rodrick alexander ROBERT HERIEL
Tatizo kubwa la cinema za bongo ni technical issues,
ma director ni wabovu sana.pamoja na
Art Direction,
Visual Effects ,
Scripting,
editing,
choreographers,
Back ground score,
music compose,
sound designer,
Sound Recorders,
Costume Designer,
Production Designer,
Cinematography,
Stunt Directors
na hayo ndio maeneo yanayohitaji watu wenye elimu mana ni sehemu za kitaalamu. Waweza kuta mambo yote hayo yanafanywa na mtu mmoja tu, we umesikia wapi yanafanyika hayo Zaidi ya bongo?
Kuwashutumu ma Actors sio suluhishi kabisa, amini mkuu hata tumlete Robert Di Nero kwa watengnezezaji filamu wa bongo nae tutamuona utopolo tu. acting ni kipaji, pamoja na ile hali ya mtu kuwa willing kujifunza mambo mapya kila siku, cheti cha darasani hakimati kabisa kwenye acting, ni just formalities course zakupitia kwa ajili ya kujielewa tu, ni kama vile football players au coaches waweza kuta David Moyes alipasi vizuri darasani kuliko Pep Guardiola, ila tizama hali halisi ya kwenye kazi zao.
Kukosekani kwa fedha ndio msingi wa tatizo kubwa na huku support kutoka kwenye serekali likiwa ndio tatizo kuu.
Yani hiyo hali iliyonayo Bongo movie bado serekali utakuta wana force kupata tax wakati ni mambo yanayohitaji kupata muda mpaka yasimame vizuri, naamini wapo ma financers Zaidi wahindi wanaotamani kuekeza kwenye hii tasnia lakini wanaogopa TRA isije ikapata sababu ya kuwaona kama jamaa kumbe fedha ipo wakaanza kuwasumbua.
Bila ya uwekezaji mzuri na serekali kutoa support hapawezi kuwa na mabadiliko. Hivi hata kuvaa uniform za Polisi au jeshi hawaruhusiwi.
Na jengine kubwa ni kuwa, bila ya kupata support kutoka kwa wananchi ni ngumu sana tasnia kuinuka, hata hao waekezaji wakijitokeza bila yakua na return ya wanachokiekeza ni bure kabisa, Sinema za Nigeria na India zimeinuka kutokana na kupata support kutoka kwa wananchi wao, Bongo biashara ni zero Zaidi ya kuishia kuwasukumia matusi.
Hivi ni lini tutakuta foleni kuelekea ndani ya Cinema Hall tukiwa tumejipanga tunakwenda kutizama bongo Movie? tutakapofika hatua hiyo basi mabadiliko lazima tutayaona.