Basi la Mwendokasi limeua mtu Kariakoo, Dereva Bodaboda wamshambulia Dereva wa Mwendokasi

Hapana nakupinga. Watu waheshimu sheria za barabara. Huwa najiuliza traffic hawaruhusiwi kuwakamata watembea kwa miguu wanaovunja sheria? Watembea kwa miguu nao wanavunja sheria mno. Huko Kkoo watu hawayaogopi magari kabisa.
Watanzania wengi huwa wanaamini kua sheria za barabarani zinawahusu wenye magari tu,wao watembea kwa miguu,bajaji na bodaboda huwa haziwahusu ndiyo maana wanajiendea tu bila mpango!!
 
Pisi moja hivi black.. nilimtongoza akanichomolea..
Sababu anasema wanaume wengi abiria wanamtaka.
 
Nilimuona na hilo gari akinunua mazagazaga kule shimoni Kariakoo, nikashangaa sana.
 
Kuna maswali ya kuuliza ya msingi...

1- Alivuka katika ZEBRA?
2- Dereva alishindwa kuokoa Maisha?

Gari za Mwendokasi, Fire, Ambulance huw hawaendeshi kwa tahadhari na ni kama wamepewa ruhusa ya kufanya ajali yoyote ile bila kuwajibishwa.

Msongamano wa watembea kwa miguu unasababishwa na Wamachinga.. inatakiwa sio kuweka barriers bali kuwatimua hao wamachinga ktk eneo la watembea kwa miguu ili kurahisisha flow ya watembea kwa miguu.

Watu wanakuw wanamawenge ktk kuvuka kutokana na changanyikeni ya pale. Matoroli.. boda, baiskeli, guta, bajaji, kirikuu..

Bado wabeba vinywaji.. na wauza accessories ndogo kama pete cheni miwani.. nao wanabeba mizigo inayokinga watembea kwa miguu.

Kuna maamuzi magumu yanatakiwa ikiwemo kutembeza bakora, Migambo hawana kazi ya kufanya wapewe rungu.
 
Pale taa zilikuwa zimeruhusu mkuu watu wapite, sasa huyu mwanamama katoka huko na mwendokasi mazima kamzoa mshikaji, amembuluza karibia mita mia kasoro mbele.
Dah! Ndio maana huwa napenda kuvuka pasipo tegemea taa. Watu wengi huwa wanapitiwa kwenye taa.

Akili ya dereva inawaza "Endesha huyu havuki" na wakati Akili ya mvukaji inawaza "Vuka huyu anasimamisha gari". Hapo ndio unakuta mtu kagongwa namna hiyo.
 
aada ya hapo wakamvamia Dereva wa Basi na kuanza kumpiga na kumuibia pochi yake. Baadaye Dereva ambaye aliongoza wenzake kushambulia basi na kumjeruhi Dereva amekamatwa na yupo Polisi.
Huyu inabidi awe mfano kwa wenzie.
 
Mkuu ungesema bodaboda, ukisema limegonga mtu unatuchanganya.
 
Tatizo ni wale machinga waliojazana pembezoni mwa barabara halafu wanajiona wana haki kuliko watembea kww miguu,, nchi ya kifala hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…