Bongo aliyenunua gari na kujenga nyumba anajiona ametoboa maisha

Bongo aliyenunua gari na kujenga nyumba anajiona ametoboa maisha

Huku Bongo (TZ) ukijenga nyumba ya 30mil kisha ukinunua gari la kutembelea (i.e: Carina, IST, Mazda, wish, Rav4, Dualis, Spacio, Crown Athlete, Vitz, Runnex, n.k) tayari unaonekana umetoboa maisha. Pengine hata wewe mwenyewe utajiona una akili ya maisha kuliko kiumbe chochote hapa nchini ambacho hakikufanya hivyo.

Ukisimama mbele ya masikini wenzako wanakuita TAJIRI. Hata kama haikuwa desturi yako kuvaa mkanda nje (kuchomekea sharti), sasa utaanza kuvaa hivyo ili watu waone ufunguo wa gari ukiwa umeuning'iniza kwenye suruali.

Right Marker
Dar es salaam​
Ardhi ni utajiri namba moja. Kama unamiliki kipande cha ardhi, elimu, afya ya mwili, akili na Roho inatosha kutamba mjini na vijijini.
 
Nyumba au gari sio sawa na makalio ambayo kila mmoja anayo. Kujenga ni sawa na kuzika hela ardhini na sio kila mmoja mwenye ujasiri huo.
Hakuna kitu kizuri kama kujihakikishia kuwa familia yako itakuwa na sehemu salama ya kuishi bila usumbufu siku ukitwaliwa katika huu Ulimwengu. Hela yangu ya kwanza kubwa kuipata sikufikiria mara 2 zaidi ya kujenga.

Sasa hivi i am happy kuwa familia yangu ina permanent address.
Mengine ni mapenzi ya Mungu
Je unafikiri ni sahihi MTU mwenye mshahara pekee kukopa kuanza kujenga nyumba ya gharama kubwa ya kuishi
 
Huku Bongo (TZ) ukijenga nyumba ya 30mil kisha ukinunua gari la kutembelea (i.e: Carina, IST, Mazda, wish, Rav4, Dualis, Spacio, Crown Athlete, Vitz, Runnex, n.k) tayari unaonekana umetoboa maisha. Pengine hata wewe mwenyewe utajiona una akili ya maisha kuliko kiumbe chochote hapa nchini ambacho hakikufanya hivyo.

Ukisimama mbele ya masikini wenzako wanakuita TAJIRI. Hata kama haikuwa desturi yako kuvaa mkanda nje (kuchomekea sharti), sasa utaanza kuvaa hivyo ili watu waone ufunguo wa gari ukiwa umeuning'iniza kwenye suruali.

Right Marker
Dar es salaam​
Tafuta hela kijana.

Hayo mafanikio tosha kabisa.
 
Kujenga na kumiliki usafiri ni sehemu ya success Kwa Tanzania

Maana hali ya Umasikini ni kubwa miongoni mwetu.

Baadhi ya Wazee wetu, hadi wametangulia mbele za haki hawakufanikiwa kununua hata Kiwanja cha 20x30

Kwanini usitembee kifua mbele Kwa kufanikisha hilo??
 
Mafanikio ni swala pana. So inategemea hali uliokua nayo awali na ulipo kwa wakati husika.
Kwa mfano unaweza kuta mtu kwao kakulia kwenye nyumba ya udongo na shule amesomea 2km umbali kutoka nyumbani na anaenda kwa miguu kila siku, sasa mtu kama huyo akijenga nyumba ya milion 30 na kagar ni mafaniko makubwa sana kwake ila kwa mtoto wa mengi au bakhresa kwao mafanikio ni vitu tofauti na hivyo.
Kama umewahi kushiriki social surveys, mfano unakwenda kwenye Kijiji au mtaa X kwa lengo la kujua hali za maisha za watu (wealth ranking) vigezo vikuu vya kubaini madaraja ya watu kiuchumi au levels za umasikini ni pamoja na umiliki wa mali/vitu mfano: mtu ana nyumba (ya aina gani? Ya tope na nyasi? Tofali na bati?), usafiri anao ( baiskeli, pikipiki, gari etc), ana redio,Tv, stuli, makochi? Ana shamba au anakodisha? Kama analo shamba ekari ngapi? Kiufupi umiliki wa mali ni indicators muhimu sana, na ndiyo maana hata benki ukikopa wataangalia una dhamana gani?? Mwisho kabisa kwa karne hii tuliyopo ilitakiwa walau watanzania asilimia 70 wawe wanamiliki walau gari ndogo. Sijawahi kujua ni kwa nini serikali haitaki watu wake wamiliki magari kwa kigezo cha kuweka ushuru mkubwa sana wa kuingiza magari.
 
Back
Top Bottom