Kanuni hii ni ya kwangu binafsi, Si kwamba ni kanuni ya watu wote.
Kanuni hii ni kutokana na kwamba watu wanaodai Mungu ni chanzo cha ulimwengu hawana UTHIBITISHO wa madai yao.
(Ni mawazo yao ya kufikirika tu)
Watu wengi wana amini Mungu Hana chanzo kwamba alitokea tu, Pia wana amini Mungu huyohuyo hana mwisho.
Watu wengi wameweza kuamini Mungu wasiyemjua Hana chanzo Lakini wana lazimisha kwamba Dunia ina chanzo, Na chanzo hicho wanadai ni "Mungu" Kwamba wana amini Haiwezekani Dunia iwe imetokea tu yenyewe Pasipo chanzo.
Sasa ni hivi[emoji116]
Kama "Haiwezekani" Dunia isiwe na muumbaji, kwamba lazima awepo aliye iumba "Imewezekana" vipi Mungu asiwe na Muumbaji?
Kama Mungu hana mwanzo, Inashindikana vipi kwa Dunia kutokuwa na mwanzo?
Huu ulazima wa kwamba Dunia lazima iwe na chanzo, ila Mungu yeye Hana chanzo uliwekwa na nani?
Hapa sasa ndipo,Kanuni hii inapo tumika kwamba,
Kama ni lazima kila kitu kilichopo kiwe na chanzo, Basi hata Mungu lazima awe na chanzo. Maana Mungu huyo bado "HAJATHIBITIKA" rasmi kwamba yeye ndio chanzo halisi cha ulimwengu.
( Bado ni mawazo na mafikirio ya watu tu)
Sasa kama bado Mungu HAJATHIBITIKA kuwa chanzo halisi cha Dunia, Hakuna ulazima wa kwamba Dunia imeumbwa na ina mwanzo.
Ila mtu akianza kuweka ulazima wa kwamba Dunia lazima iwe imeumbwa, Lazima athibitishe kwamba chanzo cha Dunia hakina mwanzo.
Na aeleze na kuthibitisha chanzo hicho cha Dunia, kimewezaje kuwepo bila chanzo kingine.