Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,263
- 18,201
Kwa hiyo kwa kua Priyanka hakusomea ndio maana mnaokota tu watu kisa wana makalio makubwa na wanaume wakishanyoa viduku na hereni mnawapa scene mwendo mdundo,Daaah yaaani wewe wa kuniuliza mimi elimu ya priyanka chopra? Wenzio hayo mambo ndo tunafanyia presentation.
Priyanka hajasomea film. Alikuwa mrembo na baada ya kushinda tu miss world Abbas akumuita kufanya nae movie 2002. Yaaani infact hakwenda ata chuo.
Priyanka hakusomea ila ameshindwa kuelezea elimu yakeKwa hiyo kwa kua Priyanka hakusomea ndio maana mnaokota tu watu kisa wana makalio makubwa na wanaume wakishanyoa viduku na hereni mnawapa scene mwendo mdundo,
Kuna muigizaji mmoja alikua anajisifia kila mwezi anatoa movie, hahaha unategemea matazamaji atapata kitu gani hapo?
Anadhani Priyanka aliishia darasa la nane kama dada zake anaofanya nao kazi, hapo anataka kumfananisha Priyanka na Wema Sepetu kisa wote walikua maMiss, anashindwa kuangalia education backgrounds zao.Priyanka hakusomea ila ameshindwa kuelezea elimu yake
Ndio maana mwaitwa vilaza, ukisikia make up unadhani ni kupaka poda tu, make up artist ni kipengele kikubwa sana, hizo movies za wenzetu uzionazo mfano za kutisha sio wote wanavaa masks au zamani tuliaminishwa ni computer, kuna wengine ni make up tu, mfano kaangalie movies za Guardians of the Galaxy, yule Drax mwili wake kua na michoro michoro vile ni make up ilipakwa 3 hrs, yule Gamora ile rangi ni make up pia, kuna Joker, na wasanii wengine wengi tu,
Usimchukulie poa make up artist katika kiwanda cha movie.
Na siku hizi sijui wamegundua nini, cheating mwanzo mwisho, huyu kam cheat yule, yule kamcheat huyu wake na waume za watu.
Anzeni kutengeneza movies nzuri hizo foleni zitakuwepo sasa mwataka tupange foleni kuangalia vile mnavyongonoka?rodrick alexander ROBERT HERIEL
Tatizo kubwa la cinema za bongo ni technical issues,
ma director ni wabovu sana.pamoja na
Art Direction,
Visual Effects ,
Scripting,
editing,
choreographers,
Back ground score,
music compose,
sound designer,
Sound Recorders,
Costume Designer,
Production Designer,
Cinematography,
Stunt Directors
na hayo ndio maeneo yanayohitaji watu wenye elimu mana ni sehemu za kitaalamu. Waweza kuta mambo yote hayo yanafanywa na mtu mmoja tu, we umesikia wapi yanafanyika hayo Zaidi ya bongo?
Kuwashutumu ma Actors sio suluhishi kabisa, amini mkuu hata tumlete Robert Di Nero kwa watengnezezaji filamu wa bongo nae tutamuona utopolo tu. acting ni kipaji, pamoja na ile hali ya mtu kuwa willing kujifunza mambo mapya kila siku, cheti cha darasani hakimati kabisa kwenye acting, ni just formalities course zakupitia kwa ajili ya kujielewa tu, ni kama vile football players au coaches waweza kuta David Moyes alipasi vizuri darasani kuliko Pep Guardiola, ila tizama hali halisi ya kwenye kazi zao.
Kukosekani kwa fedha ndio msingi wa tatizo kubwa na huku support kutoka kwenye serekali likiwa ndio tatizo kuu.
Yani hiyo hali iliyonayo Bongo movie bado serekali utakuta wana force kupata tax wakati ni mambo yanayohitaji kupata muda mpaka yasimame vizuri, naamini wapo ma financers Zaidi wahindi wanaotamani kuekeza kwenye hii tasnia lakini wanaogopa TRA isije ikapata sababu ya kuwaona kama jamaa kumbe fedha ipo wakaanza kuwasumbua.
Bila ya uwekezaji mzuri na serekali kutoa support hapawezi kuwa na mabadiliko. Hivi hata kuvaa uniform za Polisi au jeshi hawaruhusiwi.
Na jengine kubwa ni kuwa, bila ya kupata support kutoka kwa wananchi ni ngumu sana tasnia kuinuka, hata hao waekezaji wakijitokeza bila yakua na return ya wanachokiekeza ni bure kabisa, Sinema za Nigeria na India zimeinuka kutokana na kupata support kutoka kwa wananchi wao, Bongo biashara ni zero Zaidi ya kuishia kuwasukumia matusi.
Hivi ni lini tutakuta foleni kuelekea ndani ya Cinema Hall tukiwa tumejipanga tunakwenda kutizama bongo Movie? tutakapofika hatua hiyo basi mabadiliko lazima tutayaona.
Hili wazo zuri sanaaa, naam kama wanaibiwa na CCM au wanakandamizwa na CCM basi ni muda muafaka sana kutoa igizo linalohusu hayo manyanyaso hiyo ndio kazi ya Fasihi, kufikisha ujumbe kwa jamii.Toeni basi movie ya kuonyesha mfumo na ccm wanavyowaatiri vinginevyo mtabaki kuchangishana rambirambi na kuibiana maana hicho ndio mnakiweza
Kwa hiyo kwa kua Priyanka hakusomea ndio maana mnaokota tu watu kisa wana makalio makubwa na wanaume wakishanyoa viduku na hereni mnawapa scene mwendo mdundo,
Kuna muigizaji mmoja alikua anajisifia kila mwezi anatoa movie, hahaha unategemea matazamaji atapata kitu gani hapo?
Mkuu suala la acting ni uwanja mpana sana, kupasi vizuri chuoni hakukutoshelezi wewe kuwa ni muigizaji mzuri.
Kuna movie ya kijeshi imeigizwa kiporipori nimeisahau mkuu.Mkuu naomba unitajie jina la hiyo muvi ambayo koplo anampigia saluti koplo au ni mwigizaji gani aliigiza kwa hiyo movie ili niitafute.
Tusije tukawa tunaongelea vitu ambavyo havipo ili tu tufurahishe umma
Watanzania aisee! kipindi industry inafanya vizuri na kina kanumba wapo hawa waigizaji ambao mnasema hawajasomea mbona mlikuwa hamsemi. Uigizaji sio udaktari. NI UFUNDI KAMA KUSHONA NGUO. Mimi naweza kukutajia waigizaji mia ambao hawajasomea na wanaigiza vizuri tu.
Cha pili amna msomi aliyekatazwa kuingia kwenye industry kama wewe ulikutana na wawili watatu thats you mimi najua watu wengi wamemaliza elimu zao na wako kwenye industry. Pambana acha kulalamika humu.
Kitu cha pili
CCM ndio wanawafundisha nyie kuigiza? Mbona ngono mnazipatia? Nchi hii ni kubwa sana yaan mmeshaizunguka koooote mkatafuta hata stories za makabila flan mkaigiza? Kuna locations chungu nzima mnashindwa kwenda huko mkaigiza muachane na locations za mahotelini? Big budget gani, watu wanasema hamna ubunifu, stories zenu ni zile zile za mapenzi na uchawi, waigizaji hawana viwango, mnajali makalio na hereni za kuning'inia na make ups kama clowns,
Mpishe wasomi waliosomea tasnia hiyo wapige kazi na wao, sura zenu haziuziki tena.
Tunalalamika sie au nyie? Mngekua mnafanya kitu cha kuonekana hata serikali ingewekeza.
Mkuu umeongea ukweli mtupu hawa watu lazima wawe na utaalamu kuhusu fani husika.
Kama mtu anaigiza udaktari basi aigize kweli aelewe mambo muhimu ya udaktari juu ya script anayocheza.
Sio unaigiza daktari alafu umevaa nguo za nesi.
Kama mtu anaigiza polisi kweli awe na taaluma kuhusu upolisi,sio polisi wa kituoni na nguo zake za kaki ati ana ndevu wakati polisi wale hawatakiwi kufuga ndevu.
Sio polisi wawili wameenda kukamata kila polisi anamwita mwenzie afande wakati kijeshi lazima kuna mmoja atakuwa senior na mwingine mdogo
Sio mtu anaigiza movie ya kijeshi ati private wa jeshi anampigia saluti coplo wa jeshi jambo ambalo halipo na ni upuuzi.
Kiufupi wanaigiza kama watoto wadogo vile wakati wenzetu huko nje unajiuliza ni kweli ama maigizo wakati huo hapa bongo unaona kabisa hapa ni changa la macho.
Wanachofanya bongo movie ni kutudanganya hata juu ya wanachoigiza,yaani huwezi kujifunza kitu cha ukweli kwenye movie za bongo
Coplo kumpigia saluti coplo ni uongo kiuhalisia haipo hivyo kwa hiyo movie zetu wanatudanganya na ndo wanazidisha ujinga kwenye jamii kwa kuwaigizia watu jambo ambalo silo.
Kwenye mapenzi oooooh wanajua kuigiza sana hasa ukikuta mwanaume the way anareact akiona demu mwenye chura utaona kabisa ni kama wamekuona wewe lakini wapii they are experts katika hiyo sector ya mapenzi na ngono.
Nilishawahi kuwaza na mimi nije kuwa muigizaji ili nielimishe jamii juu ya mambo mbali mbali ya Nchi hii kwa kuigiza kitu cha ukweli kutokana na wao kuharibu tasnia hii lakini ndo nina malengo mengine tofauti na uigizaji.
Kheee wewe acha kupotosha watu. Unaposema wanatumia bajet ya kawaida unamaanisha nini?
Hivi unajua series ya korea "kingdom" walikuwa wanatumia bajeti ya 1M Usd per EPISODE!
Mkuu unajua series ya Gu Family Book featuring Lee Seungi walikuwa wanatumia kiasi gani kwa episode moja?
Nigeria? Niambie mara ya mwisho kuangalia movie MPYA kutokea nigeria ilikuwa ni lini?
Acha kupotosha watu mkuu. Fatilia vitu kabla ya kuandika hapa.
Steps alibanwa sababu ya kukwepa kodi na mbaya zaidi alikuwa anaibia mpaka wenye movies, alikuwa anawakata asilimia 5 anasema analipa serikalini wakati halipiNimekuuliza hizo filamu unazozisema tukishatengeneza kwa bajeti unayoisema wewe tunaonyesha wapi ili turudishe faida unazunguka tu.
How Do we Distribute our movies if the government banned STEPS and haikuja na solution yoyote?
Alafu acha kujikaririsha ujinga inaonekana hata filamu zenyewe huangalii
Unaongea vitu kirahisi sana kwamba unazunguka tu paaap movie imetoka wakati we mwenyewe unalalamika hupewi nafasi. Nijibu movie tutasambaza wapi turudishe faida?
Hizo ndizo fikra zenu za kimaskini, unauliza watamuuzia nani, Kuna mtu haangalii kitu kizuri?, hebu fanyeni hivyo muone kama hamtopata wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi,
Kama mnaweza kukopeshana pesa hadi kufikia hatua ya kutukanana matusi ya nguoni kwanini msiungane mkachukua mkopo bank na kufanya mambo makubwa?
Angalieni wenzenu wa Bongo flavor wanavyojitahidi, sasa hivi hadi Wamarekani wameanza kufanya collabo na Waafrica baada ya kuona hatusikilizi tena miziki yao tupo busy na ya kwetu, kwanini Bongo movies msibadilike kama Bongo flavor? Na kama hamuwezi basi mtuachie fursa sie wapya tufanye mapinduzi lakini bado mnatubania,
Aibu yenu.
Industry ya Bongo haijawahi kufanya vizuri Budah, sema zipo baadhi ya Movie zilijitahidi, na hiyo ni kutokana na sababu kuwa kipindi hicho jamii ilikuwa gizani, wenye elimu walikuwa wachache, wenye Tv walikuwa wachache, Hapakuwa na Smartphone ambazo zingelinganisha kazi zetu na za kigeni.
Huoni mambo yamebadilika sasa, wewe darasa la pili utaigiza jambo gani kuifundisha jamii hii ya utandawazi zaidi ya vichekesho vyako?
Nimekuuliza hizo filamu unazozisema tukishatengeneza kwa bajeti unayoisema wewe tunaonyesha wapi ili turudishe faida unazunguka tu.
How Do we Distribute our movies if the government banned STEPS and haikuja na solution yoyote?
Alafu acha kujikaririsha ujinga inaonekana hata filamu zenyewe huangalii
Unaongea vitu kirahisi sana kwamba unazunguka tu paaap movie imetoka wakati we mwenyewe unalalamika hupewi nafasi. Nijibu movie tutasambaza wapi turudishe faida?
Hizo ndizo fikra zenu za kimaskini, unauliza watamuuzia nani, Kuna mtu haangalii kitu kizuri?, hebu fanyeni hivyo muone kama hamtopata wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi,
Kama mnaweza kukopeshana pesa hadi kufikia hatua ya kutukanana matusi ya nguoni kwanini msiungane mkachukua mkopo bank na kufanya mambo makubwa?
Angalieni wenzenu wa Bongo flavor wanavyojitahidi, sasa hivi hadi Wamarekani wameanza kufanya collabo na Waafrica baada ya kuona hatusikilizi tena miziki yao tupo busy na ya kwetu, kwanini Bongo movies msibadilike kama Bongo flavor? Na kama hamuwezi basi mtuachie fursa sie wapya tufanye mapinduzi lakini bado mnatubania,
Aibu yenu.