Bila Freeman Mbowe na Jordan Rugimbana, Tundu Lissu angepoteza uhai siku ile aliyopigwa risasi Dodoma

Wale walenga shabaha(snipper )baada ya kushindwa kumuua Tundu Lissu ,alipelekwa hospitali ya General kwa matibabu.

Lengo lilikuwa apelekwe Muhimbili.

Mbowe mtoto wa mjini akahisi hapa kuna mchezo mchafu unaweza kuchezwa,akampigia rafiki yake Captain Minje wakakodi ndege chapchap wakamtorosha mgonjwa mpaka Nairobi then ulaya,ilikuwa kama movie ya chuck Noris vile.

Mkuu wa mkoa Jordan Rugimbana akapigiwa simu toka juu kuwa imekuwakuwaje anga la Dodoma alikufungwa mpaka mgonjwa anatoroswa kibabe kama sinema.

Haikuchukua muda akatumbuliwa,npaka leo yupo kijijini kwake Chamazi kwenye kambi ya vijana wa kikristo,i UVIKIUTA anafuga kuku.

Hawakuishia hapo mradi wake wa makumbusho ya wanyambo kule kijijini kwake Nyakahanga, Karagwe ukapigwa stop,ulikuwa ni mradi wa mabilioni toka kwa wafadhili.

Rugimbana kule mbinguni kuna kiwanja chake,mtu mwema kabisa,baba yake alikuwa kamishna wa kwanza wa magereza nchini,alikufa zamani sana enzi za Nyerere na kuwaacha wakiwa wadogo,Nyerere aliwachukua na kuishi nao kama watoto wake.

Barikiwa sana Jordan Rugimbana na Freeman Mbowe kwa msaada wa Mungu Tundu Lissu bado yupo akitema madini
Aiseeeeee JIWE alikuwa katili sana.
 
Umemsahau Mzanzibar mh Turkey
 
Lisu alieleza vizuri kwamba kama Siyo Juhudi za" Dada " ( Msaidizi wake wa nyumbani) basi asingepona

Beki 3 ndiye aliwasha Gari na kumuwahisha Lisu hospital kabla hajapoteza Damu nyingi
Umetazama picha umeme ukakatika kabla move haijamalizika.
 
Hakukuwa na mlenga shabaha pale,mlenga shabaha apige risasi zaidi ya 20 bado awe mlenga shabaha?

Wale ni wahuni tu kama wale waliotaka kumteka bwashee wa watu huko Kiluvya,ila mengine yote umeandika sahihi.
Kwani risasi hazikumpata !.
 
Utawala uliopita ulikuwa wa kikatili mno. Nampongeza sana Mbowe kwa utu wake. Sisi wanaCCM hatutakaa tusahau wema wa Mbowe kwa Lissu ingawa Lissu ameshakengeuka na kusahau kila kitu.
Lissu ni mtu mwenye papara sana hana subra kabisa.

Hii si sifa njema hata kidogo,nadhani anashindwa kuelewa namna njema ya kupambana.

Mara kadhaa nimemsikia akikinanga chama chake badala ya kuishambulia CCM.
 
Wale walenga shabaha(snipper )baada ya kushindwa kumuua Tundu Lissu ,
Wale hawakuwa snipers, snipers ni trained, watu wenye shabaha waliofunzwa kulenga na kwa kawaida hutumia bunduki za risasi moja tuu, na huwa hawakosi shabaha.

Ndio maana hata Samia, alisema wazi, wale sio wa kwetu, wa kwetu wakikosa mbili, unaandika maelezo.

Wale ni watu tuu wasiojulikana, usiwape sifa za kuwa ma snipers ukatuchafulia jina safi la ma snipers wetu wanaofanya a clean job!. Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

P
 
Makamu ña Balozi walivyomtembelea TAL hospital walimkabidhi mwenyekiti bahasha iliyoletwa na Serikali

Mchungaji anasema bahasha ile hadi Leo haijulikani ilipotelea Wapi

Nabii Kesho kwenye Press yake nadhani atalizungumzia 😂😂
Nakuwekea hapa link ukasome uache uvivu.

ile shooting style ya Mateja ya keko kabisa, Sniper hawezi piga risasi Kama mganga anabishana na majini.
 
Wale hawakuwa snipers, snipers ni watu wenye shabaha waliofunzwa kulenga na hutumia risasi moja tuu, na huwa hawakosi shabaha.

Ndio maana hata Samia, alisema wazi, wale sio wa kwetu, wa kwetu wakikosa mbili, unaandika maelezo.

Wale ni watu wasiojulikana
P
Mimi huwa nasena ni Mungu hakuruhusu,maana zilimpata sema hazikulenga sehemu muhimu,siku yake ingekuwa imefika hata asiyejua kushoot angemuua tu
 
Wale walenga shabaha(snipper )baada ya kushindwa kumuua Tundu Lissu ,alipelekwa hospitali ya General kwa matibabu.

Lengo lilikuwa apelekwe Muhimbili.

Mbowe mtoto wa mjini akahisi hapa kuna mchezo mchafu unaweza kuchezwa,akampigia rafiki yake Captain Minje wakakodi ndege chapchap wakamtorosha mgonjwa mpaka Nairobi then ulaya,ilikuwa kama movie ya chuck Noris vile.

Mkuu wa mkoa Jordan Rugimbana akapigiwa simu toka juu kuwa imekuwakuwaje anga la Dodoma alikufungwa mpaka mgonjwa anatoroswa kibabe kama sinema.

Haikuchukua muda akatumbuliwa,npaka leo yupo kijijini kwake Chamazi kwenye kambi ya vijana wa kikristo,i UVIKIUTA anafuga kuku.

Hawakuishia hapo mradi wake wa makumbusho ya wanyambo kule kijijini kwake Nyakahanga, Karagwe ukapigwa stop,ulikuwa ni mradi wa mabilioni toka kwa wafadhili.

Rugimbana kule mbinguni kuna kiwanja chake,mtu mwema kabisa,baba yake alikuwa kamishna wa kwanza wa magereza nchini,alikufa zamani sana enzi za Nyerere na kuwaacha wakiwa wadogo,Nyerere aliwachukua na kuishi nao kama watoto wake.

Barikiwa sana Jordan Rugimbana na Freeman Mbowe kwa msaada wa Mungu Tundu Lissu bado yupo akitema madini

Barikiwa sana mh mbunge Turkey kwa kuleta ndege chapchap japo wewe ni CCM uliangalia ubinadamu zaidi
Duuh duniani kuna mambo!
 
Back
Top Bottom