Bora kuolewa na mzee aliyejipanga kimaisha kuliko kuolewa na kijana maskini mwenzio

Bora kuolewa na mzee aliyejipanga kimaisha kuliko kuolewa na kijana maskini mwenzio

Bila kupepesa macho wewe ni CHOMBO CHA STAREHE na sio vinginevyo
 
Jukumu la boyfriend ni kukupa mapenzi (upendo) tu,hayo mengine binti ni ya wazazi na walezi wako-Aunt sadaka,mshauri wa mahusiano,malezi na ndoa
 
Maisha yetu ni mafupi sana hapa duniani, hivyo tunapaswa kufurahia maisha muda wote. Hii habari ya kuoana na mtu eti mchume wote baadaye mtafurahia maisha haikubaliki. Maana hakuna aliye na mkataba na Mungu, unaweza ukafa the next morning.

Na kwa taarifa yako furaha na umaskini havikai pamoja, ni kama maji na moto. Ukiolewa na maskini maana yake ni kwamba umeipiga teke furaha ktk maisha yako. Asikwambie mtu, pesa ndiyo sabuni ya roho.

Kama huna hela utalala sehemu yenye uvundo kama banda la beberu la mbuzi. Huyo mume wako maskini anakuwa amelala huku akikoroma maana amechoka utadhani yuko ICU (ndiyo maana ya mlalahoi). Mate
yanamtoka na kulowesha godoro unaweza kudhani kakojolea.

Utajikuta tu unaamka na kuanza kulia kwa uchungu huku ukimuuliza Mungu; why me? Maisha haya mpk lini?

Na kuna ndharia mpya kuwa maskini hatauona ufalme wa Mungu. Kwasabb kila siku anatenda dhambi ya manung'uniko. Maskini hana shukurani kwa Mungu wake. Kila siku akijisogeza mbele za mola wake anaorodhesha maombi zaidi ya mahitaji yake kwa Mungu. Lkn tajiri kila siku anamtukuza na kumshukuru kwa hatua aliyopiga. Ndiyo maana hisikii tajiri akiangushwa na pepo wachafu.

Umaskini ni ugonjwa. Kwann ? Umaskini husababisha magonjwa ya kizembe na kupelekea mtu kufa kizembe.

Usikubali kuolewa na maskini.

UPDATES;
Nimesoma comments zenu zote. Lakini nasema hivi "Mm sitaki kuteseka duniani na ahela. Yaani niiishi kwa shida kisa eti nampenda kidudu-mtu asiye na hela. Naanzaje kwanza? Ujana wako wa kimaskini peleka kuchanganya zege huko!!"
Kweli
 
Mwanamke siku zote ni mpumbavu,kama huyu hawazi kujipigania atoke kwenye umaskini anawaza kuolewa na tajiri
 
Usishangae To yeye
Wapo wanawake wa Aina iyo
utaskia wakisema
"Niolewe TU mie, maisha yameshakua magumu mtaani"
Wako sahihi. Sasa ukimbie maisha magumu mtaani uende kwa mnuka jasho? So bora uendelee ku-hustle peke yako!!?
 
Kasikilize nyimbo ya Ngwair ft Lady jdee inaitwa kama demu sikiliza.
Huo utabqkia kuwa wimbo tu. Mm naongelea uhalisia. Mume maskini HAPANA.

No money no mapenzi
No money no furaha
No money no pepo
 
Huo utabqkia kuwa wimbo tu. Mm naongelea uhalisia. Mume maskini HAPANA.

No money no mapenzi
No money no furaha
No money no pepo
Iko hivi kama hujui
Tajiri anaoa tajiri mwenzake. Hapa anaangalia kwa mke wake wanahela au ni masikini? Akioa mwanamke kwao ni masikini, baba yake, mama yake, wadogo zake na ndugu zake watamtegemea kwa kuanzia kula mpk elimu. Shida haziishi.
Wanawake wenye ndoto ya kuolewa na tajiri halafu kwao ni masikini huishia kugongwa na kuachwa.
Masikini na masikini. Hapa wote maisha ya kuunga kuunga ndiyo wanaoana
 
Yaani mtu hata hela ya kula inakupiga chenga, hao wazee wenye hela utakutana nao wapi? Ukiacha yule wa machache ni wanawake wangapi wameolewa na vizee vyenye hela huku wao hawawezi hata kuingiza hela? Wazee wenye hela wana viwanja vyao ,ili uwapate lazima.na wewe uwe unajiweza.
 
Back
Top Bottom