Basi Kampuni ya Baraka kutoka Newala - Dar lapata ajali na kusababisha vifo 14
Ajali imetokea kijiji cha Mtama majira ya saa 2 asubuhi, gari ilifeli breki ikiwa inateremka mlima Kinolombedo kabla ya kuufikia huo mteremko gari ilikuwa kasi sana kiasi wananchi wa vijiji jirani wakawa wanajiuliza mbona baraka inatembea kama inaendeshwa na wezi.

Ilipofeli breki pale mteremkoni, konda aliamriwa kushuka na kukimbia kutupa mawe barabarani ili gari isimame lakini gari haikuweza kusimama wala kupunguza mwendo, ilipasua hayo mawe na ikaendelea kushuka kwa mwendo mkali, dereva akamuamuru Konda wa kike ambae alibaki ndani aende nyuma kabisa ya gari kwa sababu alishahisi gari inaweza kupata ajali.

Baada ya kumaliza mteremko gari ilifika eneo la Kona kali mbili (Kona ya Nyale), dereva alifanikiwa kuimaliza kona ya kwanza, alipoianza kona ya pili gari ikachepuka ikaingia kwenye karavati, kutokana na ilishafeli breki na iko kasi ilidunda tu kwenye ule mfereji wa karavati na ikarudi tena barabarani na ilivyofikia pale kwenye karavati ikatimua mzinga wa nyuki kwahiyo fungu la nyuki likaingia ndani ya gari, taharuki ikawa kubwa, wakati huo gari imechomoka kwenye karavati ipo barabarani imeinama inatembea kwa matairi ya upande mmoja.

Gari inatembea kwa taili za upande mmoja + Nyuki wanawashambulia Presha ya abiria ikawa kubwa wakaanza kutaka kuruka kupitia madirisha, wengi wakawa wapo madirishani wameshatokeza vichwa nje kwa kuruka, ile gari kutokana na ilitembea kwa taili za upande mmoja kwa sekunde kadhaa na watu walishajaa madirishani kutaka kuchomoka ikadondoka kwa upande kwa bahati mbaya zaidi upande wa chini ulipofikia gari barabarani ndio upande watu walitaka kutokea, gari iliburuza ule ubavu ikiwa barabarani kipande kama cha mita 15 (kwa makadirio) mpka ikatoka barabarani ma kufika pembeni, Watu wakawa wameshasagwa vichwa na viungo vingine, barabara ilitapakaa maini, mautumbo, umeshuhudiwa moyo wa mtu unadunda kwenye nyasi, kuna maiti fulani ilikatika kiunoni vipande viwili, Rasta man mmoja alichinjwa shingo yake, dada mmoja alisafiri nae akabeba kichwa cha rasta kukileta kwenye ambulance. Waliosafiri pamoja ikitokea mmoja amepona anatafuta maiti ya mwenzake kwa kuangalia nguo aliovaa sio sura au mwili.

Usaidizi na utoaji abiria nje ulikuwa mgumu kutokana na nyuki ambao walijaa ndani ya gari wakifanya mashambulizi, wakazi walijitahidi kuwatoa abiria kwenye gari wakiwa maiti ma wengine majeruhi, pia majeruhi wengine ni wakazi wa mtama ambao wamenga'atwa na nyuki kwa kiasi kikubwa mpka wakazidiwa, Ambulance 2 na gari ya Polisi Mtama zilitumika kukimbiza majeruhi hospitali.

Ajali imeua pia mkazi mmoja wa mtama ambae ni mzee akienda shamba akiwa kwenye baiskeli yake, gari ilivyoanguka ilimkusanya na yeye.

Maiti 5 zilichelewa sana kutolewa kutokana na zilikandamizwa chini na gar, na kati ya hizo mbili ziliunganishwa Kama mshikaki na chuma kwahiyo kukata kile chuma ilikuwa ni kazi ya masaa, sijui walitolewa saa ngapi lakini mpaka saa 7 bado ngoma ilikuwa ngumu.

Braza mwanajeshi ambae ulichomoka kwenye ajali na ukutaka kukaa hata dakika 10 ukidai unawahi kuripoti kambini Zanzibar natumai umefika salama.

Ajali ya Baraka pale Mtama ni mbaya sana. Mungu awarehemu wote waliotangulia mbele za haki ma awaponye majeruhi wote waweze kurudi kwenye majukumu yao kwa haraka.
Pole,umeandika tukio kwa undani,natumai umeokoka
 
Kwa maelezo ya kufeli breki..

Kosa hapo ni la Dereva. Ndio.

Dereva siku zote ni yule wa kujihami na wa kufanya MAAMUZI sahihi ktk wakati sahihi.

Gari ukishaona hii breki hakuna kuna mechanism nyingi mno za kufanya ikumbukwe hilo ni Bus na nafkir ni Manual hiyo gari. Kuna kufanya change down technique kuna kuvuta handbrake ambayo mfumo wake hausiani kbd na brek za kawaida haiwezi hii mifumo miwili yote ikafeli kwa pamoja.

Na gari hizi zina Emergency brake mbili.
Ok tuseme zote zimefeli. Alishindwa nini kutoa tahadhari kwa abiria muda huo akitafuta KICHAKA au Miti midogo Ni heri uuwe wawili au chombo kiumie kuliko watu wote hao.

Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi ndio silaha kubwa sana ya kupunguza makali ya ajali.
Na pale kuna ukuta na shimo ni bora angeipiga ukutani, nadhan alijiaminisha kuwa atatoboa hadi chini na ile speed
 
Alafu kingine gari sio kama Binadamu useme utakufa tu ghafla.. ktk vyombo vya moto hasa ktk upande wa breki kuna Viashairia vingi tu ila tunapuuzia mfn kuwaka kwa taa ya ABS.. upepo kukosekana.. etc..

Bado nawaza:
1_ Breki zifeli (Regular / ABS)
2_ Emergency Brake ifeli (1)
3_ Emergency Brake ifeli (2)

Na magari mengi yanatembea hizi brake za emergency zikiwa zimekufa. Ndio maana wakipaki wanaweka vijiwe/gogo. Ukiona gari ikapaki wametega mawe ujue hamna parking/E_brakes hapo.

Sasa balaa linakuja hizi normal brakes zikifeli means hauna options tena (hauna chako hapo).

Hii kampuni ichunguzwe.
yaani bora wasingizie imekata (link) ile chuma ya steering rack, wakisema imefeli breki moja kwa moja ni uzembe wa maintenance na wanatakiwa kuwajibika kwa uzembe wa hali ya juu.
 
Roho 14 za watu zimezimika hapo.

Bado madereva wa mabasi wanacheza na roho za watanzania.
20231127_134452.jpg
 
Ajali imetokea kijiji cha Mtama majira ya saa 2 asubuhi, gari ilifeli breki ikiwa inateremka mlima Kinolombedo kabla ya kuufikia huo mteremko gari ilikuwa kasi sana kiasi wananchi wa vijiji jirani wakawa wanajiuliza mbona baraka inatembea kama inaendeshwa na wezi.

Ilipofeli breki pale mteremkoni, konda aliamriwa kushuka na kukimbia kutupa mawe barabarani ili gari isimame lakini gari haikuweza kusimama wala kupunguza mwendo, ilipasua hayo mawe na ikaendelea kushuka kwa mwendo mkali, dereva akamuamuru Konda wa kike ambae alibaki ndani aende nyuma kabisa ya gari kwa sababu alishahisi gari inaweza kupata ajali.

Baada ya kumaliza mteremko gari ilifika eneo la Kona kali mbili (Kona ya Nyale), dereva alifanikiwa kuimaliza kona ya kwanza, alipoianza kona ya pili gari ikachepuka ikaingia kwenye karavati, kutokana na ilishafeli breki na iko kasi ilidunda tu kwenye ule mfereji wa karavati na ikarudi tena barabarani na ilivyofikia pale kwenye karavati ikatimua mzinga wa nyuki kwahiyo fungu la nyuki likaingia ndani ya gari, taharuki ikawa kubwa, wakati huo gari imechomoka kwenye karavati ipo barabarani imeinama inatembea kwa matairi ya upande mmoja.

Gari inatembea kwa taili za upande mmoja + Nyuki wanawashambulia Presha ya abiria ikawa kubwa wakaanza kutaka kuruka kupitia madirisha, wengi wakawa wapo madirishani wameshatokeza vichwa nje kwa kuruka, ile gari kutokana na ilitembea kwa taili za upande mmoja kwa sekunde kadhaa na watu walishajaa madirishani kutaka kuchomoka ikadondoka kwa upande kwa bahati mbaya zaidi upande wa chini ulipofikia gari barabarani ndio upande watu walitaka kutokea, gari iliburuza ule ubavu ikiwa barabarani kipande kama cha mita 15 (kwa makadirio) mpka ikatoka barabarani ma kufika pembeni, Watu wakawa wameshasagwa vichwa na viungo vingine, barabara ilitapakaa maini, mautumbo, umeshuhudiwa moyo wa mtu unadunda kwenye nyasi, kuna maiti fulani ilikatika kiunoni vipande viwili, Rasta man mmoja alichinjwa shingo yake, dada mmoja alisafiri nae akabeba kichwa cha rasta kukileta kwenye ambulance. Waliosafiri pamoja ikitokea mmoja amepona anatafuta maiti ya mwenzake kwa kuangalia nguo aliovaa sio sura au mwili.

Usaidizi na utoaji abiria nje ulikuwa mgumu kutokana na nyuki ambao walijaa ndani ya gari wakifanya mashambulizi, wakazi walijitahidi kuwatoa abiria kwenye gari wakiwa maiti ma wengine majeruhi, pia majeruhi wengine ni wakazi wa mtama ambao wamenga'atwa na nyuki kwa kiasi kikubwa mpka wakazidiwa, Ambulance 2 na gari ya Polisi Mtama zilitumika kukimbiza majeruhi hospitali.

Ajali imeua pia mkazi mmoja wa mtama ambae ni mzee akienda shamba akiwa kwenye baiskeli yake, gari ilivyoanguka ilimkusanya na yeye.

Maiti 5 zilichelewa sana kutolewa kutokana na zilikandamizwa chini na gar, na kati ya hizo mbili ziliunganishwa Kama mshikaki na chuma kwahiyo kukata kile chuma ilikuwa ni kazi ya masaa, sijui walitolewa saa ngapi lakini mpaka saa 7 bado ngoma ilikuwa ngumu.

Braza mwanajeshi ambae ulichomoka kwenye ajali na ukutaka kukaa hata dakika 10 ukidai unawahi kuripoti kambini Zanzibar natumai umefika salama.

Ajali ya Baraka pale Mtama ni mbaya sana. Mungu awarehemu wote waliotangulia mbele za haki ma awaponye majeruhi wote waweze kurudi kwenye majukumu yao kwa haraka.
Ajali mbaya sana.
 
Kwa maelezo ya kufeli breki..

Kosa hapo ni la Dereva. Ndio.

Dereva siku zote ni yule wa kujihami na wa kufanya MAAMUZI sahihi ktk wakati sahihi.

Gari ukishaona hii breki hakuna kuna mechanism nyingi mno za kufanya ikumbukwe hilo ni Bus na nafkir ni Manual hiyo gari. Kuna kufanya change down technique kuna kuvuta handbrake ambayo mfumo wake hausiani kbd na brek za kawaida haiwezi hii mifumo miwili yote ikafeli kwa pamoja.

Na gari hizi zina Emergency brake mbili.
Ok tuseme zote zimefeli. Alishindwa nini kutoa tahadhari kwa abiria muda huo akitafuta KICHAKA au Miti midogo Ni heri uuwe wawili au chombo kiumie kuliko watu wote hao.

Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi ndio silaha kubwa sana ya kupunguza makali ya ajali.
NYUKI nao walizidisha taharuki, itakuwa na yeye kiwewe kilimpata. Watu wengine kwenye matatzizo ndio wanapanic mpka wanazidi kuharibu
 
Back
Top Bottom