Bila kuleta udini na uhafidhina, kati ya Israel na Palestina nani aliyevamia eneo la mwingine?

Bila kuleta udini na uhafidhina, kati ya Israel na Palestina nani aliyevamia eneo la mwingine?

wasipokuamini waambie wamuulize raisi wa ufaransa Macron juzi alithibitisha hilo...wasipomwamini huyo achana nao mbumbumbu hao
Mkuu, jibu ki-staha, huu ni mjadala. Katika mjadala hatuitani majina ya kebehi kama hayo uliyoyaandika-mbumbumbu, kila mtu anafikisha anachokijua, mwishowe tutapata ukweli.
 
wasipokuamini waambie wamuulize raisi wa ufaransa Macron juzi alithibitisha hilo...wasipomwamini huyo achana nao mbumbumbu hao
Ha ha ha! Macron tena? Haya, mtume mwingine huyo anaandika kitabu chake.
 
Mkuu, jibu ki-staha, huu ni mjadala. Katika mjadala hatuitani majina ya kebehi kama hayo uliyoyaandika-mbumbumbu, kila mtu anafikisha anachokijua, mwishowe tutapata ukweli.
"My learned brother" aka "wakili msomi" ni namna tu ya kistaarabu ya kuheshimu upande kinzani wanapokuwa na mijadala mikali mahakamani. Husaidia sana kupunguza "joto" baina ya pande mbili kila moja ikijitahidi ku-win case. That's it.
 
Umekaza nati! Pitia vizuri nilichokijibu. Jitahidi urejee kwenye mada, huku ulikoenda ni mbali sana.

Mada haihusiani na mambo ya Uumbaji, ila imejikita kwenye huu mgogoro endelevu kati ya Israel na Palestina.
Pole sana...ningekusaidia kukupa nyuzi za kuunganisha dot ya nilichokisema na mada lakini naona kama nitakuwa napoteza muda ivi.
 
Pole sana...ningekusaidia kukupa nyuzi za kuunganisha dot ya nilichokisema na mada lakini naona kama nitakuwa napoteza muda ivi.
Nisingeku-confront usingeongea haya yote! 😂😂😂, anyway I am all ears.
 
Uungane na mvamizi? Israel waungane na Palestina kweli? Ni ngumu mno. Hapo inabidi wazitwange tu mpaka mvamizi atakapotoka kwenye ardhi ya mwenzie.
Uvamizi wa Wapalestina uko wap?
 
Yakobo alikuwa ana watoto wakiume 12 wote kwa pamoja walikuwa wanaitwa Waebrania au Israelites.

Mataifa kumi yalichukuliwa uhamishoni wakati wa Uhamisho/Uvamizi wa Ashuru (Assyrians).

Makabila yalibaki ni Kabila la Yuda na Benjamin haya makabila mawali yakaunga yakaunda Dola inaitwa Judea.. neno Yahudi linatokana na (Yuda) na hii ni historical fact.

Tukizungumza Historia bila kuweka Quran (sababu sio historical text)

Sinwar kama Mpalestina historia yake haizidi vizazi 8 Hadi 10, Wapalestina wengi wameishi Hapo kwa Miaka karibu 400 tu, wakati wayahudi kabla ya mwaka 70AD Walioishi hapo kwa Miaka zaidi ya 3000.

Historia ya Palestina hata kwenye website yao inaanzia mwaka 1986.

Hata wakimzungumzia Yesu hawamtaji kama Myahudi wakati alikuwa Myahudi hawamtaji Daudi kama mfalme wa Dola ya Israel wakati alikuwa Mfalme wa United Israel kingdom.

Hakujawahi kuwepo taifa huru/Sovereign state au Ufalme wa Palestina ambao una Kiongozi wake.

logic ya madai ya Wapalestina Iko Lakini wote mnajaribu kuilezea kijinga au kwa hoja za kijinga
Una hoja, usikilizwe
 
Hesabu 33:

Kisha Bwana akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko na kumwambia:

"Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka Mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote (Wakanaani) wa hiyo nchi mbele yenu.

"Nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunjavunja mahali pao pote palipoinuka Nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki.

"Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo. Hao walio wengi mtawapa urithi zaidi na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao. Mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake. Mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo.

"Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu, ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa."
Mtihani wa jibu hili ni kuwa, Mfano mimi nikija kwako nikiwa na kitabu changu ninachokiamini na nikakuonesha mstari kuwa Mungu wangu kanila ardhi hii utanipisha?

Au Niende pale Magomeni Kanisani niwaambie kuwa jana nimetokewa na Yesu Kristu kaniambia eneo hili lote liko chini ya milki yangu nanyi mnipishe! Ao Maaskofu watanipisha? Au wataita ambulance nipelekwe milembe?
 
Hata Qur'an inawatofautisha kati ya Wayahudi.na Watoto wa Yakobo. Qur'an ina waita Bani Israel lakini Wayahudi inawaita Yahudi.
Mkuu,
Kabla Kurani haijakuwepo Wayahudi walikuwepo maelfu ya miaka kabla. Kwa hiyo Korani haiwezi kuwa rejea sahihi kwenye hilo jambo.

Hata kutofautisha Wayahudi na watoto wa Yakobo ni kichekesho kingine, maana makabila 12 ya Wayahudi yanatokana na watoto 12 wa Yakobo. Na kwa taarifa yako, jina lingine la Yakobo ni Israel
 
1920 hadi 1922 tayari muingereza alikua anaitawala Palestina kwa jina hilo hilo Palestina , baada ya wahamiaji wa kizungu kwa jina la kiyahudi kua wengi na wakaanzisha vurugu za kutaka watambuliwe na wao , muingereza na marekani wakaunda Taifa bandia kule ili kudhibiti eneo lile na maslahi yao , hivo mwaka 1948 ndio Israel inatangazwa nchi na umoja wa mataifa huku wapalestina wenye eneo lao wakinyimwa haki yao na kiti chao umoja wa mataifa wakakipiga pin, nini kilifanyika hadi waarabu wa eneo lile kunyanyaswa hadi Leo na kupata mateso miaka yote hiyo ndio unatakiwa ujifunze historia pale juu
Mkuu kwanini unaipotosha wazi wazi historia namna hiyo?
 
Back
Top Bottom