Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Mimi naweza sema nilikuwa karibu zaidi na mahali bomu lilipolipuka na pia tulikuwa hasra zaidi polisi walivyokuwa wanamkimbiza mlipuaji wakati sisi tulikuwa tunamtaka tummalize hapo hapo

So confirmed kuwa mtuhumiwa kachukuliwa na Polisi na dhamira ilikuwa ni Jukwaa Kuu.
 
unamfahamu mtu anayeitwa lwakatare, ben sa8, ludovick na vijana wao? Usifanye mchezo zile ni machine hatari sana ni kama idd amin

Ni makamanda wa vita, wanaweza fanya multiple right things at the same time..kutoa huyo ktk red.tabaki kulia na magazeti yanapomwaga story zinazomzimisha huko ndani na ameshakiri kuwa ni gaidi ambaye atapatikana na hatia wakati wengine wakiachiwa huru.

Mwaka wa shetani kwa CCM.
 
Je vilaza wa CCM ambao wanasema kwamba CHADEMA wamefanya njama unaona ni sawa??

Mimi naona uchunguzi unatakiwa, na kukurupuka kwamba CCM ndio waliotega bomu, au CHADEMA ndio waliotega bomu, kabla ya uchunguzi hakufai.
 

Hakuna kipya hapo..yote yanajulika..yote yalishatokea tena ktk miaka ya karibuni.Polisi sijui km watamwacha huyo msomali baada ya kuwataja wenzie....lazima kaliwe na fisi..ama kwa wema au akwa ubaya.
 

Mara zote uchunguzi na ushahidi utangulie conclusions. Sio conclusion zitangulie kabla ya uchunguzi na ushahidi.

Katika scientific research, kuna chunguzi nyingi sana wataalam wamezianza ili "kufuata formalities tu" za kisayansi, kwa sababu walifikiri kwamba majibu wanayo tayari. Wakaingia katika uchunguzi na kukuta data zinawapeleka tofauti na kule walikofikiria awali. Hapo ndipo umuhimu wa uchunguzi na ushahidi unapokuja.

The Michaelson-Morley was supposed to be able to easily solidify the proof of the existence of the ether, it did the opposite.

See here

Hii ni kanuni ya msingi kabisa.

Ukisoma hadithi za Sir Arthur Conan Doyle na mhusika wake Sherlock Holmes utaona kwamba mara nyingine kile kinachoonekana cha wazi kabisa si kilichotokea, na kile kinachoonekana hakiwezekani kabisa ndicho kimetokea.

Ingawa hilo halimaanishi kwamba kile cha wazi kabisa hakiwezi kuwa ndicho kilichotokea mara zote.

Kuondoa utata unaoletwa na dunia yetu ya sasa yenye mambo lukuki yenye mchanganyiko, uchunguzi ufanywe na ushahidi upatikane. Hata kama kuna njama za kubabaisha uchunguzi makini na kuharibu ushahidi, njama hizi zimulikwe.

Mwishoni penye ukweli uongo utajitenga, na Watanzania si wajinga watajua ukweli ni upi na uongo ni upi.

Lakini mkikimbilia kusema "hawa ni CCM" kabla ya uchunguzi wala ushahidi, hata kama ni kweli hawa ni CCM, watu makini wakiangalia mambo watashindwa kujua kwamba hawa ni CCM kweli au mmechagua kurahisisha mambo magumu tu bila ushahidi wala uchunguzi.

Cooler heads shall prevail to investigate this fully and bring the culprits to justice.
 
Mkuu hiki ni kitendawili na majibu yake yapo; uchaguzi wa madiwani una kipi kikubwa mpaka wauane? na kwanini Arusha? Mbona Iramba na kwingeneko kulikuwa shwari?
Kwa vile mzee wa mipango anatoka Iramba na si Arusha. Arusha ndipo target yake, ukabila ndio msingi wake wa Fikra. CCM hawajaanza leo kuwafuta wachaga kila mahali ktk vita yao ya kuangamiza wachaga....hata Mengi kakumbana sana na haya mambo.....ya hawa wauza nchi wa karne hii.
 
Mimi naweza sema nilikuwa karibu zaidi na mahali bomu lilipolipuka na pia tulikuwa hasra zaidi polisi walivyokuwa wanamkimbiza mlipuaji wakati sisi tulikuwa tunamtaka tummalize hapo hapo
ukiwa na akili unganisha na tukio la mtu aliye Arusha bomu ktk kanisa katoliki Olasiti kwanini mpaka sasa hajakamatwa na polisi!
 
Bomu tena Arusha. Inavyoonekana kulikuwa na njama za kumpata ama Lema au Mbowe. Watu wameumia sana.

mkuu, kuna taarifa hapa jamvini zinasema Mwigulu Nchemba amehama kwa ulinzi kutoka kwenye hoteli aliyokuwa amefikia hapo mjini Arusha. je taarifa hizi ni za kweli?
 

Bomu ya leo itatoa siri nyingi sana....itajibu hadi olasiti....bomu hiyo si ya kutengeneza mitaani...bomu halisi la kiwandani..Na mataifa makubwa yanajua hadi serial numbers na type..Labda kama ni ya china ndipo itakuwa siri.Ila siku yanapiga raia wa kichina ktk migodi haramu China nao watasema kitu.

Hilo bomu km limetok aktk maghala yetu itajulikana, km limetoka somalia pia itajulikana tuu.
 
Kwa nini bomu lilipuke baada ya mkutano na siyo kabla au wakati wa mkutano?.

Kwa nini bomu lisubiri mpaka viongozi wa CHADEMA wamalize kuwapa wananchi ujumbe wa uchaguzi na jinsi ya kupiga kura ndiyo bomu lilipuke?. WHY?.

Nini kilichoko nyuma ya hii SIRI ya kisiasa?.

Kuna maswali ambayo ukiangalia kifikra unapata jibu pamoja na kwamba uchunguzi ni muhimu sana.
 
mkuu, kuna taarifa hapa jamvini zinasema Mwigulu Nchemba amehama kwa ulinzi kutoka kwenye hoteli aliyokuwa amefikia hapo mjini Arusha. je taarifa hizi ni za kweli?

Hata mimi ningekuwa Arusha halafu nikutane naye hata ghorofani ningemtupa atakayekuja mfufua aje fanya hivyo.Keshakuwa burden kubwa sana kwa CCM..Hao jamaa na wanajulika arusha.Watu wa nji ya vumbi huwa wanatakiwa wawe termed kwanza.CCM wamempaisha haraka sana bila kujua watu hao wana mtatizo engi sana ya kisaikologia.

Watoke ktk kuchunguliwa wazai wao wakifanya mapenzi na matusi ya mfululizo hadi kuja ona usataarbu wa mjini si kazi ndogo.Ndio maana alikuwa akimporomoshea matusi Dr. slaa bila hata haya.Ni kawaida sana kwa watoto wa aian ya akina mwigulu kutukana matusi ya nguoni watu wazima.
 

Unajuaje km hakuna vitu vilivyokwamisha timing muda wote hadi pale walipojaribu wawahi kabla hawajaondoka?
 

Yaliyotokea ni mbinu chafu za kuwafanya wapenda Mageuzi wasijitokeze kwenye uchaguzi. MaKamanda lazima tujitokeze kupiga kura kwa wingi ili kuwaaibisha hawa waliopanga hizi mbinu chafu; ukombozi wa nchi hii NI LAZIMA .
 
Arusha. Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa.

Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.

Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.

Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.

Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa bomu hilo lililipuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema, wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua za kumaliza kuhutubia.

Taarifa zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki.

Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani.

Hali hiyo ilifanya barabara zote za mji wa Arusha kujaa watu waliokuwa wakikimbia ovyo.

Hali hiyo ya watu kukimbia ovyo kuliwafanya askari polisi wengi kuingia mitaani kudhibiti watu na hivyo nao kulazimika kutumia mabomu ya machozi hali ambayo ilizidisha taharuki.

Baadhi ya watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na wengine katika Hospitali ya Seliani na wafuasi wa Chadema na watu wengine waliokuwa katika eneo hilo.


Miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo la mlipuko wa bomu ni Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa ambaye amelazwa katika hospitali ya Selian.

Mbowe akizungumza katika hospitali ya Selian jana aliwataka wanachama wa chama hicho watulie kwa sababu tukio hilo ni kubwa na lina mambo mengi ndani yake.

Alisema wanachofanya sasa ni kuhakikisha kuwa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo wanapata matibabu kwanza.

Mbowe aliwataka watu wote waliopotelewa na ndugu kufika katika hospitali zote za mji wa Arusha kutambua ndugu zao waliojeruhiwa.

Alisema Chadema itagharimia matibabu ya watu wote waliojeruhiwa katika tukio hilo.

Mbowe alisema chama chake kwa sasa hakiwezi kutoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo la bomu kwa sababu wanafuatiliwa na baadhi ya askari polisi na maofisa wa Usalama wa Taifa.

Katika hospitali ya Selian, Mganga wa zamu, Dk Ekenywa alisema kuwa hospitali hiyo imepokea majeruhi 25 ambao wanaendelea kupatiwa matibabu.

Waandishi wa habari walishuhudia baadhi ya wanachma wa Chadena pamoja na viongozi wao akiwamo Mbowe wakitoa damu kwa ajili ya majeruhi.

Awali Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana alihitimisha kampeni kwa chopa katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli na kukumbana na mkutano wa kampeni wa CCM uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Edward Lowassa.

Viongozi hao, walifanya mikutano katika kata hiyo na kila chama kilitamba kushinda leo na kuwaondoa wananchi na hofu za kutokea vurugu.

Mbowe licha ya kufanya mkutano huo, pia alifanya mikutano katika Kata ya Kaloleni Uwanja wa Soweto mjini Arusha na mamia ya wakazi wa Arusha wa kata zote nne na mkoani Manyara, katika kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani unaofanyika katika kata mbalimbali nchini.

Uchaguzi mdogo wa kata nne za Jiji la Arusha na Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli, unatarajiwa
Uchaguzi wa Kata ya Makuyuni, unafanyika kuziba nafasi ya Diwani wa CCM, Abdilah Warsama aliyefariki dunia, kata nne za Jiji la Arusha, uchaguzi unafanyika kutokana na waliokuwa madiwani wa Chadema kufukuzwa uanachama kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.

Vyama vilivyosimamisha wanaogombea udiwani ni CCM, Chadema na CUF. Kwa upande wa CCM ni Emanuel Meliali (Kaloleni), Emmannuel Laizer (Elerai), Edna Jonathan Sauli (Kimandolu) na Victor Mkolwe (Themi) .

Chadema wanaogombea ni Melance Kinabo “Kaburu” (Themi), Emmannuel Kessy (Kaloleni), Jeremiah Mpinga (Elerai) na Rayson Ngowi (Kimandolu).

Kwa upande wa CUF waliosimamishwa kugombea ni Abbas Mkindi Darwesh (Kaloleni) John Bayo (Elerai) na Lobora Ndarvoi (Themi).

Kampeni

Kampeni za uchaguzi huo, mdogo, zilikuwa na upinzani mkubwa na kwa Jiji la Arusha, wakati Chadema, ilikuwa ikiongozwa na mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema, CCM iliwatumia vigogo wake wote wa juu wa chama hicho.

Vigogo hao waliokuwa Arusha ni Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Nchemba, Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdalah Bulembo.

Wengine waliokuwa Arusha ni Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwanri, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), Stephen Wassira na wabunge kadhaa wakiongozwa na mbunge wa Simanjiro, Christopha ole Sendeka.

Kata ya Makuyuni

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema jana kuwa chama hicho, kina uhakika wa ushindi katika Kata ya Makuyuni na kata nne za Arusha.

“Tumefanya kampeni kwa amani na utulivu na nina imani ya ushindi mkubwa hasa hapa Makuyuni,” alisema Nangole.

Mbowe katika kata hiyo, jana alifanya mkutano mfupi baada ya kutua kwa chopa, akitokea mkoaniManyara.
Mbowe aliwataka wakazi wa kata hiyo, wasiwe na hofu wajitokeze kupiga kura leo. Kwa upande wa Lowassa, ambaye ameweka kambi katika kata hiyo, pia alitoa wito kwa wakazi wa kata hiyo, kujitokeza kwa wingi kupiga kura leo.

Kwa pamoja viongozi hao ambao walipishana muda mfupi, Mbowe akianza kupita na baadaye Lowassa kuhitimisha mkutano, kila mmoja alitamba chama chake kushinda leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nape alisema chama hicho kina imani na ushindi leo na alipongeza kampeni kuwa za amani.

“Tuna imani polisi wataimarisha ulinzi leo,” alisema Nape.

Nape jana jioni, alitarajiwa kuhitimisha kampeni mkoani Manyara.

Lema akizungumza katika mikutano jana, alisema wana imani Chadema itaibuka na ushindi katika kata zote.
 
Tuachie vyombo vya usalama vifanye kazi yake maana humu kila mtu anaongea la kwake ambalo halina ushahidi wa kutosha. Inawezekana kuna kikundi kinachojihusisha na maswala haya ya ulipuaji wa mabomu mjini Arusha.
 
JF kwa miaka hii ya karibuni imekuwa si sehemu ya great thinkers,wengi ni wakurupukaji na washabiki wanaoongozwa na utashi wa hisia zao.Jambo hili ni kubwa sana na linahitaji umakini pamoja kutoa mawazo yatakayo saidia au kubaini nani yupo nyuma ya matukio haya kikatili.Bahati mbaya watu wanachangia ushabiki na hata kupotosha uhalisia wa jambo lenyewe.Mwingine yupo nje ya nchi,naye anataja fulani anahusika.Wakati mwingine unapata mashaka huyu anayekuwa wa kwanza kumnyooshea kidole fulani anahusika,kwamba pengine yeye ndiye muhusika.Ukweli wakati mwingine unapata uzito kuchangia baada ya kuona wachangiaji wengi wanavyofanya ushabikibr>Poleni majeruhi wote,poleni wafiwa wote
Code:
Code:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…