Zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa Chama cha Kikomnisti cha China (CPC) maonyesho mbalimbali yameandaliwa jiji Beijing ambayo kwa sehemu kubwa yanaonyesha mafanikio ya utawala wa chama hicho ndani ya muongo mmoja uliopita.
Maonyesho hayo yenye kauli mbiu isemayo 'Forging Ahead in the New Era' yanaonyesha mafanikio ya CPC katika kipindi cha miaka 10, yanagusa sekta zote muhimu kwa nchi, maelfu ya watu wanatembelea kujionea mambo mbalimbali.
Katika ukumbi wa taifa wa maonyesho wa Beijing yanakofanyika maonyesho hayo, kumewekwa picha za mambo mbalimbali ambayo yanatajwa kuwa ni mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi hicho, watembeleaji hupata maelezo na kujibiwa maswali yao.
Miongoni mwa vitu vilivyovutia wengi ni maendeleo ya teknolojia katika zana za ulinzi, na ubunifu unaotoa masuluhisho kwa changamoto mbalimbali ambazo awali zilikuwa zikiikabili jamii.