kumjua ni huyu....
Hapana! ninachosema ni hawa viongozi kutozungumza hata kwenye simu,bar,kahawa nk kushare mambo fulani mapya tena kwa kucheka,kutaniana,kujadili namna na mipango kama hiyo.mfano wewe uko kwenye familia ukiona jambo fulani linalogusa familia unaweza kumjulisha mwenza juu ya jambo na kusudio lako la kuchukua hatua ya awali licha ya kuwa kila mmoa ana uwezo na maoni yake!.
hawa viongozi wako hivyo? au wanakutana kwenye vikao na kuandikiana barua? basi kama ndivyo kuna tatizo kubwa!
Uongozi ni wajibu na ukisha kuwa kiongozi suala la 'haya ni maoni yangu' kwa kiasi kikubwa upungua sana na hakina unanyoweza kujitetea.
zito ni naibu katibu mkuu,coments zake kama hizi haziwezi kukijenga chama chao,bali kuwavuruka tu.
kila mtu anasema lolote,issue eti ni maoni yake?
Nani kakwambia uchunguzi aujafanyika???umemsikiliza Lissu??weMarioo vipi weweMh Zitto
Chadema have failed to practice what they preach,
Huwezi kuwashinikiza wengine wajiuzuru kupisha uchunguzi wakati yakitokea kwenu mnawakingia kifua bila kufanya uchunguzi kwanza.
ungekuwa na chembe ya hekima ungeizungumzia ccm na mafanikio yenu ya kuweka virusi. Kwani wewe ulijiuzuru au ulifukuzwa? Ndiyo maana dr. Alex paurine amefanikiwa kutushawishi una magonjwa yanayohitaji immediate attension.
Watu bana utajuaje kama ndo mpango wa chama kuwasilisha kitu kwa njia ya barua afu ndo kinajadiliwa.....ila sishangai mitanzania ndo tulivyogo na aliyetueoga ashakufa aisee hatuezi kuona mazuri na kusifia na kumpa moyo mtenda mazuri hayo azidi kutenda na kua juu zaidi.... lazima vikasoro muanze.....Mkuu nimekupata vizuri sana.Huwa napata wakati mgumu sana na kijana huyu "Zitto"nimejaribu kuangalia ushauri wake kwa chama ni mzuri mno.Nilikua najiuliza kwa nini aandike barua, wakati hii ni serious issue ambayo angeweza kukaa kitako na katibu wake mkuu na wakaijadili kwa kina kwani ni suala linalohitaji muda wa kutosha?Lakini jambo la pili, je haiwezekani kwamba yeye aliandika hii barua huku akijua italeak then atoe maoni yake na kuonekana yuko vizuri?Kwenye hili napata picha Zitto kuna kitu anakijua hivyo amejiandalia mazingira ya kuja kuonekana ni Mr. clea.Nimejaribu kuangalia tena kirusi anachokizungumzia ,nikapata picha pengine inaweza kuwa hicho kirusi, ndicho kinachotafutwa CDM kwani ,inawezekana kuwa ndio Kikwazo kwa Zitto na kundi lake kutekeleza malengo yao.najaribu pia, kuangalia urafiki wa Zitto na Msacky, pia uhusiano wa Zitto na baadhi ya mafisadi,nahitaji kumjua Zitto vizuri.
Ila yote katika yote,nawapongeza walioratibu mpango mzima wa kuisambaratisha CDM,umepangwa kwa Ustadi wa hali ya juu sana.Ndio maana haikuwawia vigumu CCM kuanza kuzungumza kwenye Press kuwa CDM itasambatratika.Hapa ndipo nataka kuona umahili wa Viongozi wa CDM, wakilivuka hili nina imani CDM itakua imekomaa vilivyo.Huu mtego una vikwazo vingi sana.