Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Huu uhuni wa Kishenzi ulianzia Mwanza toka kwa mwanachama wa utopolo Mtanda kwa maelekezo toka Juu kwenyr uongozi wa utopolo

Hili la Dar tumeonyesha ukubwa wetu Simba ni dude kubwa sanaa "SIMBA TAIFA KUBWA"
 
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha leo Machi 8, 2025, ilipitia shauri la klabu ya Simba kuzuiliwa kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC (Young Africans SC vs Simba SC) uliopangwa kufanyika kwenye uwanja huo leo kuanzia saa 1:15 usiku.

Soma Pia: Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Katika shauri hilo, klabu ya Simba iliandika barua kwa Bodi ya Ligi kueleza kususu tukio tajwa hapo juu, huku pia ikieleza nia yao ya kuto shiriki mchezo huo kwa sababu wamezuiliwa kutumia haki yao ya kikanuni kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni ya 17:45 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

View attachment 3263593
Kwa Hili Mpira wetu unarudi nyuma sana.
 
Jambo lipo kikanuni team mgeni atatumia uwanja kwa mazoezi siku moja kabla ya mchezo sasa hapo unahitaji taarifa ya nn?
Ikitokea hawajatumia uwanja wagomee mechi?
 
Jambo lipo kikanuni team mgeni atatumia uwanja kwa mazoezi siku moja kabla ya mchezo sasa hapo unahitaji taarifa ya nn?
Yanga wametupita Hapa Geza wanaenda Uwanjani, Itakuwaje sasa?
 
Hamna kitu umeeleza bado ni blah blah, unaulizwa sababu zilitokea, unaanz akulala tff inahangaika na yanga, seriously? It that all?
Yanga iligomea mechi kwa sababu ya kubadilishwa kwa muda wa mchezo bila sababu yenye mashiko, TFF ilifanya makusudi ili kuiondoa Yanga mchezoni., kwa huu ujinga wenu wa kuhangaika nje ya mchezo makombe mtayasikia tu, kama mnavyoyasikia misimu yote.😀😂😂😂
 
Ujinga mtupu! Watu wamesafiri kutoka mikoani, mechi imefanyiwa promotion zaidi ya mwezi mzima alf ina ahilishwa kizembe!
Unafanya promotion ya mechi lakini unaruka baadhi ya kanuni za mchezo, lazima upate hasara.
 
Huwa Simba wanao huu utaratibu wa kufanya mazoezi wakiwa ugenini kabla ya mechi katika uwanja husika!? Au ndio kutafutiana sababu tu😁
Nachokiona hapa kwa wote, ni kuwa na imani za kishirikina badala a kuamini katika mazoezi, mbinu na matayarisho..!
Kanuni ya 17: 45 imewekwa kwa sababu za kiufundi.
Timu kujaribu kuizoea pitch, mwanga wa taa nk.
Taratibu hizo siyo ushirikina, kama unamzuia mpinzani wako asifike uwanjani wewe ndiye mshirikina.
 
Kuna watu wameingia chaka na msomali wao wa tifu tifu, tupo zetu uwanjani
 
Bodi ya Ligi imekuwa bodi ya HOVYO sana, kwanini mchezo uahirishwe? Mbona mchezo wa JKT Queens haukuahirishwa? Yanga hatupo tayari kwa mchezo siku nyingine na tunafahamu mchezo ni leo.FULLSTOP
Pole kwa makasiriko.
Siku nyingine mjifunze kuheshimu kanuni.
 
Nawambiaga kila siku Tifu Tifu ni muunganiko wa Simba na Yanga. Ingekua Pamba point 15 zingekatwa na wangeshushwa ligi. Ila kwa sabab ni hao hao wenyewe hamna lolote hapo.
Simba na yanga ndiyo alama ya mpira wa Tanzania.
Hata kama hupendezwi na hio lakini ndiyo iko hivyo.
 
sasa hii barua inasema kuna vitendo inachunguza hapo hapo inasema mechi itapangiwa siku nyingine

vipi kama uchunguzi huo utaonesha simba ana makosa
 
Ubaya Ubwela

Hiki kiburi kisiwe kwa Simba tu, bali timu yeyote inayofanyiwa mambo ya kihuni.. Yanga na mashabiki wake wamekuwa na mambo ya kisenge sana.

Mnakumbuka RC wa Mwanza? Tukaingiza timu, mwisho wa siku inaonekana kama kitu cha kawaida tu.
Si kweli mkuu... Wewe ni mtu mzima na una akili.
Usiwe boya .

Mmekimbia hii game.. pumbavu
 
Back
Top Bottom