Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

Daah hawa viongoz ni shidaa una muweka mtu kwenye Cage amekua ndege?
Ukiachana na Rais mwnyewe, nchi hii Hakuna mtu huru.


Hata wabunge wa CCM hawana Uhuru na amani.

Ukitaka kuongea ukweli bungeni, tayari Kuna speaker wa mchongo atakudili hata kukufukuza, ingawa kwa utaratibu speaker alipaswa kuchaguliwa na wabunge na kuwa chini ya wabunge.

Kuna wakati, sheria ilitaka kubadilishwa (sijui Kama walibadili), ili mtu aweze kugombea Ubunge, urais au udiwni inabidi uwe mwanachama wa chama unachotaka kugombea kwa mwaka mmoja.

Tafsiri yake ni kuwa, MwanaCCM akikatwa ndani ya chama asihamie chama kingine akawasumbua.

Uoga uliozidi kiwango.

Hata suala la kukataa KURUHUSU MGOMBEA BINAFSI, ni uoga.


Kwasababu wanaona watashindwa kudhibiti watu.
 
Huo ndiyo ukweli ingawa mchungu! Vigogo wa CCM wanapenda kudhibiti wenzao kwa maslahi ya matumbo yao!
 
Kwa hiyo huyo mtoto atakuwa Muingereza na Mtanzania bila kunyimwa haki zake bongo? au sio hana haja ya special status ya kimchongo??
 
Uraia pacha uruhusiwe ila uwekewe masharti maalumu ili kuzuia wale raia especially wa kigeni wanaoweza tumia fursa hiyo kuja kuchuma rasilimali na kukimbia.

Hiyo hadhi ya uraia pacha mimi napendekeza iwe kwaajiri ya watanzania wa kuzaliwa hapa Tanzania ambao ni waafrika na ancestors wao wamezikwa katika ardhi ya Tanzania vizazi 8 nyuma kutokea yeye, yaani babu wa mababu wa sita na bibi wa mabibi sita awe alikuwa mtoto wa hapa Tanzania kwa kuzaliwa.


Hawa kanjibia tuwe nao makini sana watachuma sana rasilimali hapa na kufilisi taifa.
 
Urai pacha ni muhimu kwa maendeleo ya taifa, kwani kuna watanzania kibao wapo nje wanatamani kuleta uwekezaji Tanzania wanashindwa kwa sababu ya gharama za kuja kama wawekezaji bado masuala ya ununuzi wa ardhi
Hili swala la ununuzi wa ardhi litaleta shida sana. Kuna watu huko nje watakomesha kwa kununua maelfu ya heka halafu wanayahodhi kimya na kufanya wengine wakose hata sehemu ya kufanyia shughuli za kilimo na ufugaji na ndio mwanzo wa uharibifu wa mazingira.

Me nadhani wawezeshwe kuwekeza kwenye maeneo yaliyopo mfano real estate. Kununua hisa za makampuni ya real estate. Kuwekeza mitaji ya kampuni,kuwekeza kwenye elimu mfano kujenga shule za kisasa zenye teknolojia ya hali ya juu, uwekezaji kwenye miundo mbinu kama kupewa ruhusa ya kujenga barabara ambazo zitakuwa zinalipiwa watu kupita. Kuwekeza kwenye sekta ya umeme, etc


Hili swala linataka umakini sana.
 
True mkuu.
 
50Cent mwenyewe babu na bibi yake walikuwa wenyeji wa Kilwa kivinje. So ni mtanzania by asili.
 
50Cent mwenyewe babu na bibi yake walikuwa wenyeji wa Kilwa kivinje. So ni mtanzania by asili.
Na ndugu zake wamekosa fursa ambazo angependa kuwekeza kutokana na sheria hii!
 
Uraia Pacha.... ? No Problem am a Globalist na Binafsi naona Dunia kama kijiji na mtu anaweza kuishi popote na kupaita ni kwake...

Kwamba Uache kuwekeza Sehemu au usifanye lolote sababu hauna Kijitabu kinachosema wewe ni raia wakati huko ndipo ulipozaliwa ? (well hata ukipewa hilo karatasi huenda deep down hauna attachment na hio sehemu; just a mercenary....; Which is not bad so long as the end justifies the Means....
 
Acha uoga
 
Mkikubali uraia pacha basi mkubali na ushoga kuruhusiwa inchini..

Hivi mtu ana uraia wa inchi zinazokubali ushoga unaweza kumuhukumu na kumfunga kwa hapa tanzania?


Jibu ni BIG NO...
 
Mkikubali uraia pacha basi mkubali na ushoga kuruhusiwa inchini..

Hivi mtu ana uraia wa inchi zinazokubali ushoga unaweza kumuhukumu na kumfunga kwa hapa tanzania?


Jibu ni BIG NO...
Mtu akitenda jinai anahukumiwa kwa mujibu wa sheria bila kujali uraia wake!
 
Wanaofolisi taifa ni wabongo wenyewe na kwenda kuficha mali Dubai na mauricius
 
Madhara ni ardhi yote nzuri watachukua wageni na tunaweza kuja kutawaliwa na mamluki nusu mtz nusu muingereza, hatufungulii mlango mabeberu
hili watu hawalioni........
na tunaweza kuwa na mawaziri nusu watanzania, nusu wamarekani...... sijui wata-serve interest za nani
 
hili watu hawalioni........
na tunaweza kuwa na mawaziri nusu watanzania, nusu wamarekani...... sijui wata-serve interest za nani
Hadi sasa bila hata kuwa na uraia pacha bado kuna mawaziri wana-serve interest zao na za wawekezaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…