Benki Kuu Tanzania: Mlioficha Dola zirudisheni kwenye mzunguko

Benki Kuu Tanzania: Mlioficha Dola zirudisheni kwenye mzunguko

Hivi watu wa kitengo hawawezi kutoa taarifa nyeti kuhusu wahusika wakuu wenye kuhusika kuficha fedha za kigeni hasa dola za Kimarekani?

Yaani kweli BoT imefikia hatua ya kuishia kulalamika kuhusu upungufu uliopo katika mzunguko wa fedha za kigeni hapa nchini na kisha kuwapigia magoti wahujumu uchumi?

Taassi nyeti zinapaswa kuwachukulia hatua wahusika kwa kuwa wanafahamika, kama vile ambavyo alithubutu JPM kufanya. Ukiona serikali imeuchuna, huku taasisi yake nyeti ya fedha, BOT inalalamika, basi tambua inawagwaya wafanyabiashara na matajiri wakubwa, na hata inashindwa kuwachukulia hatua ijapokuwa inawatambua.

"Toothless bulldog"
Usiturudishe kwenye ule UHAYAWANI wa
MAGUFULI. Kunya g'anya fedha za mtu aliyezitolea jasho lake siyo uungwana. Ndiyo maana JITU lile lilikufa tarrhe 17/ 03/21.
 
Ni muda Afrika kuwa na currency yake ili tuepukane na Dola domination.
Ewe mwafrika ukumbuke una marejesho ya dola sababu ya mikopo ya riba na isiyo na riba uliyokopeshwa kwa dola, unaihitaji sana dola usijisahaulishe.
 
View attachment 2761849
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amewataka watu walioficha Dola kwa malengo ya kusubiri zipande thamani na kujipatia Faida zaidi kubwa, waziachie kwenye mzunguko wa Biashara, ili kuondoa uhaba wa Fedha hiyo Nchini.

Kauli ya BoT inakuja ikiwa ni wiki chache tangu Mkurugenzi Utafiti na Sera wa Benki hiyo, Suleiman Misango, aseme upungufu uliopo sasa wa Fedha za kigeni ni himilivu kwakuwa akiba ipo ya kutosha.

Hii kauli hii ya Benki Kuu inakupa tafsiri gani?
Anazungumza akiwa kwenye V8, full AC, dereva na uhakika wa posho kila kikao/safari. Watoto wanasoma Australia
 
Watu waluoko ccm ni mzigo wa misumari na haubebeki

uongozi wa awamu hii umefeli kuliko awamu zote

Sijawahi kushuhudia cadi za ccm zikirudishwa kwa wingi na kila sehemu tena mbele ya ma DC
Ona huyu, anaambiwa dola yeye anasema kadi za ccm,
Tukiwaambia ccm itatawala miaka elf mbili mnapinga
Bwashee sio kila mahali ni siasa, kuwa siriasi wakati mwingine
 
View attachment 2761849
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amewataka watu walioficha Dola kwa malengo ya kusubiri zipande thamani na kujipatia Faida zaidi kubwa, waziachie kwenye mzunguko wa Biashara, ili kuondoa uhaba wa Fedha hiyo Nchini.

Kauli ya BoT inakuja ikiwa ni wiki chache tangu Mkurugenzi Utafiti na Sera wa Benki hiyo, Suleiman Misango, aseme upungufu uliopo sasa wa Fedha za kigeni ni himilivu kwakuwa akiba ipo ya kutosha.

Hii kauli hii ya Benki Kuu inakupa tafsiri gani?
Hii sasa tunaacha kufikiri kisomi, ina maana kenya nao wameficha dollar ?
 
Ni muda Afrika kuwa na currency yake ili tuepukane na Dola domination.
Africa mashariki yenyewe tumeshindwa kuwa na sarafu ya pamoja, ndio itakuwa Africa? Huku afrika viongozi wanawaza wizi wa kura tu.
 
Dola ziko kwa wavaa kobazi huko zimepelekwa mpk wanagaiana ili wanunue misosi.
 
Back
Top Bottom