Bila kuleta udini na uhafidhina, kati ya Israel na Palestina nani aliyevamia eneo la mwingine?

Hesabu 33:

Kisha Bwana akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko na kumwambia:

"Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka Mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote (Wakanaani) wa hiyo nchi mbele yenu.

"Nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunjavunja mahali pao pote palipoinuka Nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki.

"Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo. Hao walio wengi mtawapa urithi zaidi na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao. Mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake. Mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo.

"Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu, ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa."
 
Mwaka 1948 wakati Taifa la Palestine linaundwa je kuna wapalestina waliondolewa hilo eneo??
Au lilikuwa halina mtu?
Jamii zote zilikuepo hasa nani apewe mamlaka , japo waarabu ndio wakazi waliokuepo toka awali , hao wengine ni wahamiaji wa eneo lile , wakitokea maeneo mengine , tufuatilie machapisho mbalimbali kufahamu ukweli wa mambo
 
Nashukuru kwa mchango wako ila ukianza kunukuu vifungu vya vitabu vya dini unaenda kinyume na Uzi. Tukiwa neutral bila ku-base kwenye dini na uhafidhina, ni nani aliyevamia ardhi ya mwenzie kati ya Palestina na Israel?

Ukisoma vitabu hivi viwili-Quran na Biblia unapata mikanganyiko na ndio maana nimeonelea kuachana na misingi ya dini.
 
Suala la wapalestina na waisrael ni la kimungu mwenyewe,lilitokana na mwendelezo wa kizazi cha Ibrahimu kushindwa kutekeleza maagizo ya Mungu ya kuwaangamiza wenyeji wote wa kanani ndipo aweze kuimiliki nchi ya Canaan aliyopewa na Mungu,ambaye aliapa kutokuwaangamiza wa Canaan kwa kuwa aliyetakiwa kuwaangamiza hakuwaangamiza na kwamba watakuwa mwiba kwao mpaka mwisho wa dunia.
 
Umechagua upande wa dini, itakuwa ngumu kujibu hoja zako. Ahsante kwa mchango wako ila upo kinyume kabisa na huu Uzi.
 
Palestine wanacho kiti umoja wa mataifa bhana
 
Wapalestina wametajwa wapi kwenye Qoroani? Na historia yao ipo wapi ilianzia kingdom ipi na mfalme wao aliitwa nani?
 
Palestine wanacho kiti umoja wa mataifa bhana
Kilirudishwa baadae , miaka ya 1980 hadi 1990 , hivi unafahamu Israel pekee ikiitwa nchi , Palestina ikiitwa mamlaka na haikutakiwa kua na jeshi , walinda amani wakitokea UN , hadi akina Arafat walivokomaa sasa rasmi
 
Hadi Karne ya 12 eneo lile liliitwa peleset , wakati wengine wakiita Canaan au promised land , peleset au Palestina ndio ilianza kabla ya unachokiita Israel , machapisho yapo maktaba mbalimbali hasa egypt
Mkuu kwanini uanzie karne ya 12 wakati ukirudi nyuma kuna viashiria kwamba hilo eneo lilikuwa la israel. mfano utawala wa mfalme Daud na kisha mtoto wake mfalme Suleiman alijenga had hekalu maeneo hayo utasemaje kwamba hapo sio kwao hao Israel?

Tupe vielelezo vya hilo dola la Palestina kama lilikuwepo awali na wafalme wake waliitwaje na kama kuna vielelezo kama hapo juu.
 
Wapalestina ndiyo waliovamia ardhi ya Waisrael wakati Waisrael wakiwa uhamisho by kutawanywa katika mataifa mbali mbali tangu miaka ya 70 AD!
1948 wakarudi kutoka Ujeruman baada ya mauaji ya Holocaust!
 
Umechagua upande wa dini, itakuwa ngumu kujibu hoja zako. Ahsante kwa mchango wako ila upo kinyume kabisa na huu Uzi.
Bila kuingiza habari za kile unachoita kidini japo kuwa siyo kidini kama unavyoamini wewe, kwa kuwa Mungu ni Mungu na dini ni dini kamwe hutaweza kupata jibu la swali lako.
 
Wapalestina wametajwa wapi kwenye Qoroani? Na historia yao ipo wapi ilianzia kingdom ipi na mfalme wao aliitwa nani?
Hilo linawaumbua sana! Kingdoms zote middle east zinafahamika; hapajawahi kuwepo kingdom yoyote related to kabila la mchongo Palestine.
 
Sawa mkuu
 
Kiufupi wenyeji wa hapo aswa hawajulikani maana hao wakuja hapo kwa maana ya waisrael na waarabu waliingia hapo kwa vita sana, kama muisrael aliambiwa kabisa awaue wenyeji bila kuwaacha hai hata mmoja, kwahiyo kwasasa wenyeji wamejichanganya miongoni mwa wapalestina wengine walikimbia kuokoa maisha yao , hivyo ndivyo mambo yalivyo
 
Hao Israel (halisi) wako wapi?
Kuna Wayahudi wengi wa kisasa ambao hawana kabisa ukoo wao kwa Yakobo na wanawe. Wanajiita Wayahudi kwa sababu ya dini zao.

Watoto 12 wa Yakobo walisha gawanyika walio baki pale ni walikuwa Waislamu wametokana na kizazi cha mwanae Yousuf ambaye mnamuita Joseph ndio siku zote tunajaribu kuwafahamisha Yahudi ni dini na Israel ni mtu lakini hamtaki kufahamu.
 
Aliyewaambia (waamuru) wa-Israel wawaue wenyeji ni nani?
 
Ila kwa kweli mie kuna vitu vinanichanya sana, tuseme Kenya, Uganda na Tanzania wote weusi yaan African alafu gafla anatokea Mzungu anaanza kusema yeye ni Mzawa na ndio mwenye asili ya Tanzania, Hii inaingiaje akilini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…