Uchaguzi 2020 Biharamulo - Rusahunga Dkt. Magufuli aikacha Ngara, aelekea Kigoma

Uchaguzi 2020 Biharamulo - Rusahunga Dkt. Magufuli aikacha Ngara, aelekea Kigoma

Yani wasafiri wanataka kuwahi kufanya shughuli zao za kuwapatia kipato wanawekwa pembeni kupisha msafara wa dikteta uchwala mmoja masaa zaidi ya matatu???
HATUMTAKI HUYU MTU!

Nilizisikia laana toka kwa wasafiri waliokuwa wamepigwa pini kusubiri msafara ipite huko utakakopita.

Jiwe mwaka huu mbona kazi anayo?

Wale wasafiri pia wana ndugu zao achilia mbali wapendwa wao. Kampeni nyumba kwa nyumba. Tamu hiyo? Mbona haihitaji TBC 1 na matangazo ya kukata kata.

CDM panatakikana mkakati thabiti wa kuzilinda kura.
 
Mkoje lakini? Nani kawambieni Dr.Magufuli analazimika kufanya kampein kwenye Wilaya zote za Mikoa anayo tembelea? Mbona hamlalamiki kwamba hakwenda Wilaya ya Karagwe why pick on Ngara!!

Mnapenda penda sana kukuza kuza mambo madogo madogo kwa kuwa hamna any substance to talk about mnapokuwa kwenye kampein za vyama vyenu - chukulia mfano was Lisu wa kusema eti reli ya TAZARA hipo kwenye kundi la SRG!! Nani anaweza kuchukulia kauli zenu seriously - NANI?
 
Atakuwa ndo hataki tena mambo ya Bukoba baada ya kukataliwa ila Kigoma ndio watamuonesha mbaya zaidi.
Na kweli kigoma wamemuonyesha "mbaya kweli" mpaka anataka kurudi huko tena, tena amewahahidi Salala huko kabisa, jinsi Kigoma inavyo waka.
Yaani jamaa wa saccos akienda huko akachukua "kula" kiurahisi kabisa pamoja na Ngara ,kwabi sera au ilani ya saccos inasemaje juu ya Barabara za huko .
 
Nenda uelekeo wa Ngara to Rwanda and Burundi, kuna poda nyekundu barabarani yaani inshort lami iliondoka miaka mingi gari zinaoga vumbi na kukwama kwenye vumbi.
Tatizo lako ni kufikiria Magufuli atatatua kero zote za maji, umeme, barabara, elimu, na nyinginezo kwa mara moja. Unaposema kuna barabara mbovu huko. kuna bado barabara mbovu nyingi sana. Cha muhimu ni nia ya kuzijenga na lini. Lakini hilo jibu linategemea na kodi zinazokusanywa, kwa hiyo usitudanganye kuwa kutojengwa hiyo barabara moja kati ya nyingi na matakwa ya raisi. Hapana. Ujenzi huo unategemea pesa tunayokusanya kutatua matatizo elfu kidogo.
 
Nilizisikia laana toka kwa wasafiri waliokuwa wamepigwa pini kusubiri msafara ipite huko utakakopita.

Jiwe mwaka huu mbona kazi anayo?

Wale wasafiri pia wana ndugu zao achilia mbali wapendwa wao. Kampeni nyumba kwa nyumba. Tamu hiyo? Mbona haihitaji TBC 1 na matangazo ya kukata kata.

CDM panatakikana mkakati thabiti wa kuzilinda kura.
Hicho kipande cha vumbi ni km 112 au zaidi ??
 
Mkoje lakini? Nani kawambieni Dr.Magufuli analazimika kufanya kampein kwenye Wilaya zote za Mikoa anayo tembelea? Mbona hamlalamiki kwamba hakwenda Wilaya ya Karagwe why pick on Ngara!!

Mnapenda penda sana kukuza kuza mambo madogo madogo kwa kuwa hamna any substance to talk about mnapokuwa kwenye kampein za vyama vyenu - chukulia mfano was Lisu wa kusema eti reli ya TAZARA hipo kwenye kundi la SRG!! Nani anaweza kuchukulia kauli zenu seriously - NANI?

Mahaba mengi mwishowe upofu. Umeshindwa kuona kwa nini kuja Ngara ilikuwa muhimu zaidi?

"Baada ya kufuatilia kampeni za jiwe na kutambua kuwa baada ya Bukoba alielekea Biharamulo, ilitegemewa asingeacha kwenda Ngara ili pia aione barabara ile pendwa ya Rusahunga - Rusumo."

Ramani kwenu bila shaka ni mapambo. Asingeweza kufika Karagwe bila kufika Ngara kwanza akiwa rusahunga kutokea Biharamulo.

Umeshindwa kujiongeza pia kujua kuwa hata huko karagwe nako ni "maji ga nyanja!" Kama kulivyo Ngara karagwe hakuna miundo mbinu ya kumwimbisha mapambio yoyote ya ya mafanikio tuliyozoea kuimbishwa!

Sina hakika pia kama hata ramani niliyoweka uliweza kuiona kuhalalisha kusimamishwa shughuli za wengine 30km kutokea atakakopita mwomba kura za watu huyu.

Inawahusu nini waliowekwa 3 hours + kumsubiria yeye aamke atakapojisikia ili atumie barabara lote peke yake kwa raha zake?

Adha inayo wasibu wengine kwenye mipangilio hii si kitu sana kwako kwa sababu haikukufika wewe? Huu si utakuwa ndiyo ule binafsi uliopitiliza?

Rais ajaye na aliangalie hili. Tunamini hata kwa kutumia Chopa ingekuwa ni nafuu mno kwenu na kwetu pia tusiokuwa na cha kufanya na state he zenu.
 
Na kweli kigoma wamemuonyesha "mbaya kweli" mpaka anataka kurudi huko tena, tena amewahahidi Salala huko kabisa, jinsi Kigoma inavyo waka.
Yaani jamaa wa saccos akienda huko akachukua "kula" kiurahisi kabisa pamoja na Ngara ,kwabi sera au ilani ya saccos inasemaje juu ya Barabara za huko .

Usipende kulishwa matango pori na maafisa vipenywa wa TBC moja.

Nenda kajionee mwenyewe.

Nisingemvutia kasi mzee baba ningeujua u mbayuwayu wake au adha za nyantakara anapokuwa kwenye kampeni zake?

Sina hakika katika ile halaiki niliyoiona nyantakara kama atapata kura hata moja kwao. Watu wale walichoka hasa.

Kumbuka pia huu ulikuwa upande mmoja tu Nyantakara kuelekea Nyakanazi. Bado kuna Kakonko - Nyakanazi, Biharamulo - Nyakanazi na Muzani - Nyakanazi.

Subiria ya Ryoba kuaminishwa kuwa hata Bukoba hakukuwa na zomea zomea.
 
Hicho kipande cha vumbi ni km 112 au zaidi ??

Kwani hata ni vumbi tu? Unaoshuhudiwa Tanzania hii hii au ni wale ambao Tanzania ni Dar?

Unaweweseka sana mkuu. Yaonesha ulidhani flyover zimejengwa nchi nzima.

112km ambazo umuhimu wake ni kupendezesha jiji ambazo ujenzi wake labda umeshaanza hizo ni Dodoma. Hali ya rusahunga - rusumo haina dharura wala umuhimu kwa jiwe.

Rusahunga Rusumo ni 92km tu. Hii ni barabara kuu yenye umuhimu wake kwa bandari ya Dar. Barabara hii kutokukuhusu wewe kiuchumi kama mtanzania kwa kuwa tu kwenu ni Ruangwa, Makongorosi, Ukara au kokote kule nchini, ni umbumbu uliopitiliza.

Barabara hii iko hali hohehahe kwa miaka nenda rudi. Nyuzi hizi ni baadhi ya zina zoihusu barabara hii:

Hali ya mbaya mno ya barabara Nyakanazi Rusumo vipaumbele vyetu ni nini?

Barabara ya Rusahunga - Rusumo ifungeni tu ieleweke

Rusumo - Rusahunga njia kuu kwenda Dar taswira halisi ya awamu ya tano - ukweli mchungu

Ziara ya Kagera, Magufuli usiende pekee tu Wasaidizi wako wanakokupangia kwenda

Wewe ndiyo kuisikia leo?

Zipo nyuzi nyingi zaidi. Sema kama huwezi ku search tuendelee kuzifukua.
 
Ramani umeiona? Pia kumeelezwa:

"Lusahunga - Muzani ni kuelekea rusumo. Nyakanazi - kakonko ni kuelekea Kigoma. Nyakanazi - Biharamulo ni 50km."

Yote ni mahaba tu? Ama kweli mapenzi upofu!

Amekula right. Hadi kufunga safari kuja huku safari binafsi unadhani ni lelemama?

Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea

Picha ni nyantakara kuliko X kwenye ramani. Magari yalikopigwa stop.

Barabara inayopigiwa kelele unakula right ukitokea Biharamulo ili uelekee rusumo.

Pia kupo hivi:

Ukarabati kichekesho Rusahunga - Rusumo
Hatutaki maendeleo ya vitu sisi watu hawali barabara sindio sera zenu hizo tena kumbe munataka lami ya nini?
 
Hatutaki maendeleo ya vitu sisi watu hawali barabara sindio sera zenu hizo tena kumbe munataka lami ya nini?

Hayupo mwenye sera hizo. Mnachotaka hapo ni kujichekesha kwa kujitekenya wenyewe.

Labda kama ndiyo zilizo sera zenu. Kwa maana serikali madarakani ni yenu na barabara hii ipo katika hali kamili ya utekelezaji wa sera zenu:

Ziara ya Kagera, Magufuli usiende pekee tu Wasaidizi wako wanakokupangia kwenda

Pamoja na yote haya aliziba masikio?

Oct. 28 atavuna alicho panda.
 
Baada ya kufuatilia kampeni za jiwe na kutambua kuwa baada ya Bukoba alielekea Biharamulo, ilitegemewa asingeacha kwenda Ngara ili pia aione barabara ile pendwa ya Rusahunga - Rusumo.
Atakwenda Tundu Lissu
Rais anakwenda na ratiba,hii ni kampeni sio ziara ya kiserekali,muda ukiwepo tutarudi muhimu ni utekelezaji wa ilani
 
Back
Top Bottom