Hakuna aisee, umezidi uchawa, hata hivyo huwa naheshimu ustahimilivu wako pale members wanaposhindwa kujizuia na uchawa wako na kujikuta wakikuporomoshea matusi, mara zote umekuwa muungwana, huwa unawajibu kistaarabu, ila katika watu wanaochukiwa hapa jf wewe unaweza kuwa #2 na #1 akabakia nayo
Tlaatlaah
chuki binafsi haifai ndrugo yango
Capt Tamar
mwenye chuki dhidi ya mwingine kwasababu yoyote ile,
kwanza lazima awe ni mchoyo, lakini pia mbinafsi na mwenye kiherehere sana kwenye mambo hata yasiyo muhusu wala asiyo yaelewa
lakini pia wenye chuki, wengi ni waamini wa imani potofu za uchwi, nguvu za giza na washirikina balaa, aiseeeh....
ni watu ambao ni wavivu walio kata tamaa, na ambao wamefikia ukomo wa fikra mbadala, na matokeo yake hujikuta wakiporomosha matusi tu bila hata sababu za msingi ili mradi tu useme kinyume na mawazo yake
binafsi,
nakupenda, na nina kukubali sana sana gentleman, wewe pamoja na wote wenye kaliba na hulka ya chuki binafsi yoyote dhidi yangu.
Ninakuombea Baraka na Neema za Mungu ziambatane na kuandamana nawe daima, ili ninapo barikiwa na Mungu, basi, ujionee kwa macho yako mwenyewe, licha ya kwamba unaweza kuchukia zaidi....
aidha,
nawaombea moyo wa ustahimilivu na subra wale wote wenye chuki binafsi dhidi ya wengine, Mungu awape utulivu mkuu na kuwafanyia wepesi mioyoni mwao waondokane na roho hiyo mbaya ya chuki isiyojenga....
Tukijaaliwa baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu, nitakualika jimboni kwangu kama hutojali, tujumuike pamoja na kuona namna tunavyoweza kuondoa hicho kijiba cha roho ndani ya moyo wako dhidi yangu bila sababu yoyote, ili walau uwe huru....
Namuombea Rais Dr.Samia Suluhu Hassan, afya njema, bidii na moyo wa thabiti wa kuendelea kuwaletea waTanzania maendeleo huko waliko
