Bila kuleta udini na uhafidhina, kati ya Israel na Palestina nani aliyevamia eneo la mwingine?

Kama hutumii rejea za kidini Wa-Israeli walikuwa wakazi asili wa eneo hilo walilopo leo kwa hiyo swali lako ni null and void kama kuuliza leo Watanzania walipata ardhi yao kutoka kwa nani.
Juu pale umesema Israel alipata aridhi yake kwa sababu ya vita. Ndio nikakuuliza alipata kutoka kwa nani?.

Kama hutumii rejea ya kidini kwa nini Israel mpaka mwaka 1948 hakua ndani ya nchi yake?. Na kwa nini alitaka kupelekwa Asia, middle east, pamoja na Africa wakachagua middle east?.

Nini kilisababisha mpaka Rooselvet from Austria ashawishi kuundwa kwa nchi ya Israel ambae nae alikua Austria Jews?.
 
Sisi hatutakiwi kufanya nukuu ya vitabu vya dini-Quran na Biblia. Ukipitia mwanzo wa Uzi utaelewe mjadala huu unaendaje.
Nazungumza kwa hao wanaoamin aridhi hio wameahidiwa na Mungu, ambae Mungu huyo nae anaonyesha kwamba haikua aridhi yao. Nimeshakuelewa mkuu.
 
Sikiliza hawa waislam walioanza kujielewa

View: https://youtu.be/TTfLeoy2bQQ?si=IlUUXJQUC0DCVOkK
 
And We gave Moses the Scripture and made it a guide for the Children of Israel, ˹stating:˺ “Do not take besides Me any other Trustee of Affairs,

Allah mwenyewe huyo! Anaitambua Israel vilivyo! Mafilisti are nowhere to be recognized.
 
Mzee baba Abraham hakuwa Myahudi, na Uyahudi haukuwepo kipindi Abraham yupo.

2. Hakukuwahi kuwa na sehemu ikiitwa Israel, ila kulikuwa na jamii ya kama ukoo au kabila ndiyo maana wakiita uzao wa Israel kama unavyoweza kuita leo Mangi etc! Ata Yesu alipokuwepo hukuwahu kuona kuwa alienda Israel ila utaona ikitanwa Jerusalem etc!.

3. Israel ki geographia m hakato wake wa kuanzishwa ulianza Nov 2, 1917 mara baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Arthur James Balfour kumuandikia barua Lord Rothschild mwakilishi wa Wayahudi ikimueleza kuwa Uingereza iko tayari kuanzisha makazi ya kitaifa ya wayahudi katika eneo la Palestina.
 
Wa-Israeli wamekuwa kwenye hiyo nchi miaka yote kabla ya kuwa taifa la Israel rasmi mwaka 1948 kulikuwa na wayahudi karibia 50,000. Wakati wa utawala wa Mamluk ndipo walipopungua na kubaki kama 3000, wakati wa Ottoman Empire wakarejea.
Wa-Israeli wamekuwepo Palestina kipindi chote cha Roman Empire na hata kuwa koloni la Warumi.
 
Umenukuu Biblia tena, vipi mkuu?
Anaejenga hoja kuwa kulikuwa na Israel kabla ya Palestina hawezi kuithibitisha hoja yake pasi kuleta vifungu vya biblia, ili kumuweka sawa akuelewe lazima tumpe vifungu hivyo hivyo.
 
Herode mfalme wa Wayahudi wakati wa Roman Empire alikuwa anatawala wapi??
 
Anaejenga hoja kuwa kulikuwa na Israel kabla ya Palestina hawezi kuithibitisha hoja yake pasi kuleta vifungu vya biblia, ili kumuweka sawa akuelewe lazima tumpe vifungu hivyo hivyo.
Ipo Historia secular ya Herode mfalme wa Wayahudi.
 
Hajui ashike lipi aache lipi huyo. Akienda kihistoria moto; akienda kidini ni moto zaidi.
Unajua wewe ndiye huelewi maana kihistoria hakuna uthibitisho wowote unaoweza kuuweka hapa kuonesha Israel ilikuwepo kabla ya Palestina bila kunukuu vitabu vya dini ijapokuwa tuntatofautiana katika kuelewa kifungu husika.
 
Unajua wewe ndiye huelewi maana kihistoria hakuna uthibitisho wowote unaoweza kuuweka hapa kuonesha Israel ilikuwepo kabla ya Palestina bila kunukuu vitabu vya dini ijapokuwa tuntatofautiana katika kuelewa kifungu husika.
Pontius Pilate(Pilato) alikuwa gavana mrumi wa Judea ambayo ndiyo Israel ya leo na yuko kwenye Historia ya kidunia(secular).
 
Nioneshe uhalali wa Israel kihistoria.
Kuna watakaoanzia pale jews sababu iliyowafanya wakimbie jerusalem na kusambaa huko ulaya.
Ubaya wa historia ya mgogoro huu ni kwamba watu wanaanzia pale wanapoona pataunga mkono madai yao.
One thing mimi kama mimi nachopinga, ikiwa wangoni zama hizi hawawezi kurudi s.a kudai eneo lao, why jews walipewa exclusive ya kufanya hivyo in modern times wakati zama za kuhama hama hovyo tayari zimekwisha?
 
Historia ya Wangoni na Wayahudi ni tofauti sana. Chuki iliyopitiliza(kutokana na conspiracy theories mbalimbali) dhidi ya Wayahudi na baadaye ushawishi wa Jewish Lobby huko magharibi ndicho kilichowafanya wakubwa wa dunia kuamua hawa watu warudi kwenye ardhi yao ya zamani tu kuepusha mizozo zaidi na holocaust.
 
Pontius Pilate(Pilato) alikuwa gavana mrumi wa Judea ambayo ndiyo Israel ya leo na yuko kwenye Historia ya kidunia(secular).
Embu elewa wewe kenge! Nimekuambia hakukuwahi kuwa na eneo likiitwa Israel mashariki ya kati toka Abraham anafika toka Mesopotamia mpaka Herode mkubwa anatawala Yudea.

Kulikuwa na Herode mkubwa alianza kutawala Yudea 37 - 4 Kabla ya kristo

Kulikuwa na Pilato alitawala Yudea badae na akaja Herode mdogo ambaye yeye alikuwa mtoto wa Herode mkubwa Galilaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…