Nitajitahidi sana kutokuweka mambo ya DINI though ni ngumu kukwepa kwa 100%.
Wanaosema Israel imeundwa mwaka 1947/8 hawana wanacho kijua; wangepumzika kwanza. Chanzo cha kitu kinaitwa Israel/Wayahudi na Waarabu ni mtu 1 anaitwa Ibrahim mwana wa Tera; huyu bwana alikua mwenyeji wa taifa linaitwa Uli ya Ukalydayo (sasa Iraq ) huyu bwana alitokea familia ya wafugaji specifically KONDOO na ngamia, Iraq ndio kitovu cha hi dunia, huyu bwana alihamia hapo panapoitwa Palestine or Israel hi ya leo, walikiwepo wenyeji wanaitwa Wahiti, Wahivi, Wakaanani nk. Waliishi kwa pamoja bila shida; baadae huyu Ibrahim alikwenda uhamishoni Misri kukimbia njaa then alirudi na binti wa Kimisri kama house girl; hakubahatika kupata mtoto na baadae alikuja kuzaa na huyo house girl wake, mtoto huyo wa house girl ndio chanzo wa Waarabu wote wa leo; baadae alipata mtoto kwa mkewe aliyeitwa Isaka/Isaac/Isihaka; Isihaka alizaa mapacha, mmoja ndio baba wa Waisrael hawa wa leo na pacha mwingine aliitwa Esau ndio baba wa taifa lilitwa Edom or Lebanoni ya leo; so you can see jinsi gani hawa watu walivo na undugu wa karibu. Well, Yakobo aliishi hapo hapo kwa babu yake Ibrahim na wanae na baadae nae alikimbilia Misri kama babu yake; huko walizaliana kwa wingi, both watoto na mifugo; baada ya miaka 430 kupita ndio waliporudi nyumbani kwao wakiongozwa na Musa, hapa sasa ndipo ilipoanza TABU, walipigana sana kwa zaidi ya miaka 2000; wakati Yesu anazaliwa; wote pale mashariki ya kati walikua wanatawaliwa na dola ya Rumi so sio Waisrael/Wayahudi wala Waarabu or Wapalestina walikua na chao, wote walitakiwa kua chini ya mtawala anaitwa Rumi; mwaka 70 AD, Dola ya Rumi alipiga hekalu/synagogue/kanisa na kuua Wayahudi wengi; walitawanyika sehemu mbalimbali za dunia hasa Ulaya, Africa hasa Misri na Ethiopia na waliobaki wengi wao waliuawa na wengine walijiua wenyewe; miaka imekwenda sana, baadae ndio wakaanza kurudi tena nyumbani, hi ndio wanayo ijua wengi. Again, walikimbia mauaji huko waliko kua hasa German ya Hitler, Poland kuliko kua na kambi ya Sobibo na Romania as well; wale waliokua Russia, Ulaya ya Magharibi pamoja na Marekani walibaki huko huko hadi miaka ya 60, 70 na 80 nao baadhi wakaanza kurudi nyumbani; hi hasa baada ya Ukomunisti kufa, walirudi wengi nyumabni.
Baadae naweza kuelezea why mataifa mengi ya mashariki ya kati yanao wengi sana na hawajulikani, mataifa kama Iran, Iraq, Saudia, Syria na hata Misri plus Ethiopia