Salaam Wakuu,
Leo Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Bernard Membe anaongea na Wahariri wa Vyombo vya habari Jijini Dar.
Nipo hapa City Lodge Mjini kati kusikiliza kile atakachoongea niwajuze.
Taarifa zote zitapatikana kwenye hii thread.
Stay tuned.
=====
UPDATES: 1048HRS
Wanahabari Washafika eneo la tukio
UPDATES: 1100HRS
View attachment 1604746View attachment 1604747View attachment 1604748
MEMBE ANASEMA:
Nimewaitta kupitia ninyi niongee na Watanzania.
Wengi wameuliza Membe yupo wapi? Au kaunga mkono Juhudi, au kaondoka chama?
Mimi Membe ni Mgombea Halali wa ACT Wazalendo. Ni chama chetu kizuri na nitakipeleka kwenye Uchaguzi wa Mwaka huu kama Mgombea wa Urais.
Kuna watu walikuwa wanasubiri nitamke tu neno ila mambo yatimie.
Mimi hupenda kujibu Maswali.
Hapa nimekuja na Omary Faki Mgombea Mwezi kutoka zanzibar na Meneja Kampeni wa Urais wa ACT.
Ipo nadharia kwamba Vyama vikiungana vinaweza kushinda. Lakini katika bala la Africa, nadhalia hii haijawahi kufanikiwa.
Madikiteta wote wameangushwa na vyama binafsi. Afrika chama kimoja ndo huwa kinashinda sio vilivyoungana.
Vyama 19 bara la afrika vya Ukombozi, vyama 13 vimeshaondoka. Vimeondolewa baada ya vyama vyenyewe kujitafuna na kuwa na mpasuko na vyama vya upinzani vikachukua advantage.
Ili chama Tawala kife, kinatakiwa kipasuke kwanza.
Nadharia ya chama Tawala kupasuka, imeshakomaa Tanzania.
Chama Tawala cha CCM tunakiangusha Mwaka huu kama tutafanya haya nitakayo yasema.
Nini maana ya kupasuka kwa chama. Ni hadi wanachama waseme tumechoka. Angalieni wakati wa kura za maoni za CCM,watu walienguliwa. Sisi ACT tulipokea Applications 42 za kuomba kujiunga na sisi. Sijui walioenda vyama vingine.
Baada ya kura za maoni Bashiru akaanza kuwaahidi kwamba watapewa vyeo watatumbuliwa.
Mimi nlikuwa na wabunge 78 wa CCM, 46 Wamefyekwa na 23 bado wamo CCM. Siwapi majina
Mimi nlijipanga na wenzangu sita ili kushindana na Magufuli, mimi nlikuwa tayari kumkabiri kwenye Uchaguzi na bahati yao walinifukuza.
Hata chama Tawala mambo yanapoharibika wanakimbia. Lazima wapewe sehemu ya kutokea. Anaweza akachagua chama cha kujiunga.
Tunachotaka sisi ni kukipasua chama cha CCM na kimeshapasuka. Sasa aje mtu mwenye nguvu aingie madarakani.
KUSUDIO LANGU
Ndugu zangu watanzania, tumepata tabu sana. Tumepiga kwelikweli. Sasa hivi Tanzania ni Fukara, Watanzania hawana fedha. Dunia haiishi hivi. Dunia ina fedha. Sisi tumerudi miaka ya 80. Serikali haitumii fedha sababu haina kwasababu imekopa sana.
Dunia nzima Serikali ndo tajiri wa kwanza na kuzisambaza. Ukiona nchi haina fedha wa kuajibishwa ni serikali. Serikali ndo mwajiri Mkuu.
Mtu mmoja anasema sasa kama mimi nina fedha kwaninii nikope?
Kopa ulipe kidogo kidogo. Ukienda kununu vitu kwa fedha yako ili uonekane una hela jua unafukarisha Serikali yetu.
Rais aje awe Mimi au Tundu, kazi kubwa itakuwa ni kulipa Madeni. Na mashitaka yote tutakayodaiwa itabidi tulipe.
Tusidanganyane, Serikali hii haona fedha. Tuna ufukara. Na ufukara huu ndo unaofanya watu wakati wa Uchaguzi, Ukichanganya ufukara huu na hasira wakati wa Uchaguzi ndo unawasha moto.
Mimi nmesimamia uchaguzi 19.
Ukichanganya hasira ya kunyimwa haki ukajumlisha na Ufukara walionao ni fujo. Na haya mazingira tumeyatengeneza.
Kwani hatuna njaa? Siku hizi chakula chetu ni mihogo na madafu.
Pale kariakoo unakuta asubuhi anakunywa kahawa, mchana hadi jioni.
Watu wanakula mihogo mibichi na iliyoiva. Wanasisinzia hovyo hovyo
Jana saa nne usiku nimetembelea hotel za dar. Zote ni kiza, hakuna watu.
Jana nmeenda kariakoo nikiwa nmevaa kanzu. Zamani tulikuwa tunaingiza 90 bilioni kwa wiki. Nenda sasa hivi, inatisha. Fremu nyingi sana zimefungwa.
Mtu anasema ukiingia kariakoo na vazi la CCM hawakufanyi kitu kama zamani.
Hawafanyi hivyo sababu wanakuoenda bali ni uoga. Watu hawapo huru.
Uchaguzi huu tuwe na haki. Waangalizi kutoka nje watakuwa wachache. Wale wakubwa wakubwa hawaji. Hawaji sababu wanajua bado kuna COVID-19. Pia UNDP haijatoa fedha sababu Serikali ilikataa fedha za uchaguzi na kwanini walikataa? Muwaulize nyinyi.
Ila wanatakataa sababu ukipokea fedha za UNDP shariti namba moja ni lazima walete international observers. Hawa waliokuja ni Mabalozi na Wafanyabiashara.
Tutakuwa na observers.