Boeing wamefeli tena. Safari ya siku 8 imekuwa ya miezi 8

Nionavyo mimi Wamarekani wapo radhi hao wenzao wafie huko. MAGA itawazuia kuomba msaada kwa Wachina.
 
Humu bwana ubako kucheka yani mchini amzid uwezo marekani mtu ambae kaaanza kwenda space tpka 1998 huko come one bhana
 
Dah!... Africa lini tutapata mwakilishi huko anga za juu ?
 
Humu bwana ubako kucheka yani mchini amzid uwezo marekani mtu ambae kaaanza kwenda space tpka 1998 huko come one bhana
Acha kukariri, Soviet Union ndio walikuwa wa kwanza kutuma chombo anga za juu lakini wakaja kuachwa na Marekani kwenye space tech

Soviet Union walikuwa wa kwanza kutuma chombo mwezini, Marekani akadai amepeleka mwanadamu wa kwanza mwezini

Wakati huohuo China limekuwa taifa la kwanza duniani kufika moon's far side ambako hakuna taifa lolote limewahi kufika

Hiyo ni mifano michache inapohusu space tech au tech yoyote muda wowote unaweza kupitwa kiteknolojia watu wanafanya R&D na innovation usikariri
 
Hapo watengeneza movie tayari ni idea hiyo,itakuja movi inaitwa Trapped in the Outaa
 
Hapo wazee wa Hollywood wameshapata idea ya movie
"Trapped in the Outer space"
 
Hapo watengeneza movie tayari ni idea hiyo,itakuja movi inaitwa Trapped in the Outaa
Directors wa Hollywood wa movies za sci-fi wanalifuatilia tukio hili kwa ukaribu kupata idea sio?
 
Nionavyo mimi Wamarekani wapo radhi hao wenzao wafie huko. MAGA itawazuia kuomba msaada kwa Wachina.
Marekani ni watu makini kwenye safety ya watu wake. Ndio maana OSHA ndio wao waliianzisha na ilikuwa chini ya mamlaka yao ya ajira, kabla hawajaifundisha na kuisambaza duniani. Vitu vingi sana unavyotumia kwenye usalama ni vya Wamarekani.

Huwezi walinganisha Wamarekani na Wachina ambao waliwahi kuuana mamilioni kwa mamilioni kila baada ya miaka kadhaa. Mara ya mwisho hapo Mao Zedong alisababisha njaa kuanzia 1959, njaa kubwa zaidi ya mwisho kutokea duniani wakafa Wachina zaidi ya milioni 30 kwa sera mbovu za kiongozi wao.

Kwanza kwa taarifa yenu Boeing Starliner imetua duniani salama kabisa kwa autopilot, na haikuwa na tatizo lolote hivyo hata wangekuja nayo hawa astronauts wawili isingekuwa shida. Boeing walihakikisha iko sawa, NASA hawakubisha ila walitaka kuwa na uhakika kabisa. Wamefanya hivi tabia za Kimarekani kuzingatia usalama.

Wachina waombwe msaada kwa lipi? Tueleze ni capsule gani ya Kichina inaweza dock pale ISS.
 
Mbona Marekani wameshawahi kuuana sana kwenye American Civil War
 
Bora hata ya hao Boeing sisi tunaowasema tumeweza nini hata kwa 2% sanasana kutekana na kupotezana Tumeshindwa hata kulindda rasilimali zetu
 
Kwa hiyo kusema watawarudisha February 2025 ni kwa sababu za kiusalama?

Kutua duniani salama kwa autopilot bila astronauts ndio kufeli kwenyewe

Boeing wamekiri wenyewe kuwa Starliner ina hitilafu wewe ni nani uwabishie?
 
Sure wamarwkani usalama kwanza hao wachina usalama kwao 0 hata wakifa hawana shida.
 
China wana Spacesail kucompete na Starlink, upande wa reusable spacecraft wana Mengzhou
Mengzhou itawapeleka astronauts wa China watue kwenye mwezi. Project ni waweze kutua mwezini miaka ya 2030s, jambo ambalo Marekani walifanya 1969. Hiyo ni gap ya miaka 60!

Alafu anatokea muuza nyanya mmoja anakwambia eti Marekani iwaombe msaada China kurudisha astronautsšŸ˜‚

Alafu China wanacompete na SpaceX kwa product iliyopo, bado hujui ni kampuni gani nyingine ya Marekani inakuja na lipi. Wakati SpaceX ina maelfu ya satellites angani inatoa internet hadi Kenya, hadi Ghana. Ndio kwanza Wachina wanataka kuwa na uwezo kuanzia mwakani. Elon Musk amerusha rockets zake za Falcon 9 mara 381 tangu 2010. Wana satellites zaidi ya 6,000 za internet.

Wachina tulieni kwanza haya sio mayeboyebo kwamba unafyatua tu.
 
Mengzhou itawapeleka astronauts wa China watue kwenye mwezi. Project ni waweze kutua mwezini miaka ya 2030s, jambo ambalo Marekani walifanya 1969. Hiyo ni gap ya miaka 60!
Soma meseji #45
 
Wakati SpaceX ina maelfu ya satellites angani inatoa internet hadi Kenya, hadi Ghana. Ndio kwanza Wachina wanataka kuwa na uwezo kuanzia mwakani
Mbona wameshatuma satellite mkuu? Au hauna hizo taarifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…