Mheshimiwa Rais na wataalamu wengine wa masuala ya uchumi, kwa niaba ya Watanzania wote tusio elewa nini maana ya nchi kuwa katika UCHUMI WA KATI tunaomba mtufafanulie ili wote twende sawa.
Leo tumeona mheshimiwa akipongeza kuhusu nchi yetu kuingia kwenye UCHUMI WA KATI ila kwa bahati mbaya watanzania tulio wengi hatujui hili linamaana gani.
Hivyo tunaomba ufafanuzi kidogo wa hicho kinacho itwa uchumi wa kati ndio nini na kinafanya nchi yetu kulingana na nchi zipi za mabeberu kiuchumi?
Ni ngumu kumwambia tu mwanachi wa kawaida huko chini kuwa nchi yetu ipo katika UCHUMI WA KATI wakati huo kila kukicha anaona bora ya jana. Pesa mtaani hakuna, maisha magumu, ajira kwa vijana hakuna hata za huko serikalini hazitoki na mambo mengine kama hayo.
Tunaomba ufafanuzi kidogo ili na sisi tuweze kuwaeleza wananchi kuhusu hilo pindi wanapo tuuliza huku mtaani.
Yote kwa yote hongera Tanzania kwa kufikia UCHUMI WA KATI.
View attachment 1494732
Mods msiunganishe huu uzi