Bila UMAFIA hujawa tajiri bado. Umafia ndio dira ya utajiri

Bila UMAFIA hujawa tajiri bado. Umafia ndio dira ya utajiri

Vijana msijidanganye wala msidanganywe na mawakili wa shetani hawa.

Fanya biashara yoyote kwa bidii na zungusha pesa kila fursa, kihalali, hakuna cha kukuzuwia kutajirika isipokuwa fikra zako tu.

Wachana na kufata wajinga wajinga wanaoamini hupati mali mpaka uwe mshirikina.
Adi CCM wezi bila kuiba hutoboi
 
Mbona sijawahi kuyaona Kwa Mark Zuckerberg,Jeff bezos, warren Buffett,amancio Ortega, Bernad arnault, Elon musk , Na matajiri wengine.

Matajiri wengi wa bongo Hela zao ni za makando kando lazima uwe na roho mbaya
Hao jamaa kina zucker etc biashara zao ni za uvumbuzi sasa huku kwetu uchuuzi wa bidhaa kila mtu anafanya lazima kona kona zihusike
 
Mpaka ufikie level ya kuwa tajiri, ni lazima uwe umefanyiwa umafia hadi na wewe unakuwa mafia mkubwa.

Utajiri ni himaya, kila jicho linaiangalia himaya kwa husda. Kuna uchawi, ujambazi, figisu na michezo yote michafu.

Ukiwa tajiri utajilinda wewe na uzao wako kiroho, kimwili na kitàaluma ili usipitwe na teknolojia.

Bila kuwekeza kwenye teknolojia utajiri wako utakuwa ni wa muda mfupi tu.
chai
 
Mbona sijawahi kuyaona Kwa Mark Zuckerberg,Jeff bezos, warren Buffett,amancio Ortega, Bernad arnault, Elon musk , Na matajiri wengine.

Matajiri wengi wa bongo Hela zao ni za makando kando lazima uwe na roho mbaya
Je mazingira ya bongo ni rafiki kwa wewe kuwa tajiri?

Maana nahakika mazingira ya bongo na mifumo ingekuwa kama ya ulaya huenda leo afeica ingekuwa kinara kwa mabilionea
 
Kabisa mkuu....matajiri wanaishi maisha ya ajabu sana..yupo mmoja kula yake ni ya bei ya chini mno...haangalii TV hana starehe yeyote.......halafu anasoma sana...hajichanganyi na watu....akipewa mwaliko anatuma mwakilishi......T shirt zake na jeans zina miaka zaidi ya 10.....report za biashara zake anapenda kuziweka kwenye graph,histograms,pie chart etc.
duh! Huyu naye au ni utajiri wa
 
Kuvaa nguo za gharama, na kula vyakula vya bei mbaya migahawani ni kiashiria cha umasikini.

Unaponunua nguo za gharama kila wakati na kula vyakula kwenye migàhawa ya kifahari, jua kwamba wewe ni mrija wa utajiri wa mtu fulani. Unampelekea pesa, je wewe anakupa nini?

Ukipunguza matumizi yasiyo ya lazima, ukaanzisha kabiashara kako kadogo, utatamani kukakuza na kukaongeza kabiashara kako hako.

Pia chakula cha kula nyumbani kiko healthy na fresh
halafu chakula cha home hakinaga mazingaombwe
 
Nilisha wahi kuhangaika sana na maisha ya utafutaji. Victim wa kuibiwa nikawa mimi, victim wa kutapeliwa nikawa mimi. Michezo yote michafu nafanyiwa mimi, hadi kusingiziwa uongo mkubwa.

Kwa kweli kuufikia utajiri wenu ni kazi kubwa na ngumu.

Nilianzisha kiwanda kidogo tu, vita haziishi, hadi kikatengenezwa tukio la moto
Pole mkuu hayo yapo dunia hii ina vita kali sana
 
Sasa umebadili wimbo, siyo "umafia" tena?

Kijana hakuna utajiri wa namna hizo, utajiri ni mawazo yako tu.

AlhamduliLlah Uislam unafundisha namna kuwa utajiri, wanaofata njia hizo wanatajirika tu, hakuna cha kuwazuwia.

Kwanza ni lazima uelewe, kuwa tajiri siyo kuwa na pesa zisizokuwa na kazi.
Nionyeshe kwenye Quran walipoeleza namna ya kuwa tajiri
 
.....inaendelea....huyo tajiri kimsingi nimesoma nae darasa moja shule ya msingi hakuwa na uwezo darasani....form 4 alipata div 4....ila ametubeba sana kwenye makampuni yake.....washkaji wengine wana CPA lakini wanapewa maisha na huyu tajiri.......nakumbuka kuna siku tulikuwa nae Iringa......tulifunga mamilioni cha ajabu....sie asubuhi tunakunywa supu,yeye anakunywa maji ya uvuguvugu,mchana tunapata lunch yeye akaenda sehemu yenye kilabu cha pombe aka agiza kande za jelo...sie usiku tuna choma nyama na kuhangaika na pombe na upuuzi mwingine...yeye kitambo yupo chumbani na mavitabu yake......itaendelea.....
Huu sasa ni uongo
 
Kabisa mkuu....matajiri wanaishi maisha ya ajabu sana..yupo mmoja kula yake ni ya bei ya chini mno...haangalii TV hana starehe yeyote.......halafu anasoma sana...hajichanganyi na watu....akipewa mwaliko anatuma mwakilishi......T shirt zake na jeans zina miaka zaidi ya 10.....report za biashara zake anapenda kuziweka kwenye graph,histograms,pie chart etc.
Mbona mm nipo hivyo na sio tajiri
 
Maskini tuna story nyingi sana za utajiri na matajiri kwenywe vijiwe vya kahawa.
 
Siri zake mbona zipo wazi kabisa?
Ni kweli kabisa mbona zimeandikwa hata na Wazungu? Kuna kitabu kinaitwa The History of African in Business ukurasa was 369 au 385 kaelezewa Bakhresa Kwa uzuri kabisa

download.jpeg
 
.....inaendelea....huyo tajiri kimsingi nimesoma nae darasa moja shule ya msingi hakuwa na uwezo darasani....form 4 alipata div 4....ila ametubeba sana kwenye makampuni yake.....washkaji wengine wana CPA lakini wanapewa maisha na huyu tajiri.......nakumbuka kuna siku tulikuwa nae Iringa......tulifunga mamilioni cha ajabu....sie asubuhi tunakunywa supu,yeye anakunywa maji ya uvuguvugu,mchana tunapata lunch yeye akaenda sehemu yenye kilabu cha pombe aka agiza kande za jelo...sie usiku tuna choma nyama na kuhangaika na pombe na upuuzi mwingine...yeye kitambo yupo chumbani na mavitabu yake......itaendelea.....
Si useme kwa sentence moja sasa
 
Back
Top Bottom