Bongo aliyenunua gari na kujenga nyumba anajiona ametoboa maisha

Ardhi ni utajiri namba moja. Kama unamiliki kipande cha ardhi, elimu, afya ya mwili, akili na Roho inatosha kutamba mjini na vijijini.
 
Je unafikiri ni sahihi MTU mwenye mshahara pekee kukopa kuanza kujenga nyumba ya gharama kubwa ya kuishi
 
Tafuta hela kijana.

Hayo mafanikio tosha kabisa.
 
Kujenga na kumiliki usafiri ni sehemu ya success Kwa Tanzania

Maana hali ya Umasikini ni kubwa miongoni mwetu.

Baadhi ya Wazee wetu, hadi wametangulia mbele za haki hawakufanikiwa kununua hata Kiwanja cha 20x30

Kwanini usitembee kifua mbele Kwa kufanikisha hilo??
 
Kama umewahi kushiriki social surveys, mfano unakwenda kwenye Kijiji au mtaa X kwa lengo la kujua hali za maisha za watu (wealth ranking) vigezo vikuu vya kubaini madaraja ya watu kiuchumi au levels za umasikini ni pamoja na umiliki wa mali/vitu mfano: mtu ana nyumba (ya aina gani? Ya tope na nyasi? Tofali na bati?), usafiri anao ( baiskeli, pikipiki, gari etc), ana redio,Tv, stuli, makochi? Ana shamba au anakodisha? Kama analo shamba ekari ngapi? Kiufupi umiliki wa mali ni indicators muhimu sana, na ndiyo maana hata benki ukikopa wataangalia una dhamana gani?? Mwisho kabisa kwa karne hii tuliyopo ilitakiwa walau watanzania asilimia 70 wawe wanamiliki walau gari ndogo. Sijawahi kujua ni kwa nini serikali haitaki watu wake wamiliki magari kwa kigezo cha kuweka ushuru mkubwa sana wa kuingiza magari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…