BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!

Ila kweli ni ushenzi.
Hii mikopo imewahi kuninyoosha mda fulani.
Jamaa ni freemasons. Kujinasua kunahitaji maombi mazito
 
Naunga mkono hoja...jamaa wanatia watu umaskini aisee yaani ni hawafai kabisa
 
Hawa wanaweza sababisha msongo wa mawazo,presha na hata kujinyonga
Madhila katika jamii ya watu ni makubwa mno kuliko faida
Kwa ufupi Hawa ni blackmail .
Na wale wabongo ukiwa mlipaji mzuri usipokopa tena wanakuchezea mchezo kuwa unadaiwa. Mpaka uwape Chao ndipo wanakuclear.
Kwakweli hii mikopo ni kiza nene.
Walinitesa ingawa ilinipa influence kwenye mambo fulani. Mwisho nikasema potelea pote silipi. Tukamalizana kibabe
 
Hahahaa..uliwablock au? Maana kuwakimbia walikua wanatuma sms kwa watu wote inbox
 
Ni kweli kabisa hawa jamaa ni Blackmailers , wanakupa mkopo ambao unaonyesha katika APP yao ni siku saba lakini ikifika siku ya tano saa kumi na moja alfajir wanaanza kukupigia simu kukudai kwa vitisho kuwa usipolipa mpaka saa nne asubuhi basi watawambia jamaa zako wote walio katika phone book yako ! Ikifika saa nne asubuhi wanapiga tena ! Ukiwaambia baado wanakwambia alaa kumbe hutujui eti !?? hazipiti dakika kadhaa utaanza kuona jamaa zako wanaanza kukupigia simu kukuuliza vipi ? Hawa wanatupigia simu na kutuma message eti umetapeli hutaki kulipa , je ni kweli ???? Ninachomaanisha ni kuwa wana kublackmail kwa vitisho ili uwalipe hawa jamaa ni balaa na kwa kuwa wana access ya simu yako wakati mwingine wana screenshot message za mapenzi au madeal unayofanya na watu wanakutumia halafu wanaakuuliza vipi tuwatumie jamaa zako au mkeo ??? Au unalipa ??? Ni blackmail ya hali ya juu iliyo vuka mipaka ! Wana hack simu yako wanawajua wapenzi wako wanawataja kwa majina ! wana monitor simu yako kama imeingiza pesa au imelipa pesa na wanakwambia kabisa mbona una pesa kwenye simu yako kiasi kadhaa ??!!
Kwa kifupi jamaa wana hack simu yako na kila taarifa ya simu yako wana kuwa nayo kiganjani !
 
Duuh hii kali aisee sijawahi isikia. Mi nimeiskia ya kuwapigia watu simu na kuwatumia texts na picha za IDs. Hawa jamaa ni wahalifu,haiwezekani kudai umfanyie mtu hivi hata kama kashindwa kulipa
 
Hahahaa..uliwablock au? Maana kuwakimbia walikua wanatuma sms kwa watu wote inbox
Nilichukua course ya ku deal nao kama wiki 2 hivi. Nikawazima kama taa.
App moja tu sijui nilikosea nini wakanibana nikalipa laki yao.
Wengine mpaka leo sijawalipa. App moja ya MLOAN tarehe 01.9.2024 ilikuwa kama 2.5ml
Bongo pesa 1 ml.
Wengine vilaki laki.
 
Nakazia hapa, serikali chukueni huu ushauri
 
WATU WASHAZALILIKA HAISAIDIII

NILIWAAMBIA KUNA SIKU NDUGU JAMAA ZAOO
WATAGUSWAA NA HIZI MSG WATAJUA UMUHIMU WA VILÌO VYETU

WEE TOKA APRI.MARCH.MAY.JUNE JULY AUG SEPT NDIO MNAONAA EEHEEEEEE

NA WAENDELEEE HIVIHIVIII KUTUZALILISHA TUKAE SAWA
 
WATU WASHAZALILIKA HAISAIDIII

NILIWAAMBIA KUNA SIKU NDUGU JAMAA ZAOO

WATAGUSWAA NA HIZI MSG WATAJUA UMUHIMU WA VILÌO VYETU

WEE TOKA APRI.MARCH.MAY.JUNE JULY AUG SEPT NDIO MNAONAA EEHEEEEEE

NA WAENDELEEE HIVIHIVIII KUTUZALILISHA TUKAE SAWA
Saizi hadi wabunge wanatumiwa SMS za jamaa zao kuwa ni matapeli wamegoma kulipa
 
Kumbe ni ishu ya hivi karibuni tu hahahaaa. Itakua wanajipanga waje na mashambulizi upya dadadeki maana hawawezi kubali kirahisi pesa mingi hivyo. Watu wamedhalilishwa kwa pesa ndogo mno hata 50k haifiki. Toa codes ya hiyo course saidia na wengine maana serikali haijali na kila siku tunapata sms eti tumemdhamini fulani kisa tu kakusave kwenye namba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…