Bila kuleta udini na uhafidhina, kati ya Israel na Palestina nani aliyevamia eneo la mwingine?

Bila kuleta udini na uhafidhina, kati ya Israel na Palestina nani aliyevamia eneo la mwingine?

Israel alivamia eneo la mwenzake , na Israel imeundwa mwaka 1948 , wakati Palestina ilikuepo muda mrefu sana

Ilivamia au ikipewa eneo. Waarabu wakamind wakamvamia eneo la Israel ndipo wakapigwa na kusogezwa
 
Ilivamia au ikipewa eneo. Waarabu wakamind wakamvamia eneo la Israel ndipo wakapigwa na kusogezwa
Mwaka 1917 Waziri wa mambo ya nje Uingereza Arthur James Balfour anamuandikia barua Rothschild (Tajiri mmiliki wa Mabank huko UK) kuwa Uingereza ina dhamira ya kuanzisha makazi ya kudumu ya wayahudi huko Palestina.

Ikumbukwe kuwa Uingereza inaandika barua hii kipindi kifupi mara baada ya kufanikiwa kumshinda Ottoman Empire Empire ambae akiikalia Mashariki ya kati. Ata hivo hii ilikuwa sehemu ya 3 kwa ao wayahudi kupewa baada ya kukataa sehemu 2 yaani Uganda na Argentina.

Naamini ata Vita ya kwanza ya Dunia mfadhili mkuu alikuwa myahudi na lengo likiwa pale mashariki ya kati.

Ukisema walipewa itabidi ujiulize walipewa na nani? Wapalestina wenyewe?
 
Wote wavamizi tu, maana original palestinians walishakua sucked na makabila mengine tokea uvamizi wa Persians na babylonia
Sasa basi hayupo mwenye haki ya kumfukuza mwenzake wote waishi pamoja kama united states lenye kuzingatia usawa. Mbona Australia, USA wale wote ni wavamizi lakini hakuna migogoro ya ardhi iweje hapo.
 
Sasa basi hayupo mwenye haki ya kumfukuza mwenzake wote waishi pamoja kama united states lenye kuzingatia usawa. Mbona Australia, USA wale wote ni wavamizi lakini hakuna migogoro ya ardhi iweje hapo.
Mwaka 1948 May UN ilimteua Bernadotte kuwa msuluhishi wa uo mgogoro! Bern alitoa mapendekezo yafuatayo

1. Kurekebisha mipaka
2. Palestina ipate uhuru wake
3. Wakimbizi wa kipalestina warudi Palestina
4. Yerusalemu iwe chini ya udhibiti wa Umoja wa Mataifa ili watu wote waweze kuingia.

Sept 1948 Bern aliuawa na kikundi cha Wayahudi ambao hawakutaka kusikia kabisa juu ya mapendekezo hayo na mmona ya watu aliyekaongoza ilo genge la kumuua alikuja kuwa Waziri Mkuu wa Israel kupitia chama Likud cha Benjamin Netanyahu kwasasa.

Kwanini Israel haitaki Palestina ipate uhuru? Ili swali unalopaswa kujiuliza mpaka sasa.
 
Mungu akisema amesema. There is no going back.

"The days are coming,’ declares the Lord, ‘when I will bring my people Israel and Judah back from captivity[a] and restore them to the land I gave their ancestors to possess,’ says the Lord.”
Acha kuwa mtumwa wa maupinde
 
Mvamizi ni israel.kabla ya 1948 hapa kuwa na israeli.kwa mauaji anayoifanya Israel inaonesha kuwa Adolf Hitler alikuwa sahihi kuwaangamiza hawa wahuni
 
ngoja niiweka katika lugha Rahisi.
Africa ni jina la Eneo.hakuna wakati Africa iliwai kuwa nchi ama utaifa wa mtu.

katika hiyo Africa kumezaliwa nchi nyingi.

Palestine vile vile hakuna mahala iliwai kuwa utaifa wa mtu,kila aliyekuwa mkaazi wa ilo eneo aliitwa mpalestina.

katika hiyo hiyo Palestine, waarabu baadhi wakakata 77% ya Eneo la Palestine, wakatengeneza Nchi inayoitwa Jordan.
ila sijawai sikia wapigania uhuru fake wa Palestine wakitaka Ardhi ya Jordan ilhali nayo ni Palestine.
Unaelekea kweny ukweli ,ugomvi wa pale unaletwa na mazayuni hawa wanaotumia kitabu cha Talmud wakati huko jews wanatumia Torat , wako kizamani zaidi ni watu wapole sana , wakazi wa pale ni mchanganyiko ....Kuna tetesi kwamba Raisi ya palestina ni myahudi kiasili . iko wazi wale jamaa walikuwa wanaishi vizuri tu bila ya shida , wamefunga ndoa bila ya ubaguzi wowote .

Settler waliokuja na idea ya zionism , siasa hizi ndio zinawamaliza sana ...Pale ni tatizo la kimipaka ambapo mpaka sasa wanachulia eneo lolote mpaka jordan ni lao ...Ina maana wakimaliza hapo wanatanua ,ikumbuke kila sheria wanayoshinda wanaikalia😛😛
 
Palestine vile vile hakuna mahala iliwai kuwa utaifa wa mtu,kila aliyekuwa mkaazi wa ilo eneo aliitwa mpalestina.

katika hiyo hiyo Palestine, waarabu baadhi wakakata 77% ya Eneo la Palestine, wakatengeneza Nchi inayoitwa Jordan.
ila sijawai sikia wapigania uhuru fake wa Palestine wakitaka Ardhi ya Jordan ilhali nayo ni Palestine
Palestine ni eneo tu ambalo kale liliitwa Philistia na walikuwepo watu wanaishi hapo makabila ya kutoka ugiriki huko kama caphtorites na wacanaan wengine kama Hivites na gilgashites hao ndio wakazi halisi wa eneo la palestina.

Fast forward Wayahudi wakahamia hapo na kuanza kuchinja watu na wakateka maeneo ya Palestine. However miaka mingi baadae wakaja kuwa sucked na Roman empire, Ottoman, Persians, Babylonia empire etc ambapo zaidi ya 80% ya inhabitants wakaenda utumwani au kuwa assimilated na makabila mengine mashariki ya kati na ulaya.

Since then wakaazi wengi tu waliishi hapo ambao wote sio original palestines wala original israelites. Ila cha ajabu wayahudi wakarudishwa 1948 kwa mgongo wa UK na USA na wakahodhi hilo eneo kuwa ni lao.

Ndio sasa nasema kama issue ni originality hao israelites wa sasa au palestinians wa sasa sio wakazi halisi wa miaka 2000 iliyopita!! Sasa kwanini wayahudi wanaihodhi?

Kingine nchi au taifa linakuja baada ya taifa kujitawala. Sasa hiyo hoja ya Africa is non sense hata Tanzania au Zambia hazikuwahi kuwa nchi au taifa kabla ya uhuru wa miaka ya 1960s, hivyo hivyo palestina ingepewa uhuru 1950s basi I ingeitwa taifa la palestina. Hata hao Israel walijiita Judaeah kipindi hicho same to Kurds hawakuwahi kuwa taifa ila siku walipewa uhuru taifa lao litaitwa Kurdistan.
 
Sasa basi hayupo mwenye haki ya kumfukuza mwenzake wote waishi pamoja kama united states lenye kuzingatia usawa. Mbona Australia, USA wale wote ni wavamizi lakini hakuna migogoro ya ardhi iweje hapo.
Na ndio hiko tunaita two-state solution waishi pamoja wagawane tu maeneo ya kiutawala. Cha ajabu Israel imekua ikitanua mipaka yake kila siku na kubariki walowezi??
 
Kwanini Israel haitaki Palestina ipate uhuru? Ili swali unalopaswa kujiuliza mpaka sasa.
Kwa mujibu wa data nilizonazo inatokana na kutokukubaliana kwa malengo baina ya pande mbili.

Tafadhali nieleweshe hivi doctrine za Hamas zikoje. Je, nao wanakubaliana kutatua mgogoro kwa kuwa na taifa la Palestine na Israel pale ama hawalitambui kabisa taifa la Israle, na wana aim kuwafutilia mbali kwenye uso wa dunia? Maana hizo ndo claim za Israel wanazotumia kama haki ya kujilinda.
 
Malengo ya Hamas ni kuindoa Israel kwenye maeneo inayoyakalia kwa mabavu.

Labda kwanini huyo mwakilishi wa UN aliuawa na kundi la kiyahudi?
Na kwanini Yitzhak Rabin Waziri mkuu wa Israel alipojaribu kusuruhisha mgogoro huu naye aliuawa na Wayahudi wenyewe?
 
Japo katika kujibu swali hili kutahitaji historia, naomba tujitahidi tusilete udini bali chanzo halisi cha mgogoro huu wa Palestina na Israel.

Ninachokijua kime-base kwenye dini na ndio maana nashindwa kukiweka hapa, nawaomba wataalamu wa Historia ya Israel na Palestina watusaidie, pia mtu yoyote aliye na uelewe wa haya mambo anaombwa achangie.
waisraeli ndio wamevamia ardhi ya wapalestina
 
Malengo ya Hamas ni kuindoa Israel kwenye maeneo inayoyakalia kwa mabavu.

Labda kwanini huyo mwakilishi wa UN aliuawa na kundi la kiyahudi?
Na kwanini Yitzhak Rabin Waziri mkuu wa Israel alipojaribu kusuruhisha mgogoro huu naye aliuawa na Wayahudi wenyewe?
Mgogoro ndo unaanzia hapo,
Kumbuka Arab Palestinian sio descendant wa pale kama alivyo Myahudi. Wote wana historia na hapo ila wote ni wahamiaji.

Sasa kwanini mwingine asimtambue mwenzake na ndo maana sasa ni nguvu inatumika na mwenye nguvu ndio ana muonea mnyonge wakati wangekuwa ni waliostasrabika wangeishi wote kwa amani na kuheshimiana.

Waziri Rabin alipigwa risasi na kijana mwenye msimamo mkali na sio kundi la wayahudi na alitumikia kifungo jela. Kwenye kila jamii kuna watu wema na wabaya. Huu mgogoro ukiuangalia bila kuwa na hisia za upande utagundua kuwa hakuna upande ulio sahihi.
 
Hilo eneo lilikuwa Shamba la Jamii ya Mafala ambao walimuuzia baba wa Imani Abraham

Hilo ni Shamba alilorithi Yakobo ( Israel) kabla ya kwenda uhamishoni

Ulale Unono 😄
Huyo Abraham aliuziwa sh.ngapi hilo shamba? Mashahidi, mkataba wa mauziano viko wapi?
 
Mgogoro ndo unaanzia hapo,
Kumbuka Arab Palestinian sio descendant wa pale kama alivyo Myahudi. Wote wana historia na hapo ila wote ni wahamiaji.

Sasa kwanini mwingine asimtambue mwenzake na ndo maana sasa ni nguvu inatumika na mwenye nguvu ndio ana muonea mnyonge wakati wangekuwa ni waliostasrabika wangeishi wote kwa amani na kuheshimiana.

Waziri Rabin alipigwa risasi na kijana mwenye msimamo mkali na sio kundi la wayahudi na alitumikia kifungo jela. Kwenye kila jamii kuna watu wema na wabaya. Huu mgogoro ukiuangalia bila kuwa na hisia za upande utagundua kuwa hakuna upande ulio sahihi.
Tukijadili asili basi wote hapa Dunain tulijikuta tuko katika maeneo mengine kwasababu mbalimbali eidha viita au njaa.

Kabla ya vita ya kwanza kuanza mwanzirishi wa harakati za kutafuuta eneo la wayahudi Theodor Herzl alianza kupendekeza Uganda 1903 baadae akapendekeza Argentina ila yalikataliwa!

Palestina kipindi hiki hipo chini ya ottoman na kipindi hicho bado kulikuwa na taratibu za kukonka eneo na kuchukua kuuwa lako ukishinda, Sheria za kimataifa bado wakati uo.

So baada ya www1 Uingereza anashinda na kumtoa Ottoman moja kwa moja anaanza harakati za kuipatia eneo Israel ndani ya Palestina, ikumbukwe hapa Uinngereza alikuwa amepewa Taifa la kamiili la Palestina kuliangalia mara baada ya kumshinda Otttoman. Chakushangaza Uingereza anatoka Palestina ila anmpa Uhuru Israel na sio akiomtawala yaani Palestina.

Msingi wa tunaobisha tukisema twende kisheria na historia haakuna hatuatenda kwenye mkutano wa UN na biblia cos biblia haitufanyi kusikilizana ila tutaenda na sheria za kimataifa, hapa ndipo tutarejea historia na. Kujiuliza kama UN ilikuwa na nia njema pale Palestina ilikuwa Wayahudi laki 6 wapewe 55% ya ardhi alafu Wapalestina wapewe 40% ya ardhi?

Imekuaje mara baada ya kuanza mitafuruko Israel imechukua ardhi ya Wapalestina hiyo 40% na kujenga makazi ya walowezi? Sheria za kimataifa ziko wapi?
 
Uganda, Argentina na Palestine yalikuwa mapendekezo lakini viongozi wao wengi waliona Palestine ndio logical place kutokana na historia yao. Swali je, ni kweli Palestine kuna historia ya Wayahudi? Kama ipo kwanini wasiwe na haki ya kuwa nyumbani kwao pia.

Kumbuka kipindi wanaishi ulaya hawakuwa na taifa waliishi kama wakimbizi ndipo wakaanzisha hiyo movement ya “national building movement”, Zionist movement haikuwa siri. Ndio maana British alifanya publicity. Kwa mfano angechagua Uganda ingekuwa the same pia.

Swali, je Arab palestine hawakuelewa lengo la zionist movement? Jibu ni kuwa walikuwa wanajua nini kitafuata na wengine walikubaliana na wengine hawakukubaliana.

Hawa jamaa walikubaliwa kuunda taifa lao pale kutokana na fact kuwa pale ni sehemu waliyokuepo kabla na pia sababu nyingine ni kutokana na ushawishi mkubwa waliokuwa nao. Sometime dunia huwa haipo fair kabisa maamuzi yanategemea interest za watu. Ndicho kilochofanyika na mwisho wa siku majamaa yakaanza kutanua mipaka.
 
Shida ni kwamba nchi ikigawanywa Jerusalem inakuwa upande wa Palestine
Nchi ilishagawanywa miaka mingi na mipaka ilishawekwa ugomvi unaoendelea ni kutokana na upande mmoja kuvuka mipaka na kukalia ardhi ya mwenzie kimabavu
 
Back
Top Bottom