Bila kupepesa macho, Ni member gani haumkubali humu JamiiForums

Mbona wewe kenge unsalimia watu kilugha? Hata wewe hatukupendi
 
Inasikitisha sana

Hivi kuna watu wako serious na jf mpaka wanapata anonymous wa kuwachukia!!
 
Kama unapata mshawasha wa kuchombeza anonymous huko pm sembuse kuchukia
Wote hao wanaochombeza anonymous pm, kuna wale SIMPS wanaowaandikia nyuzi mademu anonymous wa jf na nyie mnaowachukia msiowajua ni wehu

Mna matatizo ya akili. Epuka sana kuwa serious na mitandao ya kijamii kwa afya ya akili yako
 
I hATE you
 
chuki binafsi haifai ndrugo yango Capt Tamar

mwenye chuki dhidi ya mwingine kwasababu yoyote ile,
kwanza lazima awe ni mchoyo, lakini pia mbinafsi na mwenye kiherehere sana kwenye mambo hata yasiyo muhusu wala asiyo yaelewa

lakini pia wenye chuki, wengi ni waamini wa imani potofu za uchwi, nguvu za giza na washirikina balaa, aiseeeh....

ni watu ambao ni wavivu walio kata tamaa, na ambao wamefikia ukomo wa fikra mbadala, na matokeo yake hujikuta wakiporomosha matusi tu bila hata sababu za msingi ili mradi tu useme kinyume na mawazo yake

binafsi,
nakupenda, na nina kukubali sana sana gentleman, wewe pamoja na wote wenye kaliba na hulka ya chuki binafsi yoyote dhidi yangu.

Ninakuombea Baraka na Neema za Mungu ziambatane na kuandamana nawe daima, ili ninapo barikiwa na Mungu, basi, ujionee kwa macho yako mwenyewe, licha ya kwamba unaweza kuchukia zaidi....

aidha,
nawaombea moyo wa ustahimilivu na subra wale wote wenye chuki binafsi dhidi ya wengine, Mungu awape utulivu mkuu na kuwafanyia wepesi mioyoni mwao waondokane na roho hiyo mbaya ya chuki isiyojenga....

Tukijaaliwa baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu, nitakualika jimboni kwangu kama hutojali, tujumuike pamoja na kuona namna tunavyoweza kuondoa hicho kijiba cha roho ndani ya moyo wako dhidi yangu bila sababu yoyote, ili walau uwe huru....

Namuombea Rais Dr.Samia Suluhu Hassan, afya njema, bidii na moyo wa thabiti wa kuendelea kuwaletea waTanzania maendeleo huko waliko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…