Hesabu 33:Japo katika kujibu swali hili kutahitaji historia, naomba tujitahidi tusilete udini bali chanzo halisi cha mgogoro huu wa Palestina na Israel.
Ninachokijua kime-base kwenye dini na ndio maana nashindwa kukiweka hapa, nawaomba wataalamu wa Historia ya Israel na Palestina watusaidie, pia mtu yoyote aliye na uelewe wa haya mambo anaombwa achangie.
Kisha Bwana akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko na kumwambia:
"Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka Mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote (Wakanaani) wa hiyo nchi mbele yenu.
"Nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunjavunja mahali pao pote palipoinuka Nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki.
"Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo. Hao walio wengi mtawapa urithi zaidi na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao. Mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake. Mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo.
"Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu, ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa."