Bila kuleta udini na uhafidhina, kati ya Israel na Palestina nani aliyevamia eneo la mwingine?

Bila kuleta udini na uhafidhina, kati ya Israel na Palestina nani aliyevamia eneo la mwingine?

Nitajitahidi sana kutokuweka mambo ya DINI though ni ngumu kukwepa kwa 100%.
Wanaosema Israel imeundwa mwaka 1947/8 hawana wanacho kijua; wangepumzika kwanza. Chanzo cha kitu kinaitwa Israel/Wayahudi na Waarabu ni mtu 1 anaitwa Ibrahim mwana wa Tera; huyu bwana alikua mwenyeji wa taifa linaitwa Uli ya Ukalydayo (sasa Iraq ) huyu bwana alitokea familia ya wafugaji specifically KONDOO na ngamia, Iraq ndio kitovu cha hi dunia, huyu bwana alihamia hapo panapoitwa Palestine or Israel hi ya leo, walikiwepo wenyeji wanaitwa Wahiti, Wahivi, Wakaanani nk. Waliishi kwa pamoja bila shida; baadae huyu Ibrahim alikwenda uhamishoni Misri kukimbia njaa then alirudi na binti wa Kimisri kama house girl; hakubahatika kupata mtoto na baadae alikuja kuzaa na huyo house girl wake, mtoto huyo wa house girl ndio chanzo wa Waarabu wote wa leo; baadae alipata mtoto kwa mkewe aliyeitwa Isaka/Isaac/Isihaka; Isihaka alizaa mapacha, mmoja ndio baba wa Waisrael hawa wa leo na pacha mwingine aliitwa Esau ndio baba wa taifa lilitwa Edom or Lebanoni ya leo; so you can see jinsi gani hawa watu walivo na undugu wa karibu. Well, Yakobo aliishi hapo hapo kwa babu yake Ibrahim na wanae na baadae nae alikimbilia Misri kama babu yake; huko walizaliana kwa wingi, both watoto na mifugo; baada ya miaka 430 kupita ndio waliporudi nyumbani kwao wakiongozwa na Musa, hapa sasa ndipo ilipoanza TABU, walipigana sana kwa zaidi ya miaka 2000; wakati Yesu anazaliwa; wote pale mashariki ya kati walikua wanatawaliwa na dola ya Rumi so sio Waisrael/Wayahudi wala Waarabu or Wapalestina walikua na chao, wote walitakiwa kua chini ya mtawala anaitwa Rumi; mwaka 70 AD, Dola ya Rumi alipiga hekalu/synagogue/kanisa na kuua Wayahudi wengi; walitawanyika sehemu mbalimbali za dunia hasa Ulaya, Africa hasa Misri na Ethiopia na waliobaki wengi wao waliuawa na wengine walijiua wenyewe; miaka imekwenda sana, baadae ndio wakaanza kurudi tena nyumbani, hi ndio wanayo ijua wengi. Again, walikimbia mauaji huko waliko kua hasa German ya Hitler, Poland kuliko kua na kambi ya Sobibo na Romania as well; wale waliokua Russia, Ulaya ya Magharibi pamoja na Marekani walibaki huko huko hadi miaka ya 60, 70 na 80 nao baadhi wakaanza kurudi nyumbani; hi hasa baada ya Ukomunisti kufa, walirudi wengi nyumabni.
Baadae naweza kuelezea why mataifa mengi ya mashariki ya kati yanao wengi sana na hawajulikani, mataifa kama Iran, Iraq, Saudia, Syria na hata Misri plus Ethiopia
Mbona wanasema Misri ilikua nchi ya watu weusi sio waarabu?
 
Then who are Palestinian mfano Sinwar...
What is their origin
Kwanza hakuna kabila lililoitwa wapalestina. Eneo la pwani ambako waliishi wavuvi, ambao wengi walikuwa ni wafilisti, ndiyo pekee liliitwa palestine kwa sababu ya jamii ya wafilisti.

Warumi walipozipiga JUDA NA ISRAEL KINGDOMS, kama njia ya kuwadhalilisha wayahudi, wakaanza kubadili eneo lote na kuliita Palestine ili tu majina hayo mawili yenye nguvu za kiutawala yapotee. Hawa wanaoitwa sasa wapalestina, kiuhalusia ni waarabu.
 
Mwambie atuonyeshe Solomon's templet kama kweli anaweza afu huyu anaonyesha hata Uislam haujui hakuna Mitume walio kuwa sio Waislam.

Uislam unasema Nabii Sulaiman aliu rebuilt Masjid Al Aqsa with the help of the natives ye anasema Solomon's templet 😄
Dogo, hujui mambo🚮
Tulia
 
Unajua Wakanaani sio waarabu Wala siô Waisrael?
Wakanaani ni jamii Kutoka Kwa Hamu( Hamites ) àmbao kiasili ni Watu weusi(wanjano) kama Wamisri.
Hilo Eneo kuanzia Kanaani(Palestine) kurudi chini Moja misri siô maeneo ya Waarabu Bali jamii ya Hamites.

Hivyo waarabu na Wayahudi wamevamia maeneo ya Hamites
Na mimi nachojua Misri waarabu walivamia pale sio kwao
 
Israel alivamia eneo la mwenzake , na Israel imeundwa mwaka 1948 , wakati Palestina ilikuepo muda mrefu sana
Kila anayeamini/aminishwa kwamba Israeli haikuwepo kabisa au ilianzishwa mwaka 1948 anapaswa aidha aelimishe iliyo kweli au alazimishwe kuuelewa ukweli kwamba ilikuwepo.
 
Tukianza kupitia vifungu kwenye vitabu vya Kidini hapo tunaenda kinyume na Uzi, ukiachana na mambo ya dini, nani aliyemvamia mwenzie kati ya Israel na Palestina?
Huwezi kutenganisha Mgogoro baina ya Israel na Palestina na yaliyoandikwa kwenye Biblia. Ukiamua Kutenganisha ni kwenda kinyume na UKWELI.

Ipo hivi; Ibrahimu ndiye baba wa Taifa la Israel. Na ni mwenyeji wa Uru wa Wakaldayo. Inasemekena ni eneo lililokuwepo baina ya nchi za Iraq na Iran. Mungu ndiye alimwagiza Ibrahimu atoke kwenye nchi yake ya asili aende kuweka makazi eneo walipo Waisrel kwa sasa- nchi ya Palestina, na walikuwepo wenyeji. Sasa tunajua hii dunia Mungu ndiye aliiumba. Hivyo ana mamlaka ya kufanya lolote atakalo- Kama alivyoamua
kumpa Ibrahimu na uzao wake (Waisrael) nchi ya Palestina.

Je, wewe mwanadamu ni nani hata uhoji na kupingana na maamuzi na maelekezo ya Mungu? Kujaribu kuhoji mamlaka na maamuzi ya Mungu ni utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu kabisa. Wapalestina wangekubali na kutii maamuzi na maelekezo ya Mungu, kwamba nchi yao walipewa Waisrel- huu ugomvi ambao umekuwepo kwa miaka mingi usingekuwepo. Sasa kwa kuwa ni wakaidi ndio maana wanapigwa.
 
Japo katika kujibu swali hili kutahitaji historia, naomba tujitahidi tusilete udini bali chanzo halisi cha mgogoro huu wa Palestina na Israel.


Ninachokijua kime-base kwenye dini na ndio maana nashindwa kukiweka hapa, nawaomba wataalamu wa Historia ya Israel na Palestina watusaidie, pia mtu yoyote aliye na uelewe wa haya mambo anaombwa achangie.
Tundu Lissu pamoja na uliberali wake lakini kaliongelea historia ya Palestina na mazayuni vizuri sana:


View: https://youtu.be/uuCyN8MHBn8?si=LytPqkYhGCV41cn7
 
Ukiingia ndani kwenye maandiko
Hata Tanzania tupo eneo la Israel
Israel walipewa nchi kubwa sana
 
Japo katika kujibu swali hili kutahitaji historia, naomba tujitahidi tusilete udini bali chanzo halisi cha mgogoro huu wa Palestina na Israel.


Ninachokijua kime-base kwenye dini na ndio maana nashindwa kukiweka hapa, nawaomba wataalamu wa Historia ya Israel na Palestina watusaidie, pia mtu yoyote aliye na uelewe wa haya mambo anaombwa achangie.
Tupate historia kidogo maana wengine wana mahaba ya kidini ambayo tulipigwa na kitu kizito kichwani na Wazungu na Waharabu

View: https://youtu.be/uuCyN8MHBn8?si=e_N-udxVIY5bs7sy
 
Japo katika kujibu swali hili kutahitaji historia, naomba tujitahidi tusilete udini bali chanzo halisi cha mgogoro huu wa Palestina na Israel.


Ninachokijua kime-base kwenye dini na ndio maana nashindwa kukiweka hapa, nawaomba wataalamu wa Historia ya Israel na Palestina watusaidie, pia mtu yoyote aliye na uelewe wa haya mambo anaombwa achangie.

View: https://x.com/Osint613/status/1848343469929930805
 
Back
Top Bottom