Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Zingatia ushauri wa bu'yaka.Ila kama bado utaitaji kufanya hiyo biashara usiwe msimamizi tafuta mtu mzoefu ya hiyo biashara akuunganishe na wale vishoka wa stand ambao unasaini nae mkataba unamkabidhi gari kwa mapatano ya wewe unataka sh ngapi mfano laki 7 kwa mwenzi ikifika mwisho wa mwezi ndio mnaonana na makataba useme njia ni zipi na je gari likionekana nje ya hizo route iweje.Ila ukubali kuchakachuliwa.Miji mingi wapo watu wanaendesha maisha kwa dili hizo anakuwa na gari za mpaka watu kumi.kila gari akiiba hapo elfu 10 mara kumi mara mwezi.
 
Hivi nikipata toyota supr roof (dungu)nzuri..manual disel...na kufanya daladala yawezakuwa biz nzuri ????advise
 
Hivi nikipata toyota supr roof (dungu)nzuri..manual disel...na kufanya daladala yawezakuwa biz nzuri ????advise

ni poa ila kama upo dsm maeneo mengi dala dala zitapigwa marufuku ili kupisha BRT. Hiyo mtabanana maeneo yasio kuwa na huo mtandao. Nimejijazia hili mwenyewe kwa kutumia logic, usije ukaninukuu.
 
Habari zenu wana jamii wote.

Nilikuwa nataka kununua minibus kwa ajili ya kuanzisha biashara ya daladala. naomba kujuwa ni aina gani ya minibus ndio bora zaidi na zinazoweza kustahamili harakati za barabara za bongo na pia upatikanaji wa spare parts zake. Kadhalika kama kuna yeyote ambae amewahi kuwatumia serenget freight forwarder (wazee wa kazi) wa hapa uk naomba review zenu juu ya huduma zao kwa ujumla.

ahsanteni
 
Hii biashara ni pasua kichwa kwa kweli...kwanza sumatra hawatoi tena leseni...mi nnalo langu nimelipaki tu bongo
kuhusu serengeti mi nimeshafanya nao biashara....bwana lukosi yupo poa Kwenye biashara yake(napingana nae Kwenye masuala ya chama tu)....meli ikiondoka tu baada ya week wanakutumia invoice then unalipa kisha wanakupa bill of lading yako
 
kaka niPM nikupe wazo zuri kama una nia ya kununua minibus

ntakupa contacts za dealer mzuri
 
kaka niPM nikupe wazo zuri kama una nia ya kununua minibus

ntakupa contacts za dealer mzuri

Mkuu, sasa yeye ata kuPM nini tena? Kama unaona kuna la zaidi la kumjulisha ungem PM wewe ili kurahisisha mambo.
 
Vipi kuhusu zile Eicher bus? Bei yake ikoje, naona kama zinawezana sana na barabra za bongo. Summatra wakisitisha kutoa leseni itakuwaje?
 
Sumatra wamesimamisha kutowa leseni kwa magari ya mtu mmoja mmoja au mwenye basi moja, leseni zinatolewa kwa kampuni au ushirika mwenye mabasi yasiyopungua 100.

Ruti za nje ya jiji wanatoa leseni, kwa mfano, kutoka Mwenge kwenda Bunju na Bagamoyo nk. Kutoka Ubungo kwenda Kibaha, Mlandizi, Chalinze nk. Kutoka Buguruni kwenda Chanika, Masaki, Vikumburu, Kisarawe nk. Kutoka Mbagala kwenda Ikwiriri, Mhoro nk.

Magari mengi yaliyokuwa na ruti za Mwenge to Posta na Kariakoo wamehamia ruti ya Mwenge Bunju na Bagamoyo, sasa hivi kupata basi la kwenda mjini kutokea Mwenge shughuli yake ni kubwa. Kuna tetesi kuwa Azam ameagiza mabasi ya daladala 300.
 
Habari zebu waheshimiwa. Nimepata mtaji kidogo na ninataka kuwekeza katika daladala hapa jijini Dar es salaam, ninapendelea kuwekeza katika magari mojawapo tajwa hapo juu. Naomba kujua kwa wanaoyafahamu kwa undani lipi bora na kwa sababu zipi. Nawakilisha
 
Tata ndio mwisho wa matatizo kwa uimara wake-ila bei yake imesimama kweli kweli...70mil (uhakika miaka 7 -10)linganisha na Eiches ni 45m-50m...kazi kwako
 
Habari zebu waheshimiwa. Nimepata mtaji kidogo na ninataka kuwekeza katika daladala hapa jijini Dar es salaam, ninapendelea kuwekeza katika magari mojawapo tajwa hapo juu. Naomba kujua kwa wanaoyafahamu kwa undani lipi bora na kwa sababu zipi. Nawakilisha

Mkuu tunaweza kuwasiliana ? ili kubadilishana mawazo/Idea mm nina uzoefu kidogo na Eicher nimezitumia na ninawazo kama lako pia nadhani tofaut ya bei sio kubwa sana TATA 77mln Eicher 68 mln sina uhakika kwa sasa
 
TATA kampuni ya siku nyingi kweli wana hadi saloon car
 
Mkuu mtafute jamaa m1 anaitwa Kisena ana Marcopolo Tata na pia mtafute king Ay mpole ana Eicher watakusaidia kukupa uzoefu.
 
Mleta uzi unawazo zuri sn na Tata is the best, pia kwa ushauri wangu sioni km kwa dar zitakulipa zaid ya gari kuchoka tu, kuna njia ambzo unaweza enda fanya iyo kazi ikakulipa mpaka ukashangaa, ila inahitaji uamuzi wa kwenda kuishi nje ya dar. Njia km Mbeya-Mjombe-Songea inalipa, Njombe-Iringa mjini ni pesa tupu nk. Life si bongo tu!
 
Salamu wanaJamvi.Kuna haya mabasi ya Abiria 40 aina ya Heischer (samahani kama nimekosea Spelling zake!) na mengine yanayofanana nayo ya Tata Marcopolo ambayo sasa hivi yameshika chati sana kwenye usafirishaji wa abiria hapa jijini na hata miji inayopakana na Dar kama vile Handeni, Lushoto, Mor na kadhalika.

Ninaomba kuuliza kwa mwenye uzoefu nayo, Bei yake ni Kiasi gani? Uimara wake Ukoje? 'Unywaji' wake wa mafuta uko vipi? Yanaunganishwa hapa hapa ama yanakuja mazima kupitia kwa Agent? Ni Agenti gani huyo?
Ni Agent gani huyo?
Shukurani zimetangulia kwa Michango yenu..

 
Hayo yanapatikana pale africarriers na pale next to CMC automobile opposite na Holiday Inn Azikiwe Street.

Unywaji wa mafuta unategemea na size ya engine ndugu. sema hizi gari mara nyingi zinaingia zikiwa mpya (sio 2nd hand) so mwanzoni zitakuwa hazinywi sana mafuta na hazisumbui sana. But they are not durable especially for severe duty.
 
Back
Top Bottom