Sumatra wamesimamisha kutowa leseni kwa magari ya mtu mmoja mmoja au mwenye basi moja, leseni zinatolewa kwa kampuni au ushirika mwenye mabasi yasiyopungua 100.
Ruti za nje ya jiji wanatoa leseni, kwa mfano, kutoka Mwenge kwenda Bunju na Bagamoyo nk. Kutoka Ubungo kwenda Kibaha, Mlandizi, Chalinze nk. Kutoka Buguruni kwenda Chanika, Masaki, Vikumburu, Kisarawe nk. Kutoka Mbagala kwenda Ikwiriri, Mhoro nk.
Magari mengi yaliyokuwa na ruti za Mwenge to Posta na Kariakoo wamehamia ruti ya Mwenge Bunju na Bagamoyo, sasa hivi kupata basi la kwenda mjini kutokea Mwenge shughuli yake ni kubwa. Kuna tetesi kuwa Azam ameagiza mabasi ya daladala 300.