Kujipendekeza, kujiapisha, kupayuka, kujisemea, upofu, upogo na kutochelea kesho. Sijui ataramba matapishi yake au kufunika kombe. Ila Mungu anamuona, umma unamuona na sijui kwanini aliyemteua alisahau nadhili hii ya kichovu. Unajua limbukeni na maskini akipata. Hawa madaktari wa Bongo wa kuungaunga wana taabu sina mfano. Kama Bashiru angekuwa muungwana, kama alivyojiapiza angekataa ua kuomba kikombe hiki kimuepuke. Kwa vile ni mchumia tumbo na mnafiki, atanywea na kula mahanjumat. Hawa ndiyo aina ya viongozi tulio nao. Kazi kweli kweli. Shame on you Bashiru.